Sudan kumkabidhi Omar al Bashir kwa Mahakama ya ICC

kimsboy

JF-Expert Member
Oct 17, 2016
8,991
17,888
Ikiwa imepita miezi 18 sasa tangu serikali ya muda ya Sudan iafiki kumkabidhi mtawala wa zamani wa nchi hiyo, Omar Hassan al Bashir, kwa Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC), Waziri wa Masuala ya Federali wa Sudan ametangaza kuwa, Khartuom imechukua uamuzi wa kumkabidhi al Bashir kwa mahakama hiyo.

Buthaina Ibrahim Dinar Waziri wa Sudan wa Masuala ya Federali amewaambia waandishi wa habari kuwa, serikali imeamua kumkabidhi Omar al Bashir, rais aliyepinduliwa wa Sudan, pamoja na wahalifu wengine kwa mahakama ya ICC.

Wakati wa safari ya ujumbe wa Mahakama ya Kimataifa ya Jinai mjini Khartoum mwezi Februari mwaka jana, Fadhil Muhammad Saleh aliyeuwa msemaji wa serikali ya Sudan alitangaza kuwa, Khartoum imekubali suala la kuhukumiwa Omar al Bashir katika mahakama hiyo.

Mahakama ya KImataifa ya Jinai (ICC) yenye makao yake mjini Hague Uholanzi, mwaka 2009 hadi 2010 ilimtuhumu rais huyo wa zamani wa Sudan kuwa ametenda jinai za kivita na jinai dhidi ya binadamu katika eneo la Darfur. Hata hivyo al Bashir alikanusha tuhuma hizo na kuitaja mahakama ya ICC kuwa ni chombo cha kisiasa.

Tangu mwaka 2003 eneo la Darfur liliathiriwa na mapigano ya silaha baina ya vikosi vya jeshi la serikali na makundi ya waasi wenye silaha; ambapo ripoti zinasema kuwa, hadi sasa raia laki tatu wameuliwa na wengine karibu milioni 2.5 wamelazimika kuwa wakimbizi.

Jimbo la Darfur, magharibi mwa Sudan lililoathiriwa na machafuko

Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) ni mahakama ya kwanza ya kudumu ya kimataifa inayoshughulikia uhalifu wa maangamizi ya kizazi, jinai dhidi ya binadamu, jinai za kivita na nyinginezo.

Jeshi la Sudan Aprili 11 mwaka 2019 lilimng'oa madarakani Omar Hassan al Bashir baada ya kupambana moto maandamano ya wananchi waliokuwa wakilalamikia hali mbaya kiuchumi na kijamii na kisha wakamfunga jela kwa makosa ya ufisadi.
 
Ni sawa kabisa ndio iwe funzo kwa hawa madikteta ambao tawala zao zimekithiri kwa vitendo vya dhuluma na ukiukwaji wa haki za binadamu.
 
NINAPOSIKIA KUHUSU HILI KIMBA "ICC" ROHO YANGU INANIUMA SANA. KWANI MADHUMUNI YA KUANZISHWA KWAKE, NAMAANISHA MUUNDO WA MAHAKAMA YENYEWE, NI TOFAUTI NI UTENDAJI KAZI WAKE. KWANINI WENGI WA WANAOSHTAKIWA HAPA NI WATU WA KANDA FULANI. NINAMAANISHA KANDA DHAIFU. YAANI HASWA HASWA AFRICA, ASIA NA VIJINCHI FULANI VYA BARA AMERICA? KWANI HAYA MATAIFA IMARA, WATU WAKE HAWATENDI MAKOSA YENYE KUSTAHIKI KUFIKISHWA ICC? HAPO NDIPO UTAKAPOBAINI KWANINI NCHI FULANI FULANI SIYO MWANACHAMA WA ICC. TENA UTASHANGAA ZYD KWANINI WEWE NCHI DHAIFU UNALAZIMISHWA KUWA MWANACHAMA WA ICC? UKIKATAA UNATENGWA. NAOMBA NIISHIE HAPA
 
NINAPOSIKIA KUHUSU HILI KIMBA "ICC" ROHO YANGU INANIUMA SANA. KWANI MADHUMUNI YA KUANZISHWA KWAKE, NAMAANISHA MUUNDO WA MAHAKAMA YENYEWE, NI TOFAUTI NI UTENDAJI KAZI WAKE. KWANINI WENGI WA WANAOSHTAKIWA HAPA NI WATU WA KANDA FULANI. NINAMAANISHA KANDA DHAIFU. YAANI HASWA HASWA AFRICA, ASIA NA VIJINCHI FULANI VYA BARA AMERICA? KWANI HAYA MATAIFA IMARA, WATU WAKE HAWATENDI MAKOSA YENYE KUSTAHIKI KUFIKISHWA ICC? HAPO NDIPO UTAKAPOBAINI KWANINI NCHI FULANI FULANI SIYO MWANACHAMA WA ICC. TENA UTASHANGAA ZYD KWANINI WEWE NCHI DHAIFU UNALAZIMISHWA KUWA MWANACHAMA WA ICC? UKIKATAA UNATENGWA. NAOMBA NIISHIE HAPA
Mifumo ya Mahakama ni mibovu kwa Nchi nyingi za kiafrika hivyo ICC haikwepeki.
 
Marekani na washirika wake ndio waharifu wakubwa wa kivita na ushahidi upo wazi lakini hawakamatwi kwa kuwa wao ndio wafadhili wa mahakama hiyo........
Sasa nani atawakamata? Ni kwamba ICC unapelekwa na nchi yako au nchi unayoitembelea (kumbuka alipoenda South Africa) na mara nyingi watu wanaopelekwa kwenye hiyo mahakama wanakuwa wameshapoteza madaraka au nguvu ya kijeshi waliyokuwa nayo.

Viongozi wa kiafrika wanafanya jinai za kimataifa ndani ya nchi zao so wanapokosa madaraka ni rahisi kwa nchi husika kuwasalimisha ICC. Viongozi wa Marekani na Ulaya wanafanya makosa hayohayo nje ya mataifa yao kwa maslahi mapana ya nchi zao sasa hapo unategemea nani awapeleke, kwanza Marekani sio mwanachama wa ICC.
 
Back
Top Bottom