Subiri kidogo nikwambie!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Subiri kidogo nikwambie!!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by major mkandala, Mar 22, 2010.

 1. m

  major mkandala Member

  #1
  Mar 22, 2010
  Joined: Mar 6, 2010
  Messages: 74
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Si kweli!  [​IMG]
  Kuna siku nimewahi kuandika kwamba kuna usemi mmoja wa kingereza unaosema:
  “Someone is better than no one”


  Kwa maana kwamba wapo watu ambao (hasa wanawake wale ambao wanaona muda unaenda bila kuwa na mchumba au mpenzi wa kuwa naye katika maisha) huamua kushikana na bora mwanaume kwa imani kwamba ni heri kuwa na huyo mmoja (unfaithful, untrustworthy) kuliko kutakuwa na mwanaume yeyote.

  Subiri kidogo nikwambie!
  Kujiingiza kwa wanaume ambaye moyo wako hauko radhi eti kwa sababu unataka na wewe uonekana una mpenzi au una mchumba au una mume ni kuumiza hisia zako.
  Hata kama unaamini utafanikisha matakwa yako bila kuunganishwa emotionally, intellectually au affectionally utaishia kuumizwa.
  <!--[if !supportEmptyParas]--> <!--[endif]-->
  Pia huyo someone ambaye unaona ni afadhari kuliko kuwa mwenyewe ni looser ambaye anakuzuia wewe kumpata anayefaa, kwa lugha nyingine huwezi kumpata mwanaume mwenye sifa njema kama utaendelea kukaa au kushikamana na huyo someone wako ambaye hata hivyo ana sifa ovyo.

  Wengi wanajuta kwa sababu ya kuamini kwamba "someone is better than no one, hata hivyo waliokiri kwamba "no one is better than a relationship that lack respect" wanapeta.
  <!--[if !supportEmptyParas]--> <!--[endif]-->
  Tafakari kwa makini!
  <!--[if !supportEmptyParas]--> <!--[endif]-->

  [​IMG]
  [​IMG]
   
 2. m

  major mkandala Member

  #2
  Mar 22, 2010
  Joined: Mar 6, 2010
  Messages: 74
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Je, ni Kuzidiwa Nguvu au Aibu?  Eti wanaita "Cuddling"
  [​IMG]
  Kaka Mbilinyi mimi ni mwanamke wa miaka 26 na nimeolewa. Tatizo ni kwamba kila ninapokuwa na mume wangu tukifanya mapenzi nashindwa hata kumpapasa ili na yeye awe stimulated, kitu pekee nina weza kufanya ni kumbusu.
  Hii inanifanya nijisikie vibaya kwani najua na yeye anahitaji kuwa touched ili awe aroused.
  Lakini sielewi kwanini nashindwa kumshika hata kidogo naomba msaada wako.
  Je, huwa naskia raha sana mpaka naishiwa nguvu au ni aibu?
  Dada Jane (siyo jina halisi)
  Dada Jane asante sana kwa swali zuri, pia hii ni kukufahamisha kwamba nimeshindwa kutuma majibu yako kutokana na sababu kwamba kila nikituma kwa email ile umenitumia message inarudi (bounce back) hivyo nimeamua kukujibu kupitia hapa kwenye blog kwa kuwa sina namna..
  Kutokana na maelezo yako kwanza umesema kwamba unajisikia vibaya kitendo chako cha kushindwa kumshikashika ili asisimke kama yeye Anafanya kwako, ingawa hujajua kama ni aibu au kuishiwa nguvu na mahaba anayokupa mumeo.
  Hongera sana kwa kuwa na mume ambaye anaweza kukufikisha pale ambapo unahitaji kufika na hongera kwako pia kwa kuwa unahitaji kumfikisha mume wako mbali zaidi kimahaba.
  Kwanza kabla ya kukusaidia nini ufanye ili uwe unajisikia raha kumshika mume wako wakati wa maandalizi ya tendo la ndoa na wakati wa tendo la ndoa lenyewe ni vizuri kukudodosa ili kujua kama kuna chanzo (unresolved emotional issues) katika malezi na mtazamo wako kuhusu wanaume.
  Ni vizuri kuangalia upya katika maisha yako (background) umekuwa na uhusiano wa aina gani na wanaume tukianza na baba yako, kaka zako, ndugu wote wa kiume (mjomba, baba mdogo nk), wavulana ulisoma nao au fanya kazi nao kwa kujibu maswali yafuatayo:
  Je, baba yako alikuwa na uhusiano mzuri na mama yako au wewe mwenyewe kama mtoto na binti?
  Je, baba yako alikuwa na uhusiano wa aina gani na mama yako? (mzuri sana au kawaida au katili)
  Je, wakati mdogo au wakati upo shule kuna mwanaume au mvulana aliwahi kukutukana na kukudhalilisha hata kimapenzi hadi ukawa unaogopa kushikwa na mwanaume yeyote?
  Je, huwa unajisikia raha kushikwa, kukumbatiwa au kugusana mwili na mume wako hata nje ya chumbani?
  Je, mlikuwa na desturi za kukumbatiwa na wazazi au ndugu zako wa kike au kiume na kuwa jambo la kawaida katika maisha au ilikuwa marufuku?
  Baada ya kujibu hayo maswali na kunitumia majibu basi naweza kufahamu chanzo cha tatizo lako ni raha au kuzidiwa nguvu au ni mtazamo mbaya ulioingizwa ndani yako kuhusu kumgusa mwanaume (mume wako).
  Kwa kuwa unapenda nawe uwe unamshikashika mume wako ili awe anasisimka kama wewe basi jambo la msingi ni kuanza kujifunza kumshikashika mumeo nje ya chumbani kwanza na ukishajisikia vizuri nje ya chumbani basi itakuwa rahisi mkiwa chumbani kushikana bila wasiwasi.
  Fanya yafuatayo kwa wiki tatu mfululizo (yaani siku 21) kwani ukifanya kwa uaminifu itakuwa tabia na ikishakuwa tabia basi mchezo umekwisha.
  Kwanza kila siku asubuhi wakati wa kuamka hakikisha umemkumbatia mume wako au mnapoagana kwenda kazini hakikisha umemkumbatia kwa kutulia mwilini mwake kwa sekunde kadhaa hadi dakika moja na busu juu kila siku.
  Pia unapokutana naye tena baada ya kurudi kazini hakikisha unafanya the same.
  Ikitokea mnatembea njiani au Mahali popote hakikisha unamshikashika mkono mumeo (kiganja) mara kwa mara.
  Mkiwa nyumbani mmekaa hakikisha unamshika au gusa mikono, mabega yake au unajigusisha kwenye mwili wake au shika nywele zake, kidevu, shavu, sikio, uso, mgongo, miguu au vyovyote unaweza, mission ni kuhakikisha mwili wako au sehemu ya mwili wako haikali mbali na ngozi yake.
  Kama unaweza this time kabla ya tendo la ndoa mfanyie massage mara kwa mara mwili mzima.
  Ukimshambulia kwa hivyo vitu kwa siku 21 basi naamini utakuwa na ujasiri wa kumgusa na kumpa msisimko wa uhakika mume wako.
  Ubarikiwe na Bwana!
   
Loading...