Subaru Forester Vs Mazda CX5

Mkuu, iyo CX5 ya 2017 ya Diesel ina Ushuru tu wa Mil 19 hivi.

Nimeonana nazo kadhaa mjini aisee kali sana.
Mwanzoni mwa mwezi huu nimepokea CX5 ya 2015 L Package. Nishapiga trip Dar Moshi. Inaridhisha design na performance. Sijui kwanini watu wanashobokea Toyota.
 
Mimi nafikiri CX-9 na CX-7 ndiyo Mazda alituliza akili kuliko hata CX - 5
 
Mwanzoni mwa mwezi huu nimepokea CX5 ya 2015 L Package. Nishapiga trip Dar Moshi. Inaridhisha design na performance. Sijui kwanini watu wanashobokea Toyota.
L package ndio top package eeh. Mazda inafurahisha sana aisee.

Bado tuna uwoga wa “mafundi” na spea. Kwahiyo kila mtu anaamini Toyota ndio kimbilio.
 
Hakun
Hakuna tofauti wala yenye afadhali. Yote makopo tu. Gari ni Toyota ya ulinganisho huo. Na ndio maana hata bei Toyota ya ulinganisho wa hizi mfano Harrier ni karibia mara 2 ya hayo makopo. Hata ugumu ni tofauti pia
 
Hakun

Hakuna tofauti wala yenye afadhali. Yote makopo tu. Gari ni Toyota ya ulinganisho huo. Na ndio maana hata bei Toyota ya ulinganisho wa hizi mfano Harrier ni karibia mara 2 ya hayo makopo. Hata ugumu ni tofauti pia
Makopo tenaaa???
Harrier ya 2014 ina utofauti gani wa body na Mazda CX-5 ya 2014?.
Sometimes kukaa kimya ni akili pia
 
Makopo tenaaa???
Harrier ya 2014 ina utofauti gani wa body na Mazda CX-5 ya 2014?.
Sometimes kukaa kimya ni akili pia
Pole kama unahusika nazo.

Hiyo Harrier ya 2014 na mazda jaribu tu hata kulinganisha bei. Ni vitu viwili tofauti. Hata ugumu.
Bahati nzuri nafahamu magari kitambo.
Kibongo bongo tunakimbilia Mazda au subaru au Nissan duas ni ksbb tu ziko chini bei kulinganisha na Toyota zinazolingana kwa muonekano.

Mazda,subaru,Nissan duas,usumbufu wake na uharibikaji wake huwezi kulinganisha na Toyota. Hizo nilizozitaja hapo juu inaweza ikakuharibikia tu ghafla uko safarini, inaweza ikawa kwenye engine au gear box au hata mounting kiasi cha kushindwa kuendelea na safari. Lakini upande wa Toyota yoyote uharibikaji wake lazima itakutaarifu muda kidogo kwamba kuna mahala hapako sawa,labda iwe wewe tu uwe mvivu wa kufuatilia unaposikia kuna utofauti mahala.

Kwa vijana waliongia kizazi cha kuingia kwa hizi subaru,mazida na Nissan akiingia kwenye kutumia hizo tu anaweza kudhani usumbufu anaopitia humo kwenye hizo gari labda hata kwingine ni hivyo hivyo. Toyota hazina usumbufu wa kijinga jinga kama zilivyo hizo gari hapo juu. Hivi karibuni kuna jamaa yangu amepack MAZDA CX5 mpya tu alitumia si zaidi ya mwezi toka aidokoe. Ikaua turbo. Usumbufu wa aina hizo kwenye Toyota haumo.
Kwenye hizi gari tunazotumia kwa wingi huku,ingia Toyota tu itakuvumia sana kuliko hizo zingine
 
Kila MTU duniani anajua Hilo kuwa Toyota ndiyo gari zinazoaminika hakuna ubishi kwenye hili... wamiliki wa brand tofauti na Toyota tumetokea hukohuko kwenye Toyota.

Haiwezezekani wote tuendeshe Toyota Tu eti kwasababu ni imara
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…