Sub-contract kwa wakandarasi

Sub-contract kwa wakandarasi

miketee

Member
Joined
Feb 17, 2020
Posts
38
Reaction score
23
Wana JF nimekuwa nikiona wakandarasi wazalendo tena Wadogo wakipata Sub-contract kwa wachina na wakandarasi wengine hapa Dar na mikoani. Kwa wale Walio ndani wakifanya sasa au wanajua namna ya kupata kandarasi hizo naomba muongozo wa kupata.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kimsingi, jitahidi kuwa karibu na wakandarasi wakubwa na kampuni yakk ijulikane ina deal na activities zipi.

Mfano mkandarasi mkubwa anaweza kuwa anajenga jengo la ghorofa 3. Wewe ukamwomba ufanye kipengele cha umeme, au plumbing.

Kama una uzoefu na kazi hiyo atakupa bila tatizo.
Atakutambulisha kwa client wake na consultant.
Na katika malipo kuna % ambayo ataichukua kwako kadri ya mkataba mlivyo kubaliana.

Note:
Sub-Contractor ni mkandarasi mdogo.
Client-Mwenye mradi.
Consultant-Mtalaam mshauri wa mradi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jamaa hapo juu namshukuru ametoa mwanga,wengine endeleeni kutiririka,hiki swala ni muhimu Sana hasa kwa biashara changa
Asante! Muhimu tu usisite kuingia na kujaribu kuwaomba wakandarasi wakubwa wakupe Sub-Contracting kutokana na utalaam wako.

Ukiipata kazi jitahidi kuifanya kwa weredi iwe nzuri ili kuitangaza kampuni yako changa. Naye aweza kukutafutia kazi ktk kampuni nyingine.

Ukishafanya sub-contracting mbili au tatu kampuni yako yaweza kuwa imesimama na ukaomba kazi mwenyewe na ukaifanya.

Hakikisha kampuni yako imesajiriwa.

Asante.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wana JF nimekuwa nikiona wakandarasi wazalendo tena Wadogo wakipata Sub-contract kwa wachina na wakandarasi wengine hapa Dar na mikoani. Kwa wale Walio ndani wakifanya sasa au wanajua namna ya kupata kandarasi hizo naomba muongozo wa kupata.

Sent using Jamii Forums mobile app
Una kampuni unataka kazi?
 
Back
Top Bottom