Serikali yetu sikivu ya wanyonge hili suala vipi? Mbona free channels kwenye visimbusi vingi bado ni tatizo mpaka leo? Kama serikali imeshindwa kutatua hili tatizo, basi warudishe utaratibu uliokuwapo awali.
Au kwa sababu TBC inapatikana ndio basi?
...
Kazia hii ni muhimu ila mtoa mada haja fafanua ni nani anakera. Achana na tbc ....
Anaekera hapa ni mchina per say. Startimes ni kampuni ya taifa la china. Wapo kenya wapo uganda na mataifa mengi tu. Ni tanzania tu ambapo wamechukua hatma ya tbc. Mkulu alishafika more than twice ... akitoka amelowana ... Vielelezo walitoa kwa tvt .. Sasa sio tbc tena ni star! Minara yao yote ilijengwa na kikosi kazi cha tvt kama ilivyokuwa kwa celtel.
Mwanzoni television ziliruhusiwa kurusha analog tv kwa mikoa mitano kama kanda. Kanda hizo ni Dar - Dodoma - Mwanza -Arusha - Mbeya. Tv zilizokidhi hiki kigezo ni ITV, EATV, StarTV, chTEN na TBC.
Hizi chaneli ndio tunaziita za free. Serikali iliipa jukumu Startimes kubeba huu mzigo. Inawezekana hawajafikia muafaka frequency allocation zikae vipi!
Sioni mantiki ya kila king'amuzi kutumia frequ ency zao kwa ajili ya hizo free tv. Kwa kanda hii ya dar, TING ana frequency ya 530, Digitek 490, Continental 474 na startimes usipime 578; 586; 602; 610; 634; 658 ...
Hivyo basi frequency ya FTA iainishwe na zirushwe na mbia wa serikali - Startimes.
Kwa sasa Startimes wanarusha FTA mbili Guide na tbc, ila kama una king'amuzi chao unapata hizo kama FTV kwa maudhi mengi tu. Ting na continental wanalipisha stesheni husika na digitek wanarusha zote FTA ila hawajulikani wako wapi ila most likely ni assets za Mengi - RIP.
Hivyo basi frequency ziainishwe na startimes warushe hizo frequency kama FTA na waondoe restrictions kwenye kingamuzi chao.
ZMUX imekaaje Pemba na Unguja? Kwa Dar mnaonekana kwa mbinde 514.
...