Suala la wikileaks kuna la kujifunza

Yona F. Maro

R I P
Nov 2, 2006
4,202
218
Kwahiyo tumekuwa tukisoma na kujadili mambo kadhaa kuhusu taarifa za siri za Serikali ya Marekani kuvuja na kuingia kwenye mtandao wa WIKILEAKS na mtandao huo kuweka taarifa hizo hewani kwa ajili ya watu wengine kuchukua kwa ajili ya kazi zao mbalimbali .

Kwangu mimi nishitushwi sana na taarifa hizo kuvuja na hata taarifa zingine zikiendelea kuvuja kwa mtindo huu pia sintoshituka ni masuala ya kuangalia kwa njia mbili kwa wale wafuatiliaji wa mambo naomba nielezee pande mbili za sakata hili .

Kwa kipindi cha miaka 10 hivi iliyopita baadhi ya nchi duniani haswa za ulaya na marekani zimekuwa zikihamisha mawasiliano yao ya kimtandao kuhifadhiwa na kampuni binafsi kwenye mfumo wa cloud kwenye mfumo huu wa cloud kwa mfano ofisi za ubalozi wa marekani zilizosambaa dunia nzima mawasiliano yake yanaweza kuwa yanahifadhiwa kwa mtindo huu .

Ina maana mfanyakazi wa ofisi wa ubalozi wa marekani kuna taarifa anaweza kuziona au kuchukuwa baadhi ya taarifa kwa mtindo Fulani akiwa hapa Tanzania kwa kutembelea huko zinakohifadhiwa kwa mtandao ingawa kunaweza kuwa na mambo ya ruhusa na nini .

NOTE :
Moja ya athari za mtindo huu wa mawasiliano ni usiri wa taarifa zinazosambaa kwa njia ya mtandao huo na jinsi zinavyohifadhiwa watu wengi wameanza kuwa na mashaka kidogo haswa kwenye masuala ya taarifa zao zinavyosambaa kwa mtindo huu kwa sababu mtu anaweza kuwa Canada akafanya kazi na mwenzake aliyepo japan watu hawa wanaweza kuwa hawajawahi kuonana lakini wanafanyia kazi kitu kimoja .


MFUMO WA MAREKANI
Marekani na taasisi zake nyingi haswa zinazohusiana na usalama zinatumia mfumo mmoja unaoitwa SLPRNET kwa ajili ya mawasiliano ya sehemu zote duniani kama nilivyosema hapo juu kwamba mtu anaweza kuwa Japan na mwingine yuko Africa Kusini wakafanya mawasiliano au kufanya mjadala bila kujuana chochote kwa mtandao ndani ya mfumo wa SLPRNET ambayo taarifa zake zinahifadhiwa na GOOGLE kwa mfano .

Wakati ambapo kampuni nyingi wanakimbilia kwenye mfumo wa cloud kwa ajili ya kuhifadhi taarifa na kufanya kazi kwa makundi wakiwa popote duniani ndipo huduma nyingi za kuhifadhi taarifa hizi kwa njia ya mtandao zinazidi kuboreshwa lakini pia kukiwa na tatizo la usalama kwenye taarifa hizi .


MAMBO YA ZIADA
Wakati mwingine taarifa kama hizi za WIKILEAKS zinaweza kuwa zinatolewa kwa makusudi kwa malengo Fulani ya kisiasa kama wewe mfuatiliaji wa mijadala ya afrika haswa afrika magharibi kuna watu wameshutumu jarida moja linaloitwa SAHARAREPORTERS kwamba linafadhiliwa na Nchi moja ya Nje kwa ajili ya kufanya shuguli zake haswa kuchochea uhasama na mgawanyiko katika nchi za Afrika magharibi kutokana na Taarifa zake za mara kwa mara .

Kinachotokea SAHARAREPORTERS kimewahi kutokea nchini IRAN wakati mtandao wa Twitter ulivyoshirikiana na Baadhi ya wanaharakani nchini humo kuandaa maandamano na fujo za aina nyingine pamoja na hujuma kibao , inaendana pia na Tetesi zingine zinazoenda kwa mtandao wa USHAHIDI ulivyokuwa unatoa taarifa zake za UCHAGUZI Tanzania hata na ule wa Kenya ambapo watu kadhaa waliuwawa jinsi pia unavyofanya kazi zake nchini kongo .

Haya ni maoni yangu tu naomba maoni haya yatumike katika kujenga kuhabarisha na kwa faida ya wengine wengi haswa hii sehemu ya chini – wanamtandao haswa wa nyumbani Tanzania tuwe makini sana inawezekana na sisi tukatumika kuvujisha siri za serikali , makampuni yetu na taarifa zingine nyingi lakini mathara yake ni kwa wale walio wengi .
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom