Suala la Uanachama ndio sumu ya maendelo

Mukuu123

JF-Expert Member
May 7, 2019
319
1,221
Kwa hapa tulipofikia naona siasa za hapa Tanzania zimegubikwa sana na ushabiki pasipo kujikita kwenye hoja na sera za Wagombea.

Sioni manufaa yoyote ya kitaifa mtu kuwa mwanachama wa chama fulani labda uwe na itikadi au ndoto za kuwa mwanasiasa, ndio naona ni sawa kuwa mwanachama kutokana na kutokuwepo kwa suala la mgombea binafsi.

Kutokana na hii naona watu wamekua wanaleta ushabiki wa Simba na Yanga kwa maswala ya kitaifa jambo ambalo naona kama ni ukosefu wa kuelewa mambo ya utawala.

Hakuna rais wa Chadema wala CCM au ACT mara unapokuwa kiongozi unakua kiongozi wa wote na kama utawala utakua mbovu ni wote ambao mwisho wa siku tutakua waadhirika wa huo utawala, hebu tuache swala la kushabikia vyama tujikite kwenye hoja pasipo kuangalia mambo ya chama na kuacha mambo ya kuwa na kadi ya chama fulani.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom