Suala la Manji na Yanga wenye akili tulishaliona mapema tukaonya

GuDume

JF-Expert Member
Jan 18, 2015
6,651
14,318
Nlisema hapo mwanzo yanga walijiweka katika mazingira mabaya sana kwa kuacha kujiandaa kujitegemea na kuanza kumtegemea manji peke yake. Manji amefanywa kama mungu na weng ya wanayanga. Wakasahau naye ni binadamu aweza umwa, pata matatizo au kufariki.

Yanga walikabidhi kila kitu kwa manji ambaye alimlipa kila mtu kuanzia yule anayeshinda pale nje kunywa kahawa mpaka anayeshinda ofisin kwenye kiyoyozi. Wengine walikuwepo tu kwa vyeo vya majina lakin kiutendaji hakukuwa na kitu cha maana.walibaki kupokea amri tu toka kwa mwenye yanga na aliyetaka kuinua kichwa kilifyekwa.

Leo yanga inasema haina pesa...hali ngumu. Hawa kutoka kuwa wakimataifa hadi wa kulialia?tuliposema jaman uhuru ni kujitegemea wengine hawakuelewa dhana hii. Huwez kuwa unategemea halafu ukawa huru. Kauli ya mkwasa kuwa hali mbaya ni kauli ambayo hatukutegemea itolewe kwa team ambayo miez miwili iliyopita ilikuwa ikijinadi na kutamba.

Ni sawa na kuringia pesa za mjomba. Je yanga wanalipwa tsh ngap na mdhamini wao quality group? Hawa yanga si walizikana hata zile pesa za azam za urushwaji wa matangazo kwa kibri?nawaona wakiziendea hizo pesa kwa magoti na kubembeleza walipwe.

Team za simba na yanga haziwez endelea kwa kutegemea mtu mmoja aziendeshe kwa matakwa yake binafsi. Kwa kuamua kuwa mfadhiri. Ufanyike utaratibu unaotumika na team za wenzetu ulaya na marekani. Ziuzwe hisa au mtu ainunue team kabisa
 
86bbc746fe418bcbabefb762d0adf740.jpg
 
Yanga na simba wa uwezo wa kujitegemea wakitaka.Shida ni makundi flani ambayo ukiweka mfumo huo tu wao Mahakamani kuweka pingamizi.Kisa ulaji unapotea
 
Timu inayojitegemea Tanzania ni ipi?
Azam ni mali ya mtu binafsi. Ni suala tofauti hilo.
Simba haitegemei watu wachache?
 
Alafu Mkwasa alivyoibwaga timu ya taifa alielekeza lawama zote kwa akina Malinzi kama watu walioshindwa kuendesha mpira. Tatizo kubwa alilolalamikia lilikuwa ni mambo ya kutolipwaposho na akadhani hapo Yanga atalipwa vizuri na kwa muda bila kujua kuwa atalipwa na mtu mmoja na sio Yanga kama timu! Sasa ameona kuwa pesa haina mwenyewe.
Tujifunze kitu hapa, kujitegemea ili kuendesha masuala yetu ikiwamo michezo ni muhimu zaidi ya kujidanganya na hawa ma-opportunists. Pia kujifunza kuongea ukweli badala ya majungu na unafiki kwenye mpira wetu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom