Suala la maji ubungo - kimara | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Suala la maji ubungo - kimara

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by DASA, Mar 6, 2012.

 1. DASA

  DASA JF-Expert Member

  #1
  Mar 6, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 1,031
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Watu wa kimara tumekuwa tukipata maji kwa mgao wa aina fulani kwa kipindi kirefu huko nyuma, ambapo ilikuwa ni angalau mara mbili kwa wiki. lakini huo mgao kwa sasa unafifia sana, kwa sasa unaweza ukapata kwa hata saa limoja tu kwa wiki nzima au usipate kabisa.

  Lakini kuna mchezo ambao nauona ambao nautilia mashaka kwa wanaotuuzia maji na magari, sababu utakuta wanafanya biashara yao vya kutosha, ndoo mpaka 500 wakati mwingine, sasa utakuja kukuta maji ya Dawasco yanaanza kutoka baaada ya hawa majamaa kufanya biashara yao vya kutosha ambapo watu mnakuwa tayari mshanunua na hamna shida sana ya maji.

  Kifupi wakati wa shida dawasco hawatoi maji, mtakapokuwa mmeshanunuanunua ndio wanatoa maji. hii inanipa mashaka sana na utendaji wa dawasco.

  Jamani kupitia JF tunaomba kama kuna mchezo mchafu unafanyika basi iwe inatosha sasa kwani maisha ni magumu sana sasa, sio kila mtu anaweza kununua maji yanayouzwa na magari kila siku.
   
 2. P

  Pelege Senior Member

  #2
  Mar 6, 2012
  Joined: Mar 1, 2012
  Messages: 137
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mbunge wetu Mh mnyika alishasema serikali inafanya makusudi kutokutupa maji kwasababu jimbo lipo upinzani na alishauri tuandamane mana kama malalamiko aliyeshayawasilisha muda sana,sasa kikubwa ni kuandamana mpaka dawasco mana hii hali haikubariki.
   
Loading...