Mshahara wa polisi ni bei gani hasa, ili iweze kumwezesha kufanya kazi kitaaluma? Wameamua kuwaachia kazi wabuya unga wa mitaani wanaowaita polisi shirikishi. Wakijua ya kwamba haitawagharimu kusumbuana na wahalifu mahakamani, kwani wale wanaowaita raia wenye hasira kali watakuwa wameshasimplify kazi kwa kuchoma moto. Mimi nimetembea nchi zote zinazotuzunguka na nakuhakikishia kwa wakati huu uliopo hakuna raia wa nchi wenye kiu na shauku ya kuua kama Tanzania. Taifa lenye midomo inayomtaja Mungu bali wakimchukia na kumkana kuliko wengine. Na hii huenda ikawa imechochewa na uongozi usiozingatia maadili ya kiuongozi na tamaa ya kuwa mabilionea kwa kipindi kifupi cha utawala wao. Mungu irehemu Tanzania.