Style mpya ya maandamano

JT2014

JF-Expert Member
Jan 18, 2014
1,863
1,367
Wana jf habari zenu, Leo asubuhi kweye taarifa ya habari ya ITV Wamemuonyesha mkurugenzi wa TECCO kule mwanza akiwa amevaa magunia na kwenda kwa mkuu wa mkoa, kanisa la KKKT na kanisa katoliki, alipoojiwa na polisi alisema kuna fedha yake aliyopewa kama zawadi ya kupanda miti jiji la mwanza na kilifanya kuonekana safi, na watu wameamua kumdhulumu.

Bila kutarajia amejikuta anafuatwa na kundi kubwa la watu ambao wamesababisha polisi kumkamata baada ya wanangaji kupiga simu kwamba anasababisha fujo.

Binafsi nimeipenda style hii ya kudai haki ambazo hazipatikani kiurahisi,wasomaji wa biblia watakumbuka kuwa kuvaa magunia ni ishara ya maombolezo, Nadhani huyu Bwana amedai haki yake,kikawaida alipoona imeshindikana akaamua kuiombolezea Naamini wenye mamlaka watahakikisha haki yake inalipwa. Kama umeiona hii habari nawewe changia kwa kadri ilivyokugusa.
 
Kafikisha ujumbe kwa umma na kwa wadaiwa pia, kama nafsi zao bado zipo hai naamini haki yake watampatia.
 
.... Namimi Kuna Jamaa, Ngoja Nitafute Magunia Niende Nikiwa Nimeyavaa
 
tukutane pale iptl tegeta uchi kuzuia tanesco kuendeleza mkataba na hao jamaa. tuwe kama 8000 hivi tuvae skin tight na wazee bukta vifua wazi
 
Back
Top Bottom