Studying au Learning? Ipi uichague katika Software Development?

Dr Orb

Member
Aug 4, 2019
10
75
Unawaza kuwekeza katika ujuzi wa kutengeneza program za simu, kompyuta au internet?

Kama una mawazo hayo lakini una wasiwasi hilo ni pepo Fanya kulishinda .....hahahahaha...kidding guys!

Lakini kama ni kweli basi una mawazo sahihi sana kwa kuwa ulimwengu wa Leo na kesho utategemea sana kompyuta kufanikisha mambo. Bila kujal taaluma yako, ili kuleta ubunifu wa kisasa na wenye manufaa katika taaluma yako lazima uhusishe tekinolojia.

Kuna namba mbili unaweza fanikisha ndoto zako,
1. By studying.
2. By learning.

Binafsi napendekeza learning badala ya studying, kwa kuwa learning haikufungi na mitaala. Ni namna ya kujifunza kutokana na mapenzi juu ya jambo ulitakalo. Lakini pia ni rahisi kwa kuwa haihitaji gharama kuwa kufanikisha jambo.

Kutokana na asili ya utendaji kazi na namba ya matumizi ya kompyuta wengi wanaofanikiwa ni wale katika mkondo wa learning kuliko studying. Sababu kuwa ni kwamba learners wanatumia mfumo wa learning ikiwa kuna jambo analilenga na amejiridhisha ili lifanikiwe lazima apate ujuzi huu wa kompyuta.

Mtazamo huu haumanishi studying haifai, hapana studying INA umuhimu wake kwa kuwa INA muongozo bora ambao haumchanganyi mwanafunzi yaani hutumia syllabus kitu ambacho ndio changamoto kubwa kwa learning style. Lakini umesongwa na changamoto kibao, kama vile Gharama, mitihani ya uhakiki jambo ambalo linaweza kukusababisha kushindwa kufocus katika kuelewa na kuwaza mitihani tu, mfumo huu unafinya uwezo wa kujua mambo kwa kuwa una mlengo wa madaraja ya ujuzi mfano astashahada, stashahada na shahada. Una kufanya kutegemea ajira zaidi kwa kuwa kuna ukomo wa ujuzi uliojikita kimadaraja zaidi. Pia ni gharama kubwa kwa kuwa unahusisha malipo ya ada Vila kujali umenufaika vipi, mfumo huu unajali zaidi muda kuliko uelewa wa mwanafunzi.

Kwa nini nakushauri learning, learning haina ukomo wa nini unapaswa kujua kwa wakati gani na ngazi ipi ya elimu, hivyo learning hainyimi ubongo uwezo wa kumeng'enya ikiwezacho. Leaning haina muda maalumu wala haihitaji msimamizi, wewe mwenyewe ndio kila kitu bidii yako mafanikio yako. Learning inafanyika popote na kwa MTU yeyote haina vigezo vya awali mfano mambo ya D nne , humu hakuna yaani ni spirit na kujituma tu ndo silaha katika learning. Kuna taasisi nyingi zinatambua mfumo wa Learning hivyo unaweza kujiandikisha na ukafanya mitihani kwa muda wako bila masharti magumu ili kuwa certified. Ni mfumo bora katika ujuzi unaohitaji ubunifu na juhudi binafsi kufanikisha mfano computer science. Haina muda maalumu, hapa tunaangalia umeelewa hata kama utahitaji miaka 10 katika mfumo huu wa learning ni fresh tu.

Kama wewe ni Technopreneur au unataka kuingia kundini nakushauri tumia learning. Huu ndio mfumo bora zaidi kwa sasa katika tasnia hii ya tekinolojia.

***Changamoto kuwa ya mfumo huu ni kufahamu nini ujifunze kwa wakati gani ili kufikia lengo mapema.***

Ntajitahidi kadri ya uwezo na uzoefu wangu katika safari yangu kuwapatia mambo ambayo nadhani ni yamsingi zaidi unapoanza lakini pia katika hatua tofauti za safari hii ya computer science self learning.

Uzi ujao ntatoa Yale ambayo nadhani ni ya msingi unapoanza safari hii.

Stay tuned.
 

Dive

JF-Expert Member
Mar 7, 2013
648
1,000
Studying unafungwa na mitaala ila learning haufungwi na mitaala.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom