Studio walioahidiwa wasanii wa bongo flavor yaotea mbawa THT

kapotolo

JF-Expert Member
Sep 19, 2010
3,727
2,214
"Wadau wa muziki wa bongo flava wamepumua kwa shukrani baada ya JK kuahidi kuwatengezea studio kubwa na ya kimataifa ya muziki ili kuwasaidia kujikwamua kiuchumi na kisanii.
JK ametoa ahadi hiyo kwenye hafla ya kutimiza miaka 3 kwa THT ambapo alikuwa mgeni rasmi kwenye hafla hiyo iliyoandaliwa na vodacom". Michuzi Blog.

vijana wa bongo flavor walisweti kumsaidia kurudi madarakani wakitegemea kuwa watapatiwa studio ya kurekodi nyimbo zao, imefahamika kuwa vyombo hivyo vya kurekodiwa muziki (STUDIO HIYO) wamepewa THT kwa maombi maalum kwa JK. Hii ni kwa mujibu wa tamko la waziri wa Habari ambaye alisema studio hiyo ni ya THT kwa maombi maalum kwa rais. Yaani studio si ya wasanii wote wa bongo flavor bali ya Ruge M. na THT yake na msanii mwingine hana chake, atarekodi kwa bei kama ya studio nyingine na sio kwa bei ya neema aliyoahidi JK.

JK nimemvulia kofia, heshima kwake, jamaa ni muongo hana mfano. Wasanii wetu nao wamezidi kujirahisi mno, wanatumika kila uchaguzi baada ya hapo wanamwaga, jifunzeni.

No wonder hawa Jamaa wa Clouds wanajikomba sana kwa Jk mpaka kumwandalia birthday kumbe wananufaika na tujimisaada
 
Hao wasanii wa ubongo wa flavour wakome kwa kujikombakomba na kukubali kutumika ka TP.
 
Saizi yao acha washike adabu...hapo msanii akikorofishana na clouds tu amekwisha hiyo studio ataisikia kwenye bomba!
 
Serikali yetu imejaa ujinga.
Mshahara wa mwezi ujao huenda usitoke kabisa kwa kuwa serikali haina hela.
Hii ni aibu kubwa kabisa kwa mtanashati na handsome boy kama kikwete
 
nyosha mkono kama ni mdau wa music unaefeel bila kikomo tuurudishe huu utawala maaana viongozi waliopo naona wote wamelala, tajiri kawanunua hata mahari pa kukemea naona wao wanachekela...kurupuka amka mtoto wa mkulima zinduka acha kupiga show za live kwa nguo za kukopa...
 
Ila hawa clouds pamoja na huyo ruge,itafika kipindi wataua bongo fleva,maana wanakua watu wa ajabu sana,wao ni THT tu ndio wanao ipigia debe,na wanamuziki watanzania nao wanajirahisisha sana,kama marlaw kutwa kuimba nyimbo za ccm,haya ndio kama hivyo tena wametoswa na THT wanashika hatamu,wasitumiwe kama( Hao wasanii wa ubongo wa flavour wakome kwa kujikombakomba na kukubali kutumika ka TP.)
 
Hahahahaaa, kucheka mjinga si kosa maana naona wamekutana katika fani yao ya usanii, hao wa ubongo wa fuleva na prezidaa wao, hakuna mbaya. nacheka tena Hahahahaaa.
 
Wajanja wachache wanatumia vizuri mianya ambayo wasanii wa Bongo Flavour wanapigwa changa la macho
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom