Stress hazipunguzwi kwa kuchepuka

Miss Neddy

JF-Expert Member
Nov 3, 2013
14,681
8,707
Igweeeeeeeeeeeeee

Hapa naongea na wale wanaodhani kuchepuka ndo suluhisho ya kumaliza msongo wa mawazo.

Unakuta mtu ana matatizo na mahusiano yake labda hawana maelewano mazuri na mpenzi wake ye anaenda kutafuta suluhisho kwa mchepuko utadhani kuku anaehatamia mayai ya chatu baadae anamezwa yeye.

Unapochepuka ukae ukijua anaekuchepusha nae anachepuka we unadhani umemkomoa mpenzi wako kumbe umejikomoa

Mahusiano kuna shida na raha mnasaidiana na ugomvi unapotokea mnayamaliza sio kutwa kupigana kama paparazi nyumbani kwa Wema

Jifunzeni kuyamaliza sio kutwa kuachana na kuchanika kama fuko la shangazi kaja looooh am out
 
Mumy ni wachache wanaolitambua hilo. Ila nadhani ni kushindwa kufikiria mara mbilimbili na kuchanganua faida na hasara kabla ya kuanza kulipiza.

Pia ni vyema kumshirikisha mungu kwa kila jambo.
 
Dawa ni nini?

manake hata pombe inasemwa sio dawa ajabu hadi madaktari sometimes hushauri mtu anywe kidogo
 
Mumy ni wachache wanaolitambua hilo. Ila nadhani ni kushindwa kufikiria mara mbilimbili na kuchanganua faida na hasara kabla ya kuanza kulipiza.

Pia ni vyema kumshirikisha mungu kwa kila jambo.
umeona eeeh ni wachache sana haswa wanaume ndo wanaongoza kwa kuchepuka ukimkorofisha anatafuta tulizo looh
 
Mwanamke anapokuwa na gubu saa zote maneno maneno ukirudi nyumbani inakuwa shida kubwa, hata tendo hulifurahii..ukimaliza kutatua kesi moja inakuja nyingine stress juu ya stress
 
umeona eeeh ni wachache sana haswa wanaume ndo wanaongoza kwa kuchepuka ukimkorofisha anatafuta tulizo looh
Hawawezekanagi hao na wala sio wa kushindana nao.

Wanawake tukiwa kama walezi wa familia inatupaswa tuzidi kupeana elimu ya kutosha mana mwisho wa siku wanaoathirika ni watoto.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom