Strategy nyuma ya Mbowe, Sabaya na IGP kuitwa kuwa mashahidi wa upande wa utetezi (FreeMan Mbowe)

Bwana Mapesa

JF-Expert Member
Apr 28, 2011
2,551
1,777
Habari Wanajamvi?

Nilivyosikia majina ya Sabaya , IGP Siro nikasema lazima Mawakili wa utetezi have a strategy in play.

Obvious Sabaya na Siro wata- turn hostile. Kwa maana nyingine ushahidi watakaotoa mahakamani hautokuwa unambeba au kumpa support Mbowe ambae kimsingi ndiye shahidi ambae Mbowe anataka kumtumia kwenye utetezi wake.

Hivyo basi, ikitokea mashahidi hawa wame-turn hostile kama nnavyobashiri. Nini strategy ya upande wa utetezi?
(Kibatara na Wenzake).

Hapa watakuwa na vitu kama viwili vya haraka either wa wa impeach mashahidi hawa ,au waweke limit ya scope ya ushahidi wao kwa kuwauliza leading questions ,ambapo majibu ni ndiyo au hapana "Yes" or "No".

Binafsi sijui strategy ipi hapo juu itakuwa adopted ila tutegemee vita kubwa ya kisheria kwenye kesi hii.

Kinachonifurahisha ni kwamba mahakamani utaulizwa chochote hata cha siri, na vyote huandikwa na kuwa sehemu ya nyaraka za jamii na mtu yeyote anaweza kupatiwa .

Je una wazo tofauti na langu? Let's brain storm here.

Niwatikie jioni njema.
 
Back
Top Bottom