Strategis Insurance acheni uhuni

Strategis Insurance acheni uhuni

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2009
Posts
76,579
Reaction score
161,430
Mimi ni mteja wa huduma ya bima ya afya ya Kampuni ya Strategis.
Kampuni hii ni ya kihuni kupitiliza.
Kupata huduma stahili na kwa wakati kwao hilo halipo kabisa, mathalani, leo nimeenda hospitali, system yao ikasema kuwa sistahili kupata huduma za matibabu. Nikajaribu kupiga Call Centre kwa namba zifuatazo:-
0782 788 800
0782 000 200
0788 599 644, 0788 599 511, 0778 100 222, 0778 800 222, 0767 882 015, 0767 882 016, 0713 800 115 na 0713 800 117.
Kila nipigapo namba hizi zinaita kisha hupokelewa na kukatwa.
Nikajaribu kupiga namba 0754 777 100. Hii ilipokelewa na jamaa aliyepokea akasema yeye yuko kwenye ambulance. Nikamuuliza call center mbona hawapokei simu akanijibu kuwa huwa wakati mwingine wanachoka kuongea na wateja.
Akanipa namba ya Daktari Florah Minja namba 0782 206 982. Namba hii haipokelewi.
Kwenye hii hospitali niliyokuja kutibiwa wameniambia kuwa huu ni mchezo wa kawaida kwa wafanyakazi wa Strategis lnsurance. Hata wakurugenzi wao ni wagumu sana kwenye kulipa huduma za afya zilizotumiwa na wateja wao kwenye makampuni mbalimbali.
Ndugu Mtanzania, ni wakati sasa wa kukataa huduma mbovu za afya. Afya ndio msingi wa uhai wa mwanadamu.
Kwa kuwa Strategis imeshindwa kutoa huduma bora za afya, bora waingie mtaani wakasake vyuma chakavu kuliko kufanya haya wayafanyayo yanayopelekea uhai wa mteja kuwa matatani.
 
Pole sana Bujibuji, Hao watakuwa wanadaiwa hivyo huduma zimesitishwa kwao au mwajiri wako ndio hajalipia kwa muda mrefu hadi wakaamua kumtoa kwenye huduma.
 
Pole sana Bujibuji, Hao watakuwa wanadaiwa hivyo huduma zimesitishwa kwao au mwajiri wako ndio hajalipia kwa muda mrefu hadi wakaamua kumtoa kwenye huduma.

Vp kuhusu call centre kutopokea simu?? Tena hili nalo ni tatizo sugu?
 
Vp kuhusu call centre kutopokea simu?? Tena hili nalo ni tatizo sugu?

Hapo usanii utakuwa unaanzia kwa CEO hivyo hata watumishi wa kawaida wanakosa majibu ya issues nyingi na kuamua kupiga kimya kuliko matusi ya wateja.
 
mimi ni mteja wa huduma ya bima ya afya ya kampuni ya strategis.
Kampuni hii ni ya kihuni kupitiliza.
Kupata huduma stahili na kwa wakati kwao hilo halipo kabisa, mathalani, leo nimeenda hospitali, system yao ikasema kuwa sistahili kupata huduma za matibabu. Nikajaribu kupiga call centre kwa namba zifuatazo:-
0782 788 800
0782 000 200
0788 599 644, 0788 599 511, 0778 100 222, 0778 800 222, 0767 882 015, 0767 882 016, 0713 800 115 na 0713 800 117.
Kila nipigapo namba hizi zinaita kisha hupokelewa na kukatwa.
Nikajaribu kupiga namba 0754 777 100. Hii ilipokelewa na jamaa aliyepokea akasema yeye yuko kwenye ambulance. Nikamuuliza call center mbona hawapokei simu akanijibu kuwa huwa wakati mwingine wanachoka kuongea na wateja.
Akanipa namba ya daktari florah minja namba 0782 206 982. Namba hii haipokelewi.
Kwenye hii hospitali niliyokuja kutibiwa wameniambia kuwa huu ni mchezo wa kawaida kwa wafanyakazi wa strategis lnsurance. Hata wakurugenzi wao ni wagumu sana kwenye kulipa huduma za afya zilizotumiwa na wateja wao kwenye makampuni mbalimbali.
Ndugu mtanzania, ni wakati sasa wa kukataa huduma mbovu za afya. Afya ndio msingi wa uhai wa mwanadamu.
Kwa kuwa strategis imeshindwa kutoa huduma bora za afya, bora waingie mtaani wakasake vyuma chakavu kuliko kufanya haya wayafanyayo yanayopelekea uhai wa mteja kuwa matatani.


sio hao peke yao ,kuna kampuni inaitwa metropolitan, hao namba yao ya simu iliyopo kwenye headed paper ukipiga unajibiwa na kampuni ya simu kuwa haipo kabisa.chini wameeleza matibabu kuzidi laki moja yafanyike baada ya kupata go on toka kwao...

Waandishi wa habari tafadhali fanyieni utafiti mambo haya kisha muwalipuwe,....hizi ni deci na sio kampuni za bima
 
Kampuni za Bima zinachangamoto ngumu sana.Nitajitahidi niweke article moja imetoka hivi karibuni pengine mtaelewa.Kuna changamoto za kizembe lakini nyingine ni due to nature of Tanzania market.
 
Bora umeniambia mi nlijiunga na ile ya laki 3 unaisha march nimetumia elf 27 tu ngoja nikafanye chek up ya gharama sio kuwafaidisha bure tu
 
Pole sana kwa yaliyokukuta. Hiyo kampuni kwa sasa iko juu ya mawe financially. Kuna jamaa yangu wa karibu alikuwa anafanya kazi kwao but akaacha baada ya kugundua madhaifu yao. Na aliniambia lililobaki ni jina kwa sasa maana hapakuwa tena na good foundation financially na ni almost bankrupt! Wewe si wa kwanza kumsikia akiilalamikia. Nazidi kuamini maneno ya rafiki yangu!
 
Dah...poleni sana kwa usumbufu kwa watu wa STRATEGIS....vipi AAR kwa wanaoitumia na huduma zao? nataka kwenda huko....
 
AAR wanajitaidi niko nao ila corporate sijaona madudu miaka 3 sasa. Ningependa kujua individual plan cost zikoje nimkatie mtu. Hao CHF siwaamini au kwavile sijamuona anayetumia.
Dah...poleni sana kwa usumbufu kwa watu wa STRATEGIS....vipi AAR kwa wanaoitumia na huduma zao? nataka kwenda huko....
 
Back
Top Bottom