STRANDED!msaada tafadhali

STRANDED!msaada tafadhali

Mh..! Haya mambo ni magumu kutoa ushauri, pengine kuna kitu kinakusukuma kumrudia ingawaje huwezi kusema hadharani. Labda ukifikiria mgegedo wa ex wako unaona ni far better kuliko uliyenaye sasa, kwa hapo ni ngumu sana kutoa ushauri maana ushakuwa slave wake.

Ila kwa vyovyote vile sikushauri urudiane naye. Ingawa maamuzi ni yako.
 
Ukikosea uoe mwanamke kama huyu utakula hasara kubwa....

hasara tena sana harafu anasema anajieshimu! uyu mwanamke ni hasara kweli. ukioa kama uyu ni kujutia na majanga.

Inaonekana ajui nin akitakacho. magume gume unaweza piga mpaka ukaua. sasa uyo jamaa yake mpya sijui anajisikiaje akigundua hivi.
 
Mimi ni msichana wa miaka 25.miaka minne iliyopita nlikutana na kijana flani nkiwa chuo,tukatokea kupendana tukawa wapenzi.muda haukupita sana,huyo kijana akaanza nionesha his true colours akawa mhuni mno.ikaanza kiburi na kikubwa akawa anacheat hadi ikawa inafahamika chuoni sababu kila kukicha kulikuwa na story kuhusu yeye na msichana flani.nliumia na kukonda sana sababu nlimpenda mno kupitiliza.nlikuwa nakosa usingizi,nakesha nalia kwa maumivu na vituko haviishi.mara nimpigie anikatie simu na kuizima kabisa hadi kesho yake akijiskia kuiwasha kumbe anakuwa yuko na binti mwingine.nkitishia kumuacha,anajirudi kwa siku kadhaa kisha anaendelea na uhuni wake.mchezo ukawa huo,nalia baadae namsamehe.na kipindi chote hicho sikuwahi cheat ingawa nlitongozwa mno na mi ni mtu ninaejiheshimu.mazoea na wanaume sinaga.nlimvumilia kwa miaka mitatu,siku akafanya tena nkajiskia moyo umechoka kabisa mateso nkaamua enough is enough nka break up mazima. Mara ya kwanza nlivomuacha hakushtuka,akijua ntarudi tu kama zamani.siku zilivoanza kukatika,akajua I was serious ndo akaanza kutapatapa begging me back kwa kila namna na mara kibao alikuja kwangu na kukesha nje hadi asubuhi akiomba nimsamehe.mi nkiamka majirani ndo wananiuliza imekuwaje wamemuona mtu kashinda nje kwangu usiku kucha.by then nkakutana na kijana mwingine anaenipenda sana na kikubwa nlichompendea huyu kaka,haoneshi kabisa kuyumbishwa na wanawake.ni mtu ambae anaweza mtukana msichana mbele yangu anaetaka kuleta mazoea,jambo ambalo sikuliona kabisa kwa ex wangu.ex wangu mara zote alikuwa bize na simu,kutwa anaflirt na wasichana.sasa saivi its already a year na ex hajaacha kuniomba nimrudie.katumia kila njia,kawafuata ndugu zake,kaenda kanisani,kawafuata ndugu zangu,amekuwa akinunua zawadi za kila aina.anatumia kila mbinu na amekuwa akiwaeleza watu amenikosea anaomba wamsaidie kuniomba msamaha.mimi kila nkiwaza kurudi,moyo unasita nkikumbuka the sleepless nights na nlivotesekea mapenzi.na kikubwa nna mpenzi who really loves me...
Naombeni ushauri,sababu at this point naona inaniweka in a sort of dilemma.najikuta naogopa kuja kuumizwa tena na my boyfriend,what if nae atabadilika huko mbeleni na my ex is really sincere anatubu.au nikaja mrudia ex,kumbe ni usanii tu akaja niumiza na hali nimemuacha a good man away who seemed to truly love me.
....Naombeni ushauri na si matusi!...asanteni.

Dah huyo jamaa ana roho.. Mie siezi yani dunia ina watu 6billion afu we mmoja unilaze nje? What for? Listen to your heart only, jiandae kwa lolote litakalotokea, huwez predict future hakuna aliekamilika 100% huyo at least unajua udhaifu wake, na huyo mpya uanze from scratch tena?

Chukua peni na karatasi, andika orodha ya sifa za mwanaume wa kuwa nae afu uanze kuwapa marks in each particular item. Atakaepata nyingi ndio huyo huyo, JIANDAE KWA LOLOTE u never know who wiil be who at this stage more than God knows
 
Binti kimbia usigeuke nyuma,naona hutujui wanaume.Ulikonda miaka mitatu,sasa utakonda mpaka kufa.Umesema alikuonesha His true color,sasa hivi atakuonesha anaetengeneza hizo true color shauri yako!
 
Jambo kubwa na zuri kwako uliweza kujitambua mapema kuwa huyo uliyenaye siye!!! Jiamini ndani yako yakuwa hujafanya makosa kumbwaga huyo mtapeli wa mapenzi.

Mwambie neno moja "haijapangwa ninyi wawili mkaishi pamoja" , ila msamehe kweli toka moyoni ili dhambi yenu isiendelee kuwatafuna.

Nakutakia kila la kheri...
 
yaani ushauri wote huo bado hujapata cha kufanya ?
MWAMBIE AKUOE MUKIWA HAPO CHUONI ,SHEREHE BAADAE HAPANA ZINAA
 
Ukikosea uoe mwanamke kama huyu utakula hasara kubwa....

Ndio maana watoto wa mjini wanasema usioe mwanamke aliepita phase na mwanaume mwingine,, wanamaanisha mwanamke yeyote ambaye ameshapita strong relation kiasi cha kuwa slave wa mwanaume mwingine ni ngumu sana kumfanya atulie..

Maana kila atapokutana na yule X wake u slave unarudi na anamegwa kama kawa
 
Mkuu Dr. Wansegamila naona umefunguka kweli kweli. Uswahilini tunasema umemwagika mzima mzima. Much of what you opened up is a true reality lived in the world of love. What I can advise is that You will be doomed if you eat your own vomit. Simply put

Usirudi nyuma dada yangu, utakuja kujuta maisha yako yote ukimrudia huyo ex wako,hana lolote. Ngoja nikwambie kitu kuhusu sisi wanaume huwa hatubadiliki hata siku moja;huyo ex wako ni kicheche na hakuheshimu wala hakupendi na ukweli utabaki hivyo milele bila kujali sasa hivi anakubembeleza kiasi gani umrudie. Ukijiroga tuu kurudi utajuta,and it will be too late. Kinachotokea sasa ni vile tuu amemiss the way u used to cry and beg for him;the way u used to worship him(if i may say so),ile yeye kuwa na authority ya kukunyanyasa na wewe kuwa helpless about it,na hiyo huwa unaweza kumfanyia msichana anaekupenda kiukweli kweli sana,na akakuvumilia,sasa tangu umuache hana tena mtu wa kumfanyia hivyo,he will say all the words and he will do anything to get that back,ila haimaanishi kwamba anakupenda. Once he get that chance again, utakiona cha mtema kuni. Umempata mtu anaekupenda move on dada. Ukifanya kosa na kumrudia huyo ex utakuja kulilia chooni.
Ngoja nikumegee siri nyingine kuhusu sisis wanaume dada yangu, ukiona mwanaume anakucheat mpaka anaonyesha waziwazi kuwa anakucheat, na hajali wala haonyeshi kujutia hata ukijua kuwa ancheat jua kuwa huyo mwanaume hajawahi kukupenda,hakupendi wala hatakuja kukupenda maisha yote ya duniani na ahera, that is a fact. Ni hayo tu.



Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Last edited by a moderator:
King'asti nimekumiss ghafula.
Ha ha ha ha. Insanity na upumbavu vinakaribiana eh? Kweli duniani kuna mengi.

Dating your ex is same as doing the same thing in exactly the same way and expecting different results. Which is a perfect definition of insanity



Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Last edited by a moderator:
Labda tuwe tunawacharaza na viboko ndo tuwape ushauri muelewe

sasa urudiane nae kwani umekogwa?

stupid girl....

Mi nawashangaa sana hawa watu

Hivi unakuaje msahaulifu kiasi hiki?

Tena unasahau kijinga hivi?
 
MadameX tatizo la baadhi ya wanawake wanadhani mwanaume akisaga goti na kulia machozi ya maji ndo wanadhani wanapendwa na kunyenyekewa.
We unadhani kwa nini ameandika kichwa cha habari STRANDED!?
Yupo njia panda anataka kurudia kula matapishi wakati kuna msosi unachemka pembeni yake.
Namsubiri arudiane halafu tunampa wiki 1 tu ya kuja kulia tena.


Duuh unampenda pressure wewe....miaka yote umekuwa nae hakukups respect sasa eti anaomba msamaha na wataka umrudia...holy ----!

Bado kumbe hujawajuwa wanaume. ...rudi ukalizwe tena



Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Last edited by a moderator:
hasara tena sana harafu anasema anajieshimu! uyu mwanamke ni hasara kweli. ukioa kama uyu ni kujutia na majanga.

Inaonekana ajui nin akitakacho. magume gume unaweza piga mpaka ukaua. sasa uyo jamaa yake mpya sijui anajisikiaje akigundua hivi.
Mkuu money stunna ....wewe embu fikiria kama jamaa anpanga mipango yake anajua mchumba yupo alafu demu anakuja kumwambia ninarudi kwa zamani.....hawa ndo wale mpaka kwenye ndoa bado wanakuwa na mawenge wenge unakuta unasema nimeoa nitulie ...lkn unakuta hamna utulivu wala nini..
 
Chukua peni na karatasi, andika orodha ya sifa za mwanaume wa kuwa nae afu uanze kuwapa marks in each particular item. Atakaepata nyingi ndio huyo huyo,
Mkuu aminia wewe, hii inaitwa mathematical way of calculating future risk!!! Sasa sijui kama ina-apply mpaka kwenye kumpata mke/mume
 
Ukikosea uoe mwanamke kama huyu utakula hasara kubwa....

Natamani huyo boyfriend mpya apite kwa bahati mbaya asome huu uzi hapa halafu kwa bahati nzuri awe anajua story ya huyo girlfriend wake.
Dadeq! Huyu dada lazima alambe kibuti cha mgambo.
Hili hata halikupaswa kufika hapa.
Inatia hasira hizi thread nyingine jamani!


Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Ndio maana watoto wa mjini wanasema usioe mwanamke aliepita phase na mwanaume mwingine,, wanamaanisha mwanamke yeyote ambaye ameshapita strong relation kiasi cha kuwa slave wa mwanaume mwingine ni ngumu sana kumfanya atulie..

Maana kila atapokutana na yule X wake u slave unarudi na anamegwa kama kawa
....Ni hatari sana mkuu...ukiingia kwenye ndoa na mwanamke kama huyu unaweza usifanye lolote la maana....wewe kila siku unakua kwenye arguments tu....na hamna kitu inaleta umaskini kama kila siku kuawa kwenye argument za mapenzi rather than argument za mambo ya maendeleao
 
Na hili ndo tatizo linalofanya wanawake wengi waendelee kubuzi buzi mda unaenda hawaolewi halafu wanasema wanaume vimeo wakati wenyewe ndo manungayembe waliokosa msimamo. Nakasirika. Ngoja niendelee kukasirika

Mkuu money stunna ....wewe embu fikiria kama jamaa anpanga mipango yake anajua mchumba yupo alafu demu anakuja kumwambia ninarudi kwa zamani.....hawa ndo wale mpaka kwenye ndoa bado wanakuwa na mawenge wenge unakuta unasema nimeoa nitulie ...lkn unakuta hamna utulivu wala nini..



Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Natamani huyo boyfriend mpya apite kwa bahati mbaya asome huu uzi hapa halafu kwa bahati nzuri awe anajua story ya huyo girlfriend wake.
Dadeq! Huyu dada lazima alambe kibuti cha mgambo.
Hili hata halikupaswa kufika hapa.
Inatia hasira hizi thread nyingine jamani!



Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
Mkuu hekima tele wanawake kama hawa huwa wanasumbua kishenzi.....ni wale wanawake ambao wanaangaka na mapenzi muda mwingii...na mara nyingi ukiwa nae utakuta na wewe unaangaika na mapenzi tu badala ya kufanya mambo mengine....
 
we sijakuelewa kabisa.. unataka umrudie ili nini????

labda utujuze hapo.

halafu pili huyi uliye nae ni kwamba humpendi au?? coz i dont real get it, uko na mtu halafu bado unahaha na mtu aliyekuumiza miaka nenda rudi.
 
Jamani mumenishambulia kweli kweli!nawashukuru though..imenijenga.na si kwamba nlikosa msimamo,mjue tu pia ukishatendwa mtu unakuwa na a lot of insecurities of hata kuingia in a new serious relationship.its human.naomba mnielewe.nampenda sana my boyfriend.he completes me.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom