Strabag ni janga jingine

Kweli hili ndio Janga la TAIFA??
 
kampuni hii wanafanya kazi vizuri sana tusipende vitu vya haraka alafu havina ubora jamaa wameaminiwa na serikali ndio maana ata bara bara kuu ya tanga-kilimanjaro pia wanatengeneza
my take; tusiwe na haraka tuwaache wapige kazi.
 
Je tukisema wewe ndio umekosea tutakua tumekosea??
 
Je tukisema wewe ndio umekosea tutakua tumekosea??
Huo ni mtazamo wako wewe. Ingekuwa vizuri kama wewe na wenzako mkajifunza kutoka kwa kandarasi anayejenga barabara ya Mwenge-Tegeta. Pamoja na kuwa moja kati ya barabara zenye madaraja mengi tena makubwa lakini wanafanya kazi kwa mfumo mzuri sana.
 
je kazi ya mwenge tegeta na kimara-kivukoni zinalingana??kwanza mwenge-tegeta ni 4 WAYS while kimara-kivukoni ni 4WAYS plus 2 CONCRETE ENFORCED BUS LANES......msiwe wepesi kulaumu
 
je kazi ya mwenge tegeta na kimara-kivukoni zinalingana??kwanza mwenge-tegeta ni 4 WAYS while kimara-kivukoni ni 4WAYS plus 2 CONCRETE ENFORCED BUS LANES......msiwe wepesi kulaumu
Kwani kanuni na taratibu za Kidaktari zinatofautiana katika kutibu mtu mwenye ugonjwa wa muda mrefu na yule wa muda mfupi?

Kinachongelewa hapa ni mapungufu katika kufuata usalama na usumbufu kwa watumiaji wengine wa barabara wakati wote wa ujenzi.
 
hayo yote ulioelezea hapo juu yanategemea uzito wa kazi.......tena mshukuru mnapita kwa shida otherwise hio barabara ingefungwa kabisa mzunguke mandela road......usifananishe kujenga simple 4 lanes za mwenge-tegeta na kujenga 4 lanes plus 4 complicated bus lane reinforced with concrete,special bus stops,pedestrian flyovers,complex intersections.....hata angekuja mkandarasi kutoka MARS lazima usumbufu uwepo.....u cant have ur cake and eat it.....either u eat it or u have it.....so tujenge tupate usumbufu au tusijenge tupite kwa "raha".....kwa sisi wapanda daladala tunaomba wajenge tu itatusaidia sana.
 
Kaka taratibu ndo mwendo ....ikianza kuwa na NDITA..aka..MAKUNYANZI utarudi tena jamvini na kuwakandia...upande mmoja ukibinuka kuliko mwingine hukawiii kunena

Wanapata shida kwa sababu miundo mbinu ya maji masafi, taka, umeme, simu, mkonga wa taifa, yote ipo eneo la barabara haijahamishwa kupisha ujenzi...WEZI wanahujumu vitendea kazi

Wana vifaa vya Kutosheleza, wanastahili pongezi 😛lane:
 
Sasa mimi nimesema nini na wewe unaongelea nini? Hao watu wako unaowasifia sijui kwa kazi kubwa ni heri wangefanya busara kufunga kabisa hiyo njia mpaka hapo watakapo maliza ili watumiaji wengine wa barabara wakajua moja, kuliko wanavyofanya ina maana hata madaladala ambayo wewe umesema unapanda yangeweza ku-diverge na hata abiria nao wangejua waende wapi ili kupata usafiri wa kuwapeleka wanakoelekea kwa urahisi na usalama zaidi.

Sasa kwa hali kama hiyo daladala linalazimika kukaa kwenye foleni masaa kadhaa kwa kipande kifupi tu cha umbali na likijaribu kuchepuka barabara nyingine Traffic Police wanalikamata. Wamiliki wa vyombo vya usafiri tunaumia sana mkiongezewa nauli kidogo tu makelele mengiii.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…