Story ya kweli. Nahitaji ushauri

Cefixine

Member
Dec 17, 2019
22
28
Wakuu habarini, hii ni story ya kweli iliyonitokea na hili jambo linanipelekea kukosa amani na kuwa mtu wa stress sanaa.
Miaka kadhaa iliyopita nilipata fursa ya kuongeza elimu katika chuo kimojawapo (dsm tz). Wakati nasoma nilikutana na binti mmoja (Jeni sio jina halisi). Huyu Jeni alikuwa muislamu na mimi mkristo, nakumbuka ilikuwa ni mwezi mtukufu ndio nilianza kumzoea na kipindi nasoma sikutaka kujulikana kama naongeza elimu but niliishi kama sijaajiriwa, hivyo nikawa namsogeza karibu kama rafiki.

Kiukweli jeni alikuwa wa familia yenye uwezo sanaa,baada ya miezi sita tukawa wapenz tukaishi vizuri sanaa,baaada ya miaka kama miwili jeni alichange na kwa mara ya kwanza niligundua amenicheat na alikiri amefanya hivyo sababu kubwa alidai kuwa mimi sina muda na yeye na sometime akinihitaji hanipati,hii ni kweli kutokana mm nilikuwa nashughuli zangu nafanya na sikutaka ajue kwa kipindi hiko,tulisameheana na maisha yaliendelea miezi kama sita mbele tuliplan kuoana na mambo ya family.

Siku moja aliniaga anakwenda kuona ndug yake na atarudi baada ya siku tatu iv cha ajabu asubuhi yake namwona (tulikuwa tunaishi karibu ila yeye alikua akiishi na rafiki yake ),nilivyomwona nikampigia cm na kumuuliza kulikoni akaniambia nakuja tuongee kwel akaja akiwa kabeba pochi alivyofika akaniambia naenda uwani (hapa ndipo tatizo lilianza), alivyoenda tuu nikafungua pochi nikakuta P2 ( vidonge vya kuzuia utungaji wa mimba) zimeshatumika alivyorudi tukaongea na akaniambia aliamua kurudi usiku, nikamuuliza kuhusu p2 akanijibu kua alikuwa anahamu na mm hivyo aliamua ameze kabisa.

Baada ya mwezi nilikuwa nimetoka nae ghafla akapigiwa cm na mwanamke wakaanza kuzozana nilivyomuuliza akasema ni ndug anamsumbua, bhas nikaamua kumwita rafiki nikamwambia naomba ufatilie cm ya jeni msg zake na anachart nin kweli akafanikiwa na akaniambia kuna dada anagombana nae kua katembea na mume wake,nikamwambia naomba namba za uyo dada,baada ya week akaniambia kuna kaka ambae ni mume wa yule dada wanachart sanaa,nikachukua hizo namba

Kiukweli nilimtafuta yule kaka nikamtumia msg moja( kama upo huku nisamehe) "xx naomba achana na jeni utanikwaza na mm sitosita kukuharibi" hakunijibu chochote,siku moja nikamtafuta mke wa xx nikamweleza unamfahamu jeni kiukweli yule dada(ane) alinieleza kila kitu na picha akanipa sasa nikipiga mahesabu ile siku niliyomkuta jene na p2 ndio siku walitkutana na kusex na xx.

Baada ya siku tatu ane (mke wa xx) alinitafuta na kuniomba tuonane kweli tulionana na tukaongea mengi akaniomba na pesa nikampa na baada ya siku 6 nililala naye, na nikaweka ushahidi ambao nilijua jeni akiona ataumia na pia xx akijua ataumia, na kweli walijua ila baada ya kujua yule mpenz wang tuligombana na alinilaumu sanaa kwa kile kitendo na hata mume wa yule dada ilibidi anitafute ila nikamwambia nilikutumia msg nikikutaja uachane na mpenz wangubl uligoma na hukujibu so na wew pata uchungu,baada ya hapo yule mwanamke hatuelewani na masomo tulishamaliza zaid ya miaka sasa.

Kwanini naomba ushauri
Ndugu zang kwanzia hapo nimekuwa nakunywa pombe ila bado, kutongoza siwezi kabisa na hata nikiona mwanamke mzuri vip nikishamvua ngua namwacha na care sina hata ya salamu,nimetamani kutembea na vitoto 21-25 nimevichoka nimejaribu watu wazima 35-45 nimewashindwaa( binafsi nina 30).

Nimenunua malaya ila hua silali na mwanamke bila kumpima HIV na homa ya ini (hepatits B) na katika haya nimesha wapima wanawake na nilikutana na +ve. Kwa sasa najiona kama nadata na haya maisha kisa hili jambo na huenda nikashidwa kulimaliza, naombeni ushauri nifanye nini maana naumia sanaa na sijui pa kutokea ni wapi?
 
pole sana rafiki yangu...tatizo ulimpenda sana huyo Jane wako...
kaa ukijua kuwa kukutana kwako na Jane lilikuwa ni darasa. unachotakiwa kwa sasa ni kukubali matokeo na kuamua tu moja kumtoa jane kwenye kichwa chako.

swala la mapenzi haswa maumivu huwa linawaumiza wengi sana wewe sio wakwanza....ila kitendo cha wewe kujikita kwenye unywaji wa pombe na ngono uzembe kinaweza kukuletea matatizo makubwa zaidi....jifikilie ulipo kosea kama uwezo unao tafuta mwanamke uoe...

acha Pombe acha ngono uzembe...mwenyezi Mungu akuongoze Rafiki yangu
 
Uwezo ninao ila upendo umenitoka.

Hao viumbe sio wa kuwaamini Sana, ukiwagegeda tu Una wadelete kichwa kwako unaishi nao Kama jumba bovu tu muda wowote linaoromoka. Basi wala hawakupi shida
Lakini ukijiaminisha papuchii yao utaichakata pekeyako tu itakula kwako
 
Hiyo hali nilishakutana nayo kidogo tu nife kwa mawazo maana mi ilinitokea kwa Ke 2 tofauti kwa mfululizo.
Mshirikishe Mungu, jichanganye na Watu tofauti kutaniana/kubadili mawazo mbali mbali ya kimaisha, fanya mazoezi, jiweke bize kikazi, pumzika kwa muda sahihi na tambua uhai wako una thamani zaidi ya Jane.
 
Aisee pole,kupenda kupenda kiasi hicho kuna umri wake lakini bado 30yrs na unadaka si bure umerogwa.
 
Sina sababu ya kukupa pole. Tatizo lako sio Jeni wala mapenzi.
Tatizo lako ni kichwa chako. Tatizo lako ni kuruhusu hisia (feelings, emotions) ziongoze akili (utambuzi).

Na hili lipo wazi, Hisia zinapoongoza akili haya hutokea:-

1. Uliacha lengo kuu(kusoma) ukazama kwenye mapenzi. Wenzako tukiwa vyuoni huwa tunachakata matunda lakini sio kwa hisia bali kiridhisha mwili.

2. Unagundua mwanamke amekusaliti halafu eti tukakaa tukayamaliza. Aliyekwambia mwanamke huwa anaacha usaliti ni nani?

3. Unaumia kusalitiwa, wanaume huwa tunatafakari baada ya kusalitiwa,kisha unafanya maamuzi magumu. Ulipaswa kusitisha uhusiano.

4. Ukamtumia meseji ya vitisho bwana wa mwanamke wako. Huo ni udhaifu mkubwa sana. Mwanamume anayemgonga mkeo akiona unaanza kumtisha kwa vimeseji huwa anakuona boya zaidi. Hisia zikakuongoza kuacha kushughulikia tatizo kuu ambalo ni huyo mwanamke ukahamia kwa mwanaume wake.

5. Kukutana na huyo mwanamke wa jamaa aliyekuwa anakugongea mwanamke wako. Ulikutana naye kujadili nini? Hayo sio maamuzi ya akili bali hisia na mhemuko.

6. Kulipiza kisasi kwa kutembea na mwanamke wa jamaa. Hapa hisia zilikufanya uhisi kwamba unasawazisha mambo kwa kutembea na mke wa jamaa. Je ulipata farijiko lolote? Je ilisitisha mahusiano kati ya Jeni na jamaa yake? Mihemko tu.

7. Kuanza kulewa na kubadili wanawake. Yaani una akili ndogo kiasi ambacho Jeni anaharibu maisha yako na ya familia yako? Je wewe ungemsaliti unadhani Jeni angefanya huo ujinga unaofanya. Unadhani familia yako na maisha yako yajayo (future) itakuwaje kama utaendeleza tabia za kijinga na za kitoto kwa kiwango hicho? Mapenzi huisha, jambo la muhimu ni kujua kutoka kwa usalama.

Embu fikiria maisha yako yajayo na familia yako. Huna baba, mama na wadogo zako ambao wanakuangalia kwa matarajio ya kuja kuwasaidia huko baadaye?

Ukiendelea hivi utafanya tukio la ajabu, usikute umeshawaza kumdhuru Jeni au jamaa yake. Na labda umeshawaza pia kujidhuru wewe mwenyewe. Maisha yako yapo hatarini.

Ndio maana baadhi ya familia mtoto wa kiume huwa unawekwa chini na baba, wajomba na hata kaka zako ili wakupe ushauri juu ya mahusiano. Hii inasaidia sana kuelewa masuala ya mapenzi kuliko kukua kindezi matokeo yake unakuja kuchanganyikiwa kwa papuchi uliyoikuta chuoni. Ubwege huu.

TUMIA AKILI ACHA MIHEMKO.
 
aiseee mm nilijua kina dada ndo hukanyaga miba kumbe hadi wanaume.

pole sana mkuu, kina dada wako hivi huwa wanajipa likzo hata mwaka sio kwamba hawapendi ila wanajicomit kuto ingia kwny mahusiano

kiufupi hii process n kama river rejuvenation
 
Mkuu nilichokukubali ni kitendo cha kumtafuna mke wa mwizi wako.. huo ni ujasiri na kitendo cha kuigwa katika jamii. Mtu akikulia demu wako usiwe mnyonge.. na wewe LIPIZA
Hapo mkuu nimemkubali ila ilitakiwa baada ya hapo apige chini Jane na huyo mke wa jamaa then aendelee na maisha yake bila tatizo
 
Nimeelewa nashukuru ila kuhusu kusoma na kuendekeza mapenzi,kumbuka wakati huonnilikuwa tayari na kazi na nilikuwa naingiza over 2M per month so ilinifanya niishi maisha tofauti na ya kiuanafunzi
Sina sababu ya kukupa pole. Tatizo lako sio Jeni wala mapenzi.
Tatizo lako ni kichwa chako. Tatizo lako ni kuruhusu hisia (feelings, emotions) ziongoze akili (utambuzi).

Na hili lipo wazi, Hisia zinapoongoza akili haya hutokea:-

1. Uliacha lengo kuu(kusoma) ukazama kwenye mapenzi. Wenzako tukiwa vyuoni huwa tunachakata matunda lakini sio kwa hisia bali kiridhisha mwili.

2. Unagundua mwanamke amekusaliti halafu eti tukakaa tukayamaliza. Aliyekwambia mwanamke huwa anaacha usaliti ni nani?

3. Unaumia kusalitiwa, wanaume huwa tunatafakari baada ya kusalitiwa,kisha unafanya maamuzi magumu. Ulipaswa kusitisha uhusiano.

4. Ukamtumia meseji ya vitisho bwana wa mwanamke wako. Huo ni udhaifu mkubwa sana. Mwanamume anayemgonga mkeo akiona unaanza kumtisha kwa vimeseji huwa anakuona boya zaidi. Hisia zikakuongoza kuacha kushughulikia tatizo kuu ambalo ni huyo mwanamke ukahamia kwa mwanaume wake.

5. Kukutana na huyo mwanamke wa jamaa aliyekuwa anakugongea mwanamke wako. Ulikutana naye kujadili nini? Hayo sio maamuzi ya akili bali hisia na mhemuko.

6. Kulipiza kisasi kwa kutembea na mwanamke wa jamaa. Hapa hisia zilikufanya uhisi kwamba unasawazisha mambo kwa kutembea na mke wa jamaa. Je ulipata farijiko lolote? Je ilisitisha mahusiano kati ya Jeni na jamaa yake? Mihemko tu.

7. Kuanza kulewa na kubadili wanawake. Yaani una akili ndogo kiasi ambacho Jeni anaharibu maisha yako na ya familia yako? Je wewe ungemsaliti unadhani Jeni angefanya huo ujinga unaofanya. Unadhani familia yako na maisha yako yajayo (future) itakuwaje kama utaendeleza tabia za kijinga na za kitoto kwa kiwango hicho? Mapenzi huisha, jambo la muhimu ni kujua kutoka kwa usalama.

Embu fikiria maisha yako yajayo na familia yako. Huna baba, mama na wadogo zako ambao wanakuangalia kwa matarajio ya kuja kuwasaidia huko baadaye?

Ukiendelea hivi utafanya tukio la ajabu, usikute umeshawaza kumdhuru Jeni au jamaa yake. Na labda umeshawaza pia kujidhuru wewe mwenyewe. Maisha yako yapo hatarini.

Ndio maana baadhi ya familia mtoto wa kiume huwa unawekwa chini na baba, wajomba na hata kaka zako ili wakupe ushauri juu ya mahusiano. Hii inasaidia sana kuelewa masuala ya mapenzi kuliko kukua kindezi matokeo yake unakuja kuchanganyikiwa kwa papuchi uliyoikuta chuoni. Ubwege huu.

TUMIA AKILI ACHA MIHEMKO.
 
Iliwahi nitokea kumpenda mtu kupitiliza, lakini nilivoona haeleweki, nikahamishia hasira kwenye pesa. Nilikuwa kila nikikumbuka napata hasira ya kutafta pesa kwa nguvu zote
 
Nimeelewa nashukuru ila kuhusu kusoma na kuendekeza mapenzi,kumbuka wakati huonnilikuwa tayari na kazi na nilikuwa naingiza over 2M per month so ilinifanya niishi maisha tofauti na ya kiuanafunzi
Sote tumesoma, wengine pia walitoka kwenye familia tajiri lakini bado walijua walichofuata shule ni elimu na sio mapenzi.
Wengi wamefanya ngono vyuoni ili kuridhisha mwili sio kujitoa moyo na hisia.
Unajitoaje moyo na hisia kwa binti uliyekutana naye akiwa na miaka 20+?

Ninachosisitiza hapa ni wewe kuchanganyikiwa kwa sababu ya Jeni.

Wenzako tulikuwa tunawapanga foleni kwa kuwa tunajua, wadada wengi wa chuoni wana mabwana zaidi ya wanne.

1. Mtaani kwake ameacha bwana
2. Chuoni anaweza kuwa na bwana Lecturer
3. Akienda field anapata bwana huko huko ofisini.
4. Kanisani kwako napo pia ana mwanaume ambaye anamsubiri kama mchumba.
5. Kuna jamaa pia anampatia mahitaji madogo madogo.

Ridhisha tamaa zako za kingono, usiweke hisia, watu hubadilika.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom