KIJANA SHUJAA….. “Ilikua ndoto yangu kuja kufanya jambo kwaajili ya Taifa”
SEHEMUYA PILI (02)
Man Middo
“Ama hakika kila mtu ana nafasi yake, kila mtu ana umuhimu wake kwa jamnii yani watu wanaopanda ndege na kulipa nauli kubwa si chini ya laki lakini leo wanaokolewa na mvuvi!? Kweli mheshimu kila anaekatiza mbele yako huwezi jua kesho yako atakusaidia nini”
Ilikua ni baadhi ya minong’ono kutoka kwa watu wakitoa maoni yao kutokana na mazingira ajali ilivyotokea. Watu wengi hawakua wakiamini kile kilichotokea, lilikua kama jambo lisilowezekana. Lakini ghafla kule kule kwa Millard Ayo ‘Rais Samia aguswa Ajali ya Ndege ya Precision Air kayandika haya..
“Natuma salamu za pole kwa wote walioathirika na ajali hii, tuendelee kuwa watulivu wakati huu zoezi la uokoaji likiendelea huku tukiomba Mwenyezi Mungu atusaidie”
Wakati watu wakihangaika na zoezi la uokoaji mara ghafla tarehe 7 Novemba 2022, BBC Swahili nao wakaibuka na taarifa yao kutoka kwa majeruhi hospitalini ikisema “Mvuvi alivyojaribu kuwaokoa marubani wa ndege iliyopata ajali"
‘Mvuvi ambaye alikua mmoja wa watoa huduma wa kwanza katika eneo la ajali ya ndege iliyoua watu 19 katika Ziwa Victoria nchini Tanzania, ameeleza jinsi alivyojaribu kuwaokoa marubani waliokua wamekwama kwenye chumba cha rubani na jinsi alivyokaribia kupoteza maisha’
“Akihojiwa akiwa hospitalini kwake katika mji wa Bukoba, Majaliwa Jackson alisema aliingiwana hofu baada ya kuona ndege hiyo ya abiria ikija kutoka upande usiofaa, kabla ya kutumbukia Ziwa Victoria”
Hakika washukuriwe BBC Swahili kwa kuwahoji majeruhi hospitalini, wao ndio sababu ya kubadilisha jina la kina wetu kutoka “Mvuvi alivyojaribu kuwaokoa marubani wa ndege, Hadi Kijana shujaa aliyeokoa watu 24 katika ajali ya ndege”
Kijana shujaa akahojiwa akafunguka kwa rafudhi yake ya kihaya…“Nikasogea hadi eneo la tukio, kufika nikakuta bado wanahangaika kufanyeje, kufungua mlango. Ule mlango ulikua kama vile umejilock, mimi nikashika ile kasia niliyokua nayo nikapigisha kwa nguvu ndio mlango kufunguka na watu wakaanza kutoka.
“Sasa mimi nikahamia upande wapili, upande wa rubani kidogo mimi mazingira ni nyumbani, kidogo mazingira kuogelea kidogo najua. Nikawa nimezama nikaingia hadi kumuona rubani, rubani akawa ananielekeza nipasue kioo, ile kupasua kioo nikaibuka juu pale huwa kuna walinzi wa uwanja wa ndege pale airport nikawambia kama wanakifaa chochote cha kuvunjia watusaidie wakawa wametuletea vishoka vidogo hivi”
“Sasa ile naelekea kuvunja ndio akaja mwanaume mmoja hivi akiwa na honi ya kutangazia (Kispika cha msemaji wa simba) ndio akawa amenizuia akasema hapana niachane nayo nisivunje kioo kwasababu rubani wanawasiliana nae kwenye simu inamaana anawaambia kuwa maji kule alipo hayapo yanaingia kidogo kidogo.
Lakini mimi nikawa nimemwambia maji yana kasi mpaka maji kuanza kuingia kidogo kidogo hapo sehemu yanapopita yanaforce kuingia. Kwahiyo ndio akawa amenisihi kuwa nisifanye hivyo, mimi hapa nikazama nikampungia mkono wa kwaheri rubani lakini akanionyesha pembeni kuwa kuna mlango wa emergency”
“Kwasababu sehemu ya Rubani walikua watu kama 6, itakua ni wale marubani wote wawili na wahudumu kwahiyo wote walikua kule sehemu ya rubani ile tungefanikiwa tu kuvunja kioo nina imani wote wangekua salama”
“Mazingira tuliyokua, ndege kwanza ilitokea maeneo ya kiyaka uku, ambacho ni kitendo kisicho cha kawaida sijawahi kuona. Ikaelekea kastama baada ya kuja kastama ndio ikaja na spidi ndogo na kuzama majini.
Sasa pale tulikua jopo kama unavyotuona hivi tulikua karibu na kazi, ndio tukachukua kimtumbwi kidogo tukasogea hadi eneo husika ndio tukakuta wanaomba msaada wakufunguliwa mlango kwasabu milango ilikua imejilock, ndio tukatumia zile kasia kufungua ule mlango ndio wakawa wametoka.
Baada ya hapo ndio tukaanza harakati za kusogeza ndege nchi kavu, tukawa tumefunga kamba ili tuweze kusogeza ndege, ndio ile kamba ikakatika nakunipiga sehemu ya uso kwahiyo hapo ndio nikazirai na kujikuta hospitalini”
Maelezo ya dakika 3 na sekunde 15 yakabadilisha taswira nzima ya maisha ya Majaliwa Jackson, yeye mwenyewe hakuamini na hakujua kama mahojiano yale yanaenda kubadilisha maisha yake yote……………….ITAENDELEA. Tuendelee kusubiri Breaking News hapa hapa.