Story: Kariakoo

Story: Kariakoo

Money Penny

JF-Expert Member
Joined
Jun 20, 2016
Posts
18,204
Reaction score
17,560
Tarime one Ngosha Mashine hilalahmed Proffesor bandamo mahondaw Smart911 lekumok HHHK Kyalow Jiwedogo Vladmir Putin

SEHEMU YA 1

A. 1980 - 1983 (CHUMA CHA MOTO)​




Jamani nisaidieee jamaaaani nakufaaaaaa, huku akiwa anakimbia kuelekea mahali asipopajua, akaja kutokea kwenye barabara ya mtaa wa uhuru, giza nene anaona msongamano wa watu wanapita kwa miguu wanawahi, si unajua miaka hii kupata usafiri ni kazi, kwanza magari hamna ya kusubiria, zile UDA UDA bado zilikuwa hazijaja ni kuchanja mbuga kwenda mbele

akapumua afadhali, akajichanganya na wale watu akawa anatembea mpaka nyumbani kwao KARIAKOO!

kufika mama yake anamwuliza, vepe hawa ulikuwa wapi mbona unatoka jasho kama umekimbizwa? kuna nini mbona unahema namna hii!

Hawa: hamna mama hamna kitu

Mama😛ole nimeshapika na maji alikuja Jafari akanijazia leo hamna kazi wewe nenda tu kaoge alafu uje ule ufanye masomo yako ulale, ila kesho usichelewe tena kama leo sijui ulipatwa nanini masikini

Hawa: akaingia kuoga lakini hakuwa na amani na hakuelewa yule mtu ni nani, na kwanini alimfanyia yale aliyomfanyia maana hajawahi kukutana na kitu kama kile ingawa hakikubana sawa sawa, akafanya mambo yake akalala, usiku mzima anawaza na kuota kile alichofanyiwa, movie ikajirudia kichwani mwake mwanzo mwisho! kuamka asubuhi mashuka hayafai!

asubuhi kufika shuleni masomo hayapandi anawaza chuma cha moto cha jana usiku, kidato cha nne sasa lazima niwe makini na masomo akajiambia moyoni, kila akimsikiliza mwalimu hamna kitu kinapanda, Somo la Kiingereza ndio kabisaa hata halipandi anaona maluweluwe

walipokuwa kwenye maongezi na shoga wake Maija kipindi cha mapumziko ya kipindi na kipindi, akaamua kufungua

Hawa: Maija mama mimi naona shule imeshanishinda, akili yangu yote inawaza chuma cha moto

Maija: chuma cha moto ndio nini tena nawewe

Hawa: we bwana na wewe hukui tu, chuma cha moto maanake machine ya mwanaume

Maija: akacheeeka sana sana sana! haiwezekani Hawa upo serious na hili

Hawa: akampa picha na mkanda mzima wa yaliyomkuta jana wakati anarudi toka twishen, walichelewa sana kurudi nyumbani, akampa maelezo yote Maija anashangaa heee!

Hawa: tangu aniingizie kile chuma cha moto maija natamani anirudie ila naogopaaaa! akiwa na ukimwi si umesikia kuna ukimwi walitangaza kwenye redio juzi

Maija: ni kweli Hawa, uwe mwangalifu

Hawa: nataka leo nichelewe tena nimpate yule bwana, na hisi ni mtu anayenijua sijui kwanini, usiku sijalala namuota tu huyu bwana sijui ni nani?

Maija: haiwezekani ... leo wahi mama umwondoe wasiwasi bwana usifanye hivo,

muda wa kipindi ukafika wakatawanyika

Kweli hawa akafanya kama akili ya kichwa chake ilivyomtuma, akachelewa kurudi nyumbani lakini usiku ule hakukutana na yule mtu aliekutana nae jana mwenye chuma cha moto!

akafanya hivyo wiki nzima lakini hakuna kitu, wiki inayofuata akapita mapema kabisa,

baada ya miezi 3 akiwa anatembea kurudi nyumbani akaja kijana wa asili ya kiarabu akawa anaongozana nae, Hawa anamshangaa anamwuliza nikusaidie nini na maswali mengi

Mwarabu kimyaaa!

Hawa alipoona hajibiwi akawa anatembea haraka, mwarabu akawa anamfukuzia kwa speed ya Hawa, wakatembea walipofika karibu na nyumbani kwa Hawa Mwarabu akageuza huyoo akaondoka Hawa akawa anacheka njoo sasa kama wewe mwanaume kweli uyoooo uyooooo ile anamzomea majirani wanamsogelea vipi Hawa kuna nini tena?

Hawa akauchuna hakusema chochote akaingia kwao... hakumwona tena yule bwana wiki na wiki zikapita

Baada ya mwezi mmoja mbele tena akamwona yule mwarabu anacheza draft kariakoo karibu na mtaa wa uhuru akajibanza maana wakati ulikuwa unaruhusu na twishen haikuwepo sikuhio akamfuatilia yule mwarabu mpaka anamaliza kucheza draft yeye amejiegesha sehemu anakula machungwa!

Mwarabu wa watu akamaliza kucheza draft akapanda juu Gorofani, Hawa akasema enhee hapa hapa ndio pa kumpata mwizi wangu akachukua kanga akajitanga usoni kama mmama mtu mzima akajifunika na skirt yake ya shule akamfuata!

Kufika juu hamwoni mwarabu, eh akashangaa akajaribu kudadisi haoni mtu anatoka, akashuka sasa aondoke anaona mtu anamshika kiuno!

Kugeuka ni yule mwarabu tobaaa nimekamatwaaa wiziii

Mwarabu: mama naona umekuja mwenyewe leo, nimekuona tangu unatoka shule nikajikalisha pale nazuga nacheza draft nakuona tu nimeegesha kioo unavyonichungulia, bora umekuja mwenyewe karibu sana hapa ndipo naishi

Hawa akasimamisha roho kwa muda alafu akarudisha mapigo, akakubali kuingia nyumbani kwake, wakaongeaaaaa Mwarabu akamfanya Hawa awe huru kabisa, akampatia na chakula akala, wakaongea sana mpaka giza likaingia Hawa akakimbia kwenda kwao, hawakuonana mpaka weekend ilipofika, saa 10 jioni Hawa akaja tena kumsabahi Mwarabu akamkuta

wakapiga stori nyingi sana, Hawa akajua kuwa Mwarabu ni mkubwa kwake kwa miaka 15,anaishi pekeyake, anawazazi wapo Zanzibar, Mwarabu ni mwarabu wa Oman Muskat, Mama ya Mwarabu ni Mzanzibar Mpemba

Hawa akazidi kufurahi sana, siku hio hio akaingia jikoni kumpikia Mwarabu!

Mmwarabu akajua Yes hapa nimepata jiko!

Ilipofika saa 11 jioni Hawa akaaga, mimi nakwenda boss, tutaonana majaliwa kesho siji nafanya homework

Mwarabu akaamua kufanya yake jioni hio hio, chuma cha moto chuma cha moto kweli, Hawa alibutuliwa kusini mpaka akashindwa kurudi nyumbani ikabidi alale pale pale kwa mwarabu

J2 akalala pale kwa mwarabu, Mwarabu anajisevia kama ameoaaaa

J3 akaamkia shuleni mapema sana maana alijua wazazi walishapaniki na j3 wataamkia shuleni, kufika shuleni rafiki yake Maija anamwambia hawaaaa jamaaani umetafuuutwaaaa hakuna mfanooo!

Hawa kwani anajali sasa! kachezea chuma cha moto tangu jumamosi yeye anawaza chuma tu!

Maija kaongea wee baadae anaskia Hawa unaitwa na Mwalimu mkuuu

Kufika kwa Mwalimu mkuu akakutana na bakora hamna mfano, kachezea bakora weeee ndio maongezi baadae, Mama yake analia Hawa mwanangu nimejua umekufa ulienda wapi, Hawa kimyaaaa!

Basi siku hiyo hawa hakurudi tena darasani akaambiwa arudi nyumbani akae wiki nzima ndio adhabu yake aje j3 ijayo na barua ya msamaha

njia nzima mama yake anamsengenya hawa jamani hawa utanitoa roho mimi mama yako wewe mwanangu wa pekee nakulea tangu baba yako anitoke usinifanyie hivyo hawa jamani!

walipofika nyumbani ikabidi Hawa aseme ukweli alipokuwa, Mama yake alicheeekaaa, we hawa umepata wapi mwanaume, Hawa hakutegemea alijua atachezea bakora za kudumu

Mama Hawa: Hawa mwanangu nakupenda sana sana sana, mimi sikuzuilii kuwa na mpenzi ila naomba uniahidi kitu kimoja tu, maliza basi shule ya form 4 kwanza ndio uolewe

Hawa: mama unajua Mwarabu ndio mwanaume wangu wa kwanza, ndio maana nilishindwa kurudi hapa hata shule haikai mama, nahisi kwa hilo nitakuangusha mama yangu mpenzi

Mmama Hawa: najua na pole na hongera sana kwa kujitunza ndio maana nakuomba ujitahidi tafadhali tafadhali mwanangu maisha yetu haya ya kariakoo sio kabisa, hautaki na sisi tukaishi huko mitaa mizuri mizuri nitoe mwanangu kwenye umaskini huu mwanangu

Hawa: Mama Mwarabu ana hela anakaa hapo mtaa wa uhuru ana biashara zake za makapeti na vitambaa vya suti na nguo za akina dada, atatutoa kimaisha... ona amenipa Tsh 10

Mama yake kweli kuangalia Tsh 10 kapewa kweli akatoa macho, akamwangalia mwanae anaechezea utajiri kwenye Tsh 10 akamwambia mwanangu mimi ombi langu bado ni hilo tu maliza kwanza shule, ukaajiriwe vizuri serikalini, unitoe kwenye maisha ndoa zipo tu!

lakini hawa alishakolea chuma cha moto, hata iyo shule akaiona kama ni sheeda

Mama Hawa: kama hautojali naomba kesho niletee huyu kijana hapa nimfahamu basi,

Hawa hakuamini, akafurahi sana sana sana akamchumu mama yake akaenda kulala

Kesho alfajiri saa 12 Hawa akaamkia kwa Mwarabu,

Mwarabu: anashangaa vIpI mama kakufukuza au?

Hawa: hapana nimekuja huu mguu wako amesema anataka akufahamu

Mwarabu: du! anifahamu tena?

Hawa: ndio mpenzi huku anamchumu chumu na kumweka sawa

Mwarabu sijui ndio kakolea dozi za mabusu akakubali sawa! tutaenda kumwona, hapo hapo akapewa mrejesho, hata kazini hakuenda hata kwenye biashara wakashinda wote hapo, alasiri saa 9 wakaondoka mpaka kwa mama Hawa

akawapokea vizuri akawapa tena msosi, wakaongea hawa kimya anamsikiliza mama,

Mama Hawa: mwanangu Mwarabu maana ndio nimeambiw ajina lako, akamweleza kila kitu kuhusu familia yake, akamwambia mimi namtegemea sana mwanangu anitoe kwenye haya maisha ya KARIAKOO, naomba mhimize maana sasa hivi shule ameshaweka pembeni anawaza mapenzi, msaidie tafadhali asome, katika mapenzi yenu huko lakini elimu kwanza

Mwarabu hakuamini, alidhani anaozeshwa ndoa ya mkeka kama sio kuitiwa polisi, akajibu sawa mama hamna neno mama yangu nitamhimiza na shule itaisha

wakaongea kwa Muda mwarabu akaaga anaondoka, Hawa akamsindikiza, hapo ni saa 12 jioni,

Mwarabu: hawa mama naomba basi tusikilize kauli ya mama yetu mzuri, kwanza nashukuru umemweka mama yako wazi juu ya penzi letu lakini naomba tafadhali shule mama shule, maliza basi shule mimi nitaleta mahari, ukimaliza tu mitihani yako ya taifa mimi naleta mahari

Hawa sijui ndio ushamba au kufurahi akaamini maneno ya Mwarabu, kesho yake asbh akaamkia shulekwa malimu mkuu, akapeleka barua ya utovu wa nidhamu akamwomba sana mwalimu arudi kusoma, akamuahidi kuwa test zote hata shuka chini ya asilimia 90

Mwalimu mkuu akamkubalia, kweli baada ya miezi 3 test zote Hawa akawa anapata 90 kwenda juu

Baada ya miezi 3 mitihani ya moko akapiga, moch 1, buzy na shule mama anafurahi, mwarabu anafurahi ila chuma cha moto kama kawa!

Mock ya 2, Hawa akaifanya kama kawa, akiwa anasubiria Mtihani wa taifa, siku wanatoka Beach yetu ya feri, Hawa akawa anaanza kujiskia vibaya, oh kichefuchefu akatapika bwaaaah! kweli chuma cha moto kimezaa matunda, wakapitia duka la dawa wakanunua dawa ya kuondoa kichefuchefu, mwuza dawa akamwangalia sana Hawa akamuhoji Hawa akajibu sawa sawa, akamwambia wewe una mimba, hata miguu yako ni mizito naiona, unafanya kazi

Hawa: nasoma kidato cha nne

Mwuza duka la dawa: nakushauri mdogo wangu ifiche hii mimba maana mitihani ya taifa ipo karibuni, jifiche wanafunzi wenzako wasijui, nitakupa dawa za kutotapika ovyo ukiwa darasani jitahidi sana bora uahirishe masomo usiende kuliko kugunduklika una mimba hautafanya mitihani ya taifa

Hawa na Mwarabu wakamshukuru sana yule mwuza dawa wakarudi nyumbani, ila hawakufikia kwa mama hawa walifikia kwa mwarabu

Mwarabu akiwa mwenye furaha tele, haamini kama mpenzi wake anaenda kumpa zawadi ya mtoto, usiku huo huo akaamua kumfungulia njia ya kusogeza ujauzito vizuri tumboni, kiru! mimi money penny sikuwepo ila nimeambiwa chuma cha moto kilifanya kazi kweri kweri! ahahahahaha

Baada ya mwezi mmoja Hawa akafanya mitihani yake ya Taifa, huku Mama yake na Mpenzi wake wakiwa wameficha siri kubwa kama ile!

Baada ya miezi 6 mbele, Hawa akajifungua mtoto wa Kiume katika hospital ya Taifa ya Muhimbili, Mama yake akafurahi kupata mjukuu, Mwarabu akapata mtoto wa kiume Jembe ni Jembe, Mzurije sasa na yale manywele ya kiarabu uuuuwi Shikamoo Hawa weee

Katika kupewa jina, Mwarabu anataka aitwe Yassin, Hwana anataka aitwe jina la Marehemu Baba yake Omar!

Basi wakafikia muafaka, jina liandikwe Omar Yassin, katoto kazuuuuuri sana, wakarudi nyumbani akawa anakula uzazi kwa mama yake, kila siku Mwarabu akawa anakuja analeta matumizi pale nyumbani kwa Mama Hawa

Katoto kakakua, kakafikisha miezi 3, kliniki nini wanaenda na mwarabu, basi kale katoto kalikuwa kanapenda sana kucheka, kanacheeka ukikachekesha kidogo kanacheka sana, na akicheka anakuwa anabonyea mashavuni madimples yanatokea, basi raha kukaangalia nakwambia alafu alikuwa hata hakatai mtu!

Majibu ya kidato cha nne yakatoka bwana, Mwarabu akaenda kuyaangalia akachokaaa! akatuma baeua kule posta kwa wazazi naomba mje haraka kuna dharura hapa kwangu KARIAKOO!

Kweli baada ya wiki 2 wazazi wakaja toka Zanzibar, Mwarabu akawaelezea kiiiila kitu kuhusu Hawa, wazazi wakachoka maana walishamtafutia mke kule Oman lakini kwasababu ya mtoto aliyezaliwa wakaona sawa basi muoe tu
Baada ya mwezi mwingine m1 mbele wa Mwarabu kujipanga, na kuwa kimya kwenye maisha ya Hawa, siku Hawa amekaa na Mama yake na mwanae wakijua Mwarabu ameshatukimbia, wakasikia ngoma zinapigwa, ah wakajua ni midundiko kama sio harusi,

mara wanskia inaingia nyumbani kwao, kulikoni wanamwona Mwarabu na wazee wengi wengi wanakuja kwenye nyumba yao, Hawa hakuamini, kaletewa Posa mama, alishtuka alikuwa amembeba mtoto akazimia kama sio mama yake kumdaka mtoto angemuumiza sana

kuja kuzinduka wazee walishaongea mudaaa, Mwarabu akawa anampepea na mkeka wa kusuka kwa ukili umeandikwa karibu mgeni tule, doh kweli wahenga!

Hawa: vepe imekuwaje , anamshangaa Mwarabu mbona uko hapa wakati ulinikimbia

Mwarabu akamweleza kila kitu mara mama hawa akaingia anacheka cheka mweyewe akamweleza kweli aliyoeleza Mwarabu ni kweli amka ukawasalimie wakwe zako wanataka kukuona

Hawa akatambulishwa kwa wakwe zake, anashangaa imekuwaj, wakwe wanasema baada ya siku 2 tunakuja kuoza maana sisi si wakazi wa hapa tunasubiri wajomba na mashangazi wanaingia kesho

Hawa anatoa macho heeee!

kweli baada ya siku mbili Hawa akaozwaaa lakini majibu hakuyajua na rafiki yake Maija hakumwona tena yangu wamalize shule maana alienda Mwanza Misungwi kumsalimia shangazi yake ambae alihitaji msaada wake kwenye kilimo!

Sherehe ilikuwa kubwa sana pale Kariakoo, si unajua waarabu wale walikuwa waarabu wenye pesa, kuja kuoa dada wa kiswahili dada wa kizaramo ilikuwa muujiza sana kwa Hawa na mama yake, Harusi ilipendeza sana watu walikula na kunywa kama sherehe ya nini sijui alafu ndio miaka ile ambayo michele haipatikani, soda shida, ila chibuku ilikuwepo, ndisi zilikuwepo, makande yalikuwepo sherehe nzuri nakwambia hata Pilau la nyama ya kuku na ng'ombe vilikuwepo!

Miziki ya kufa mtu ya akina King Kikiii!



Walipokuwa Honey Moon Zanzibar Mwarabu ndio anamtolea matokeo yake kuwa amefaulu kwa alama ya div 1.8, kwenye somo la kiingereza tu ndio alianguka kidogo lakini angekuwa amepata div 1.7

alifurahi Hawa hakuamini, kwake ilikuwa muujiza

Baada ya Honey Moon Hawa na Mwarabu wakahamia kwenye nyumba ya Mwarabu magorofani Kariakoo pamoja na mtoto wao Omar ambae alikuwa na jina la utani Dimples!

Chuma cha Moto kilizaaga naniliihiii Kilimzaa Bwana Omar Dimples, miaka ya 80 mpaka 83

uuuuuwiiiiiiiii!

KWA MWENDELEZO BONYEZA HAPA KARIAKOO... - .

 
bro povu vepe?!
hivi business zangu zinakuhusugu nini?
hunijui sikujui we soma ukimaliza kalale kimya kimya!
kuna nafasi tele hata wewe kuandika nyama zako huku na samaki...niache na maharage yangu!
we vepee pambana na hali yako achana na yangu!
Naona hakujui mpe link huyo
 
Back
Top Bottom