Story behind your date of birth

Mkuu C6 weka hizo ( genetic material DNA) Mimi nipo Blood Group 0+ niambie maelezo yangu kwa kirefu

dna zinabeba taarifa muhimu kuhusu wewe, mfano rangi ya ngozi, urefu, unene, nywele, ndo maana utasikia uyu mtoto kafanana na baba yake,

au magonjwa ya kurithi uwa taarifa zipo kwenye dna, mfano kama wewe una matatizo ya macho, si ajabu mtoto wako akivaa miwani pia. ndo maana watu uwa wanakataa watoto au kuwa na wasiwasi maana anagundua hakuna cha kufanana nae. Labda unishawishi uhusiano kati ya siku na tabia zako, au blood group na tabia, kila binadamu ni unique, hakuna tabia general, mazingira, na vinasaba vinahusika sana
 
Last edited by a moderator:
Nakuaminia mkuu, MziziMkavu hauchimbwi dawa. sikuwezi. Tarehe na mwezi ni 5/11, nipe mautabiri yangu, mkuu
Mkuu georgeallen Nyota yako ni ya nge Haya tena soma hapo chini Tabia yako na maisha yako yote kwa ujumla.
scorpio.png


NYOTA YA NG'E (SCORPIO)

  • Hii ni nyota ya 8 katika mlolongo wa nyota 12.
  • Wenye nyota hii ni wale waliozaliwa kati ya tarehe 23 October na 21 Novemba ya mwaka wowote.
  • Sayari yao ni MARS (MARIIKH).
  • Siku yao ya Bahati ni Jumanne.
  • Namba yao ya bahati ni 9.
  • Rangi ya bahati ni Nyekundu isiyoiva au Maroon.
  • Asili yao ni MAJI.

KIPAJI CHA NG'E (MYSTICAL)


Wenye nyota hii wana kipaji na uwezo wa kiroho wa kuwasiliana na watu katika kutekeleza mambo wanayohitaji.


TABIA ZA NG'E


Wenye nyota ya Nge wana uwezo mkubwa wa uvuto au kuvutia watu katika mambo yao. Ni watu wenye uelewa mkubwa na ni majasiri katika kukabiliana na matatizo ambayo wengine yamewashinda.


Ni wenye tabia ya kutilia mkazo mambo yao, tena kwa ukali na ikibidi kutumia ukatili ili jambo litimie wao wako tayari.

Ni watu wenye tabia ya siri na wanapenda kufanya mambo yao kwa siri sana.Wenye nyota hii kama ilivyo alama yao hawaogopi kiza. Wana uwezo na kipaji cha asili cha kutekeleza mambo yao na wakafanikiwa.
Ni watu wenye akili nyingi, waerevu na wepesi sana kuelewa mambo.
Watu wa Nge vile vile wana tabia au wanaweza kujidhuru wao wenyewe.Mambo yanapowawia magumu.

TABIA YA NG'E KATIKA MAPENZI


Watu wenye nyota ya Nge wanapenda sana kutumia fursa ya kufanya mapenzi kama njia mojawapo ya kuonyesha ujasiri wao katika mapenzi na namna wanavyojua kufanya tendo la ndoa.

Kwao mapenzi au tendo la ndoa ni kiungo muhimu sana katika maisha yao hasa ikizingatiwa kwamba nyota ya Nge inatawala sehemu za siri.Inashauriwa wale wenye moyo mdogo wasifanye mapenzi na Nge sivyo watajuta. Kitu kingine ni kwamba ni watu ambao hawayumbi na hawakubali kushindwa upesi.
Ni watu wenye ashki na hasira wakiwa wamedhalilishwa au wameumizwa na wapenzi wao na wanapofanya tendo la ndoa hasira zao huisha mara moja.
Ni watu wasiri sana katika masuala ya mapenzi na wanakuwa hivyo ili waweze kuwapata wapenzi wengi kukidhi matakwa au kiu yao kubwa ya ngono.
{mospagebreak}

TABIA YA NG'E KATIKA FEDHA


Hakuna kitu kinachoshindikana kwa wenye nyota hii, na chepesi zaidi ni namna ya kupata fedha. Wana uzoefu mkubwa wa kuhimili matatizo ya kifedha wanapoanguka, hata wakiwa matajiri na wakafilisika.


Watu wa Nge wana bahati ya kuvumbua fedha au utajiri katika njia ambazo watu wengine si rahisi kugundua.

Ni watu ambao sio rahisi kudanganyika wakiona mpango wowote wa kifedha. Mara nyingi ni kawaida yao kuchukua kitu au kufanya mradi ambao wengine wanauona wa kipuuzi na wakaugeuza kuwa wa thamani kubwa.
Ni wakarimu sana wanapokuwa na fedha, na hawapendi kujidai kwa utajiri wao. Wako tayari wakati wowote kuwatumia watu wengine kutekeleza malengo yao.
Kwa ujumla wao ni wataalamu wa kutafuta fedha katika njia ambazo watu wengi hawazifahamu.

MAVAZI YA NG'E


Wenye nyota ya Nge wanatakiwa wavae nguo zenye rangi inayong'ara, zenye kuonekana na maridadi,zilizo katika hali ya suti au mbili kwa pamoja.

Nguo ziwe za rangi nyekundu au shati jekundu au skafu nyekundu. Kitambaa kiwe cha sufi au cha fulana au chenye kumeremeta.
Mavazi yaendane na kofia na wanawake wapendelee sana kuvaa suruali.

MATATIZO YA KIAFYA


Nyota hii inatawala kifuko cha mkojo, uume, uke, kifandugu au kitonoko (coccy), mlango wa kizazi(cervix) na sehemu ya haja kubwa. Vile vile inatawala mfumo wa mkojo na tezi kibofu (prostate).


Matatizo yao makubwa ya kiafya yanatokana na sehemu zilizotajwa ambazo zinatawaliwa na nyota yao wenye nyota hii wanapenda kujizoesha sana mambo ya mapenzi na ngono. Wakati mwingine hisia zao zinakuwa kubwa sana kiasi kwamba wao wenyewe wanajishuku vibaya.

Inapotokea hivi wanahitajika kusafisha miili yao kwa fadhaa iliyowajaa kutokana na mfadhaiko wa hisia zao.
Kwa ujumla ni watu wenye afya nzuri na wanapona haraka maradhi yanayowasumbua. Wenye nyota hii wana tabia ya aidha kula, kunywa au kuvuta kupita kiasi au wengine hawafanyi mambo hayo kabisa.

Kwa vile nyota hii inatawala sehemu zinazoondoa uchafu wa mwili ni vizuri watu wa Nge wakawa waangalifu na mambo yanayochafua mwili wao.

Magonjwa makubwa ya wenye nyota ya Nge ni maradhi yanayohusiana na kibofu cha mkojo, maradhi ya kuziba mkojo, kansa ya tezi kibofu (prostate Cancer), matatizo ya damu ya kike na mabusha.
{mospagebreak}

KAZI ZA WENYE NYOTA YA NG'E.


Nyota ya Nge ambayo alama yake ya asili ni Maji ni nyota mojawapo ya nyota zenye nguvu katika mambo ya kikazi.

Ni watu wenye milipuko ya hisia wanapokuwa katika miradi yao ya kazi. Wanafanya shughuli zao kwa hisia kali na hamaki na wanategemea wapate majibu ya kuridhisha.
Ni watu makini sana katika kazi na wanafanya kazi kwa kutilia mkazo na ushupavu wakihakikisha wanatekeleza malengo yao. Ni watu waerevu na wenye kung'amua mambo upesi. Ni wafanyakazi wazuri na wanaheshima kwa wafanyakazi wenzao.
Kazi zinazowafaa wenye nyota hii ni kazi za madawa au tiba, kazi za upelelezi, kazi za utafiti, kazi za fundi bomba, kazi za elimu ya kale, na kazi za ushauri wa mambo ya mapenzi na ngono.

FAMILIA ZA NG'E


Wazazi wenye nyota ya Nge ni watu ambao wanaonyesha utulivu wa hali ya juu. Kimaumbile huwa hawaonyeshi hisia walizokuwa nazo juu ya watoto wao, wanaweza wakawa na chuki kubwa lakini hawapendi kuiionyesha.


Kwa ujumla wazazi hao wanapenda watoto na wanatumia muda mwingi na hisia zao kuwangalia na kuwadhibiti watoto wao.

Pamoja na ukarimu wao ni wazazi wenye kupenda nidhamu na wanataka watoto wao wafuate maadili mema. Wazazi hao walivyokuwa wadogo wamepitia ujanja wote hivyo hawakubali watoto wao wawadanganye.

Watoto watagundua kwamba wazazi wao ni watu wa kutisha na kuogopwa lakini uhusiano wao unakuwa ni mzuri. Wazazi wa kike wanakuwa na hisia kali kwa watoto wao kitendo ambacho kinawafanya watoto wawe katika shinikizo.


MADINI YA NG'E

Wenye nyota hii wanatakiwa wavae vito vinavyoitwa BERYL NA RED CORNELIUS. Mawe haya yenye rangi ya damu ya mzee (Maroon) na rangi Nyekundu yanaakisi au kuashiria asili ya Nge ya uhusiano wake wa asili na kitu chochote cha miujiza na uchawi.

UHUSIANO WA KIMAPENZI


(NG'E, NG'OMBE)

Tabia ya Nge ya wasiwasi, wivu, hisia kali za kimapenzi na dhana mbaya kwa wapenzi wao hutulizwa na kuzimwa na nyota ya Ng'ombe ambao wana tabia ya utulivu, uaminifu, wasioyumba na wanaopenda kusikiliza wanayoambiwa.

VYAKULA VYA NG'E

Wenye nyota hii wanashauriwa wale vyakula au matunda yafuatayo ambayo yanatawaliwa na nyota yao, Mananasi, wapende sana vitunguu vibichi na vilivyopikwa, Nyama ya Kondoo mchanga na vyakula viambatane na viungo vikali.

NCHI ZA NG'E

Ili kupata mafanikio ya kinyota kwa wale wenye uwezo wanashauriwa aidha kuishi au kutembelea nchi au miji ifuatayo ambayo inatawaliwa na nyota hii.
Miji hiyo ni Liverpool(Uingereza) na New Orleans(Marekani) na nchi za Poland na Switzerland.

RANGI YA NGE

Wenye nyota hii wanashauriwa wapake nyumba zao au vyumba vyao au magari yao au sehemu zao za biashara rangi nzito yenye kutia shauku na kuvutia kama rangi ya damu ya mzee (Maroon).
 
Ngoja nipitie kwanza nitarudi baadaye maana ni interesting na inahitaji itendewe haki kwa kusomwa kiufasaha.
 
NUMBER 1

You are smart, straight talking, funny, stubborn, hardworking, honest,Jealous on competing basis, kind hearted, angry, friendly, authorities,Famous

person...always want to be and regarded as first on people position, they are often like to be independent, will never be under others, self confident

people!
You are most likely to fall in love in the younger age, but will get marry when you mature! You are likely to have problems with people who have opposite

views
And you are most likely to take revenge over your enemies in a long time basis. You are a spender, but you will have a good profession in the future.

If you are guy you will be very popular that everybody will have mental attraction and respect at you. You can go anywhere from the local shop to the

heart of the parliament because you are positive and well talented in numerous issues!! But in your life you will always have some people who will work

hard to bring you & your name down. This is undercover!! Coz of your smart behavior you will be hated by some people too...

Your family life is very cool, you will have a very nice partner & wonderful children... You are pioneer, independent & original...

Your best match is 4,6,8 good match is 3,5,7 !!!


Hebu mnaonifahamu mje hapa mseme kama haya ni kweli au vipi... The Priest, Asnam, Kipipi, @gfsonwin, mimisa, cacico, snowhite, @asprin, Paloma, shem sosoliso, Arushaone, Baba V, snochet, @invisible et al..pliz kam zis way...

 
Last edited by a moderator:
mhhhh...........haya mambo mara nyingine sio kweli kumbe! mbona mie siko as my number says?!?!?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom