Stories behind popular songs

crankshaft

JF-Expert Member
Jun 12, 2019
1,411
3,384
Song: i took a pill in ibiza by mike posner


Huyu jamaa alikwenda huko ibiza na rafiki yake anayeitwa avicii ambaye alikuwa ni maarufu wakati huo.

Walipofika akashangaa kuona watu hawana shobo naye kabisa yaani hawamjui bali wanamshangilia yule rafiki yake avicii akiwa anaperform mbele.

Jamaa akabaki amesimama kwa stress sana nyuma ya umati uliokuwa unamshangilia rafiki yake.

Ghafla akatokea mtu akampa kidonge (pill) kwa stress alizokuwa nazo ilibidi ameze fasta.

Hapo ndipo alipopata idea ya kutunga wimbo na jina lake, i took a pill in ibiza.

Toleo la kwanza halikuwa maarufu sana ila ilikuja kuwa hitsong baada ya kuja kufanya remix na rafiki yake yule, avicii.

Mpaka sasa una zaidi ya view 1.5b huko youtube na ndio wimbo wake maarufu zaidi.
 
Timu ya the chainsmokers ilimfuata rihanna ili aimbe kwenye wimbo wao wa don't let me down lakini timu ya rihanna wakakataa kwa kudai kuwa wimbo ni wa kiwango kidogo. Kwa wanaowajua hawa jamaa huwa wanatengeneza beat halafu wanatafuta wasanii waimbe kama dj khaled.

Basi Ikabidi watafute mtu mwingine. Ndipo wakampata huyu binti mdogo daya ambaye hakuwa na umaarufu wowote. Kilichofuata ni historia, wimbo umekuwa miongoni mwa most popular in the world ukiwa na zaidi ya 1.5b views huko youtube.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom