Steven Wassira vs Ester Bulaya wazozana bungeni | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Steven Wassira vs Ester Bulaya wazozana bungeni

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mkurabitambo, Jun 20, 2012.

 1. M

  Mkurabitambo JF-Expert Member

  #1
  Jun 20, 2012
  Joined: Feb 3, 2010
  Messages: 229
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Sakata hilo lilitokea nje
  ya ukumbi wa Bunge
  mara baada ya
  kuahirishwa kwa kikao
  juzi usiku, ambapo
  Wassira alimfuata
  Bulaya na kumhoji
  kwamba kwanini alitoa
  maneno ya kuipinga
  bajeti ya Serikali.
  Wassira ambaye pia ni
  Mbunge wa Bunda
  (CCM)
  Alimwambia Bulaya:
  “Mimi ndiye Mbunge
  wa Bunda, wewe huwezi
  kujifanya ndiye
  uliyetumwa na
  wananchi kuja kusema
  maneno ya uwongo
  hapa, eti unaipinga
  bajeti ya Serikali, ni
  nani aliyekutuma?”
  Waziri huyo alikwenda
  mbali na kumwambia
  mbunge huyo kijana
  kwamba, “wewe
  tunakufahamu una
  pande mbili (upinzani
  na CCM) na kila siku
  unashirikiana na Halima
  Mdee (Kawe-Chadema),
  tunakujua kwamba uko
  CCM na Chadema.”
  Kutokana na kauli hizo,
  Bulaya alijibu mapigo
  akimwambia Wassira
  kwamba yeye akiwa
  mbunge wa CCM ana
  wajibu wa kukikosoa
  chama chake na
  hakuwa mtu wa kwanza
  kukataa kuunga mkono
  bajeti hadi hapo
  marekebisho
  yatakapokuwa
  yamefanywa.
  “Mimi nina haki ya
  kuzungumza ndani ya
  Bunge na kusema kile
  ninachokiamini kama
  mbunge, wala hakuna
  mtu wa kuniwekea
  mipaka. Halafu kama ni
  uhusiano na wabunge
  wengine mbona
  wabunge wengi tu wa
  CCM wanashirikiana na
  upinzani?” alihoji
  Bulaya.
  Source mwananchi
   
 2. BONGOLALA

  BONGOLALA JF-Expert Member

  #2
  Jun 20, 2012
  Joined: Sep 14, 2009
  Messages: 13,788
  Likes Received: 2,398
  Trophy Points: 280
  Wassira yapaswa ujue kuwa, business as usual hakuna siku hizi!
   
 3. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #3
  Jun 20, 2012
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Hahahaha sipati picha alivyo kasirika Tyson angerusha ngumi
   
 4. M

  Mkurabitambo JF-Expert Member

  #4
  Jun 20, 2012
  Joined: Feb 3, 2010
  Messages: 229
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  najiuliza mzee wa miaka 70 atazozanaje na kijana wa miaka 32?
   
 5. F

  Froida JF-Expert Member

  #5
  Jun 20, 2012
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 7,900
  Likes Received: 1,328
  Trophy Points: 280
  babu visa kabinti kazi kweli kweli anamiliki jimbo kwa maana yake
   
 6. M

  Mkurabitambo JF-Expert Member

  #6
  Jun 20, 2012
  Joined: Feb 3, 2010
  Messages: 229
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  najiuliza mzee wa miaka 70 atazozanaje na kijana wa miaka 32?
  Mzee tyson pumzika
   
 7. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #7
  Jun 20, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  hahahahaaa,,,,wassira mzee wangu duh
   
 8. toghocho

  toghocho JF-Expert Member

  #8
  Jun 20, 2012
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 1,177
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  anaogopa kitu kinaweza kuingia cdm kikamng'oa, anataka wote wawe mazoba wananchi wakose..choice
   
Loading...