GE2025 Stephen Wasira: Ni utamaduni wa CCM kumwongezea muda Rais anayefanya vizuri

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Just Pray

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
2,142
Reaction score
4,779
Makamu Mwenyekiti wa Chama Chama Mapinduzi (CCM) Bara, Mzee Stephen Wasira amesema, vyama vingi vya siasa ulimwenguni vina utamaduni wa kuwaongezea muda viongozi ambao wanafanya vizuri kwenye uongozi wao kwa maana ya kutowapinga ndani ya chama wanapogombea kipindi kingine cha uongozi.

Amesema ni katika muktadha huo, CCM imempa tena nafasi Rais Samia Suluhu Hassan ambaye amefanya mambo makubwa kwa Taifa kupitia miradi mbalimbali.

Akizungumza katika kipindi cha Mizani kinachorushwa na Shirika la Utangazaji Tanzania kupitia chaneli ya TBC1 na kuongozwa na Mkurugenzi Mkuu wa TBC, Dkt. Ayub Rioba Chacha, Mzee wa Wasira amefafanua kwa awamu inamhusu mtu na si miaka na kwamba hii ni Awamu ya Sita ambayo mpaka sasa imeongozwa kwa miaka takribani minne na Rais Samia na kwamba Awamu ya Tano ilimalizika kufuatia kifo cha Rais John Magufuli.

Kuhusu kazi nzuri aliyoifanya Rais Samia, Mzee Wasira ametaja baadhi ya kazi hizo kuwa ni miradi mkubwa iliyotekelezwa katika kipindi cha uongozi wake kama ujenzi wa reli ya kisasa (SGR), bwawa la kuzalisha umeme la Julius Nyerere, ujenzi wa madarasa, upelekaji maji kwa wananchi na miradi mingine lukuki yenye faida kwa jamii.


Your browser is not able to display this video.
 
takataka hii ilitakiwa kuwa kijijini kuomba msamahaa pindi umauti ukimfikia
 
Huyu mzee, mwaka 1974 marehemu baba yangu yuko darasa la 4! Yeye ni MKUU WA MKOA WA MARA KWA WAKATI HUO!

Leo mimi niliekuwa sijafikiriwa hata kidogo kuletwa duniani... mtoto nina watoto, mmoja amemaliza kidato cha 4...yeye bado yuko kwenye system!

Hivi Ccm hakuna watu wenye akili?!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…