Stendi mpya ya mabasi Dodoma mbioni kukamilika

Stendi mpya ya mabasi Dodoma mbioni kukamilika

mamayoyo1

JF-Expert Member
Joined
Jul 25, 2018
Posts
1,011
Reaction score
1,019
1548730824510.png

Kituo cha kisasa cha mabasi jijini Dodoma kitakuwa kimekamilika ifikapo mwishoni mwa mwaka huu, imeelezwa.

Hayo yalielezwa juzi na Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Mohammedi Builders, Tahir Mustapha alipozungumza na waandishi wa habari.

Kampuni hiyo ndiyo inajenga soko la kisasa na kituo hicho cha kisasa eneo la Nzuguni jijini hapa.

Mkurugenzi huyo alisema mradi wa ujenzi wa stendi unaendelea vizuri na mpaka ifikapo mwisho wa mwaka huu utakuwa umekamilika.

Alisema kampuni yao ni ya kizalendo na wanamshukuru Rais kwa kutoa maelekezo makampuni ya wazawa yapewe nafasi katika miradi mikubwa.

Mkurugenzi huyo aliahidi kuitekeleza miradi yote kwa wakati kutomuangusha Rais Dk. Magufuli.
 
Pesa za mkopo hizo world bank msije sema pesa zetu wenyewe
KWANI HAPO YANAFANYIKA MAENDELEO YA AKINA NAN?....TUJITAHIDI TUUNGE MKONO JUHUDI ZA KIMAENDELEO ...KUMBUKA AWAMU YA TANO INAFANYA MAMBO YANAYOONEKANA KWA FAIDA YA WANANCHI
 
KWANI HAPO YANAFANYIKA MAENDELEO YA AKINA NAN?....TUJITAHIDI TUUNGE MKONO JUHUDI ZA KIMAENDELEO ...KUMBUKA AWAMU YA TANO INAFANYA MAMBO YANAYOONEKANA KWA FAIDA YA WANANCHI
Kuunga mkono Juhudi ni kuhama chama ulichopo, kujivua Ubunge na nyadhifa zote ulizonazo kisha kuhamia Chama Twawala na kupewa nafasi ingine ya kugombea huku "Tume" ikitakiwa kukupitisha by any means.
 
afu stand yenyewe iko mbaliiiiiiiiii na mji# ABC for life mpaka area c inakuleta........and first choice adi wajenzi na kmbinyiko at least
 
Back
Top Bottom