Stellenbosch ni hatari zaidi wakiwa ugenini

Stellenbosch ni hatari zaidi wakiwa ugenini

Story na nadharia zitakuwa nyingi sana kuelekea huo mchezo, ila atakayekuwa na mchezo mzuri kwa maana ya kutumia nafasi zitakazopatikana kwenye huo mchezo atakuwa na nafasi nzuri zaidi ya kufuzu
 
Nasikitika mno huu mchezo kupelekwa Zanzibar

INANIUMA SANA.
HII SELIKALI NIMEMUACHIA MUNGU.
Unasikitika vipi wakati uwanja mnauharibu wenyewe kwa kufukia mbuzi?

Wale wazee wenu wameshinda siku 4 pale kwa Mkapa wanamlilia meneja awaruhusu kuingia uwanjani, unategemea kutakuwa na kiwanja hapo, mbona uwanja wa Azam hauribiki.

Jengeni uwanja wenu muwe mnafanya mnavyotaka hata mkitaka kumzika Mwamedi hakuna atakayewaingilia.
 
Hawa Stellenbosch ambao ni wapinzani wa Simba katika hatua ya nusu fainali ya CAFCC inaonyesha ni timu inayojua sana kucheza kimkakati wakiwa ugenini. Ni kama ina zile sifa kama za Al Hilal ya Ibenge, wanakuacha ucheze ila wakishakupiga kimoja hauchomoi ng'o.

Hizi ni rekodi za msimu huu za mechi walizoshinda wakiwa ugenini katika mashindano mbalimbali.

17/08/24 - Nsingizini 0-3 (CAFCC)
28/08/24 - Mamelodi 0-1
18/10/24 - AmaZulu 1-2
23/10/24 - Chipa Utd 0-2
01/12/24 - Orlando 0-1
15/12/24 - Lunda Sul 0-1 (CAFCC)
23/01/25 - AmaZulu 0-5
18/02/25 - TS Galaxy 2-3
04/05/25 - Gallants 0-1
16/05/25 - Sekhukhune 1-2
09/04/25 - Zamalek 0-1 (CAFCC)

Ili Simba iwe kwenye nafasi nzuri ya kumtoa Stellenbosch inabidi iwe na matumizi mazuri sana ya nafasi. Kwa uwepo wa Mpanzu, sina wasiwasi na utengenezaji wa nafasi, shida inakuja zitatumika vizuri?

Pia wanaweza kusuka mpango maalum wa kumkaba Mpanzu, je kina Kibu, Ahoua, Mukwala na Ateba wanaweza kujiongeza?

Hawa Stellenbosch hawako vizuri sana wakiwa nyumbani kwao. Bado hawajajenga ile "mentality" ya "nyumbani kwao hatoki mtu". Simba ikipata ushindi hata wa 2-0 kule Zanzibar basi ina nafasi kubwa ya kuvuka kwenda fainali.
Kwenye mechi za away kwenye confederation wameshinda mbili na wamepasuka 2
Wameshinda 1-0 vs Lunda na 1-0 vs zamalek
Wamepasuka mechi 2, wamefungwa 5-0 vs berkane na 2-0 vs stade malien
Kiufupi ni team ya kawaida isiyotabirika yaani ukiikamatia chini unaipiga 2+ila ikikukamatia chini inakufunga 1-0 naongelea matokeo ya confederation sio spl.Naunga mkono hoja Simba akipata matokeo ya 2-0 nyumbani anavuka .
 
Back
Top Bottom