Status za WhatsApp zinatuonesha jinsi tulivyo na tunajichora tu kwa wengine

Mambo yaliyonishinda kwenye kutumia simu;
1. Kuweka picha yangu kama wallpaper ya simu
2. Kuweka status za kupost Birthday za watu
3. Kupiga picha kweny sherehe au sehemu za starehe
4. Kupiga picha za vikundi kama wachezaji wa mpira haswa kweny event za kiofisi siwezi kabisa.

Kwenye PC yangu;
1. Kuweka picha kama wallpaper ya PC
 
Mm Huwa naweka clips za vichekesho tu tena ni moja tu haizidi mb 2 na ni mara 2 jumamosi na jumapili tu, Huwa nashangaa unakuta mtu kaweka status hazipungui 5 tena zote ni video alafu ni za ajabu mpaka unashangaa.

Kuna jamaa mmoja ni Dr nilikuwa namuheshimu sana siku Simba amekula 5 kutoka kwa Yanga kaweka status picha ya kuku mwekundu anapandwa na jogoo wa njano, nikamdharau Toka siku hiyo maana binafsi kabla sijapost status Huwa naangalia mfano hii video akaiona Mzee wangu, aunt yangu au mtu yyte ninayeheshimiana nae atanichukukiaje.
 
Status zangu hata ujifanye kauzu vipi.. ukishaview tu mara mbili au tatu inakuwa ni ulevi.. lazima ukifinguq whatsapp yako utakimbilia kuona nimeweka nini siku ya leo..

Kitu ambacho siwezi kuweka Status ni MAISHA yangu Binafsi pia hata picha zangu etc huwa hazionekan huko..

Kingine, kati ya contacts zangu 89 nimeruhusu watu 25 tu waone nachoweka huko.
 
Back
Top Bottom