Starting a Business in Tanzania

You can find the procedures are very clear but when it comes to going through them, officials tend to complicate very much the processess!

kweli kabisa...kuna hongo kibao za kutolewa BRELA to speed things up..ushauri wangu ni kwamba muachie mwanasheria hakufanyie kazi hii usisubutu kufanya mwenyewe...nilipokuwa trainee kwenye firm moja hapo dar nilijionea mengi sana brela..mambo ya kumjua mtu kwa sana tuu...na ina saidia kwenye kufanya kazi kwa haraka

kama uamini jaribu kufanya hii process mwenyewe!!
 
naomba kujulisha mambo ya msingi ya kuzingatia kabla ya kufungua kampuni( private)
 
Hujaeleweka vizuri ni nini hasa unataka hivyo sijui kama ntakuwa nimekusaidia. Kama ulimaanisha document na taratibu unazotakiwa kuzifuata kwa ajiri ya kufungua kampuni ipo hivi:

1. Tambua unataka kufanya biashara gani.
2. Je kampuni yako unataka iwe limited au partnership.
3. Pendekeza jina la kampuni yako.
4. Baada ya kuwa na majibu hapo juu. Andika barua Kwa msajili wa makampuni kucheki kama jina ulilopenekeza kuna mtu mwingine analitumia.
5.Normally inachukua 2days jina kutoka, kama hakuna anaetumia jina hilo utapewa go ahead kulitumia jina hilo.
6. Kama jibu la No. 2 hapo juu lilikuwa ni limited Company, andaa memorandum and Articles of Association 'MEMART' ya kampuni yako. Hii inaweza fanywa na Mwanasheria au mtu yeyote mwenye uzoefu but inabidi ipate baraka za Lawyer at the end.
7. Peleka MEMART kwa msajili wa kampuni kwa ajiri ya kusajiri kampuni yako.
8. Kampuni yako ikishasajiriwa utapewa Certicficate of Incorporation. Kimsingi hapa utakuwa tayari unakampuni inayotambulika kisheria but huwezi kufanya biashara yoyote.
9. Ili uweze kufanya biashara utatakiwa ukate leseni ya biashara sanjari na kufungua bank account ya kampuni. Hapa utatakiwa kuwa na physical address ya kampuni '' Office ya kampuni''.
10. Mambo haya yakiwa yamekamilika ruksa kufanya biashara kihalali.

Sijui kama nimekusaidia.

cheers
 
Mkuu BM21, hapo hata mimi umenisaidia ila ningeomba nikusumbue kido iwapo unaweza kwa lugha rahisi kabisa ukanifafanulia kampuni yangu ikiwa Limited inakuwaje na ikiwa Partinership inakuwaje...Natanguliza shukurani.
 
Ndiyo Babadesi,

Kwa lugha nyepesi limited Kampani ni ile ambayo ikitokea kwa sababu mbalimbali inatakiwa kufirisiwa labda kwa kushindwa kulipa madeni mbalimbali mfano mikopo ya bank au madai toka kwa wateja wake basi malizitakazo filisiwa ni zile za kampuni tu na si za mtu binafsi mfano wakurugenzi wa kampuni. tofauti na partnership especially unlimited partnership (maana kunalimited partnership vilevile) ikitokea kampuni inafirisiwa basi kama mali za kampuni hazitoshi kulipa madeni yakampuni basi itabidi maali za wakurugenzi wa kampuni pia zichukuliwe kulipa hayo madeni.

Lakini kwa ulimwengu wa sasa kuna faida nyingi za kuwa na limited Company kuliko unlimited Company. Mfano ni rahisi kupata mkopo wa bank ukiwa na limited company kuliko unlimited or partnership, pili hata kupata tender watu wengi hawapendi kudeal na unlimited company sababu kubwa hapa ni kitu kinachoitwa 'going concern'. Ukiendesha biashara kama mtu binafsi au unlimited company mkurugenzi akifa na kampuni imekufa hata ikiendelea ni ngumu sana kushughurikia matatizo ya kampuni yaliyosababisha na mkurugenzi aliefariki lakini Limited company huwa haifi kwa kufiwa na mkurugenzi kufa kwake ni kuandika barua kwa msajiri kuomba kufunga kampuni.

cheers
Bm21
 
Hujaeleweka vizuri ni nini hasa unataka hivyo sijui kama ntakuwa nimekusaidia. Kama ulimaanisha document na taratibu unazotakiwa kuzifuata kwa ajiri ya kufungua kampuni ipo hivi:

1. Tambua unataka kufanya biashara gani.
2. Je kampuni yako unataka iwe limited au partnership.
3. Pendekeza jina la kampuni yako.
4. Baada ya kuwa na majibu hapo juu. Andika barua Kwa msajili wa makampuni kucheki kama jina ulilopenekeza kuna mtu mwingine analitumia.
5.Normally inachukua 2days jina kutoka, kama hakuna anaetumia jina hilo utapewa go ahead kulitumia jina hilo.
6. Kama jibu la No. 2 hapo juu lilikuwa ni limited Company, andaa memorandum and Articles of Association 'MEMART' ya kampuni yako. Hii inaweza fanywa na Mwanasheria au mtu yeyote mwenye uzoefu but inabidi ipate baraka za Lawyer at the end.
7. Peleka MEMART kwa msajili wa kampuni kwa ajiri ya kusajiri kampuni yako.
8. Kampuni yako ikishasajiriwa utapewa Certicficate of Incorporation. Kimsingi hapa utakuwa tayari unakampuni inayotambulika kisheria but huwezi kufanya biashara yoyote.
9. Ili uweze kufanya biashara utatakiwa ukate leseni ya biashara sanjari na kufungua bank account ya kampuni. Hapa utatakiwa kuwa na physical address ya kampuni '' Office ya kampuni''.
10. Mambo haya yakiwa yamekamilika ruksa kufanya biashara kihalali.

Sijui kama nimekusaidia.

cheers
Mkuu maelezo hapo juu yamejitosheleza.Ila kwa siku hizi kila mfanya biashara/kampuni lazima awe na Tax Identification Number (TIN). Hiyo inatakiwa kwenye Leseni na pia kwenye kufungua Bank Account. Kwa hiyo baada ya kupata Certificate of incorporation lazima aende TRA kujiandikisha ili kupata TIN. Vitu vinavyohitajika hapo ni hivyo vilivyotajwa kwenye (9) hapo juu
 
Mkuu BM21, hapo hata mimi umenisaidia ila ningeomba nikusumbue kido iwapo unaweza kwa lugha rahisi kabisa ukanifafanulia kampuni yangu ikiwa Limited inakuwaje na ikiwa Partinership inakuwaje...Natanguliza shukurani.

Mkuu BabaDesi,

Kwa lugha nyepesi Limited company ni ile ambayo ikitokea kwa sababu mbalimbali mfano kushindwa kulipa mikopo ya benk au wateja wake ikatakiwa kufirisiwa basi maali zitakazo filisiwa ni zile za kampuni tu pasipo kugusa maali za wakurugenzi wa kampuni. Lakini kwa partnership company especially unlimited (maana kuna limited partnership vilevile) kama kampuni inafilisiwa basi kama mali za kamapuni hazitoshi kulipa madeni ya kampuni maali za wakurugenzi wa kampuni pia zitachukuliwa ili kulipa madeni ya kampuni.

Hata hivyo kuna faida kubwa kufungua limited comapny ikiwemo urahisi wa kupata mikopo katika mabank na pia urahisi wa kupata kazi 'tender' tofauti na unlimited company. Kimsing tunasema unlimited company haina princile ya 'going concern' i.e. mkurugenzi wa kampuni akifa inawezekana na kampuni ukawa ndio mwisho wake/ikafa. Wakati limited company haiweze kufa kw akifo cha mkurugenzi kwani yenyewe inasimana kama mtu 'legal person' ndio maana kama kampuni kampuni inashitakiwa basi itashitakiwa kwa jina lake na si kwa jina la wakurugenzi.

Nadhani itasaidia kidogo
 
Ndugu wazalendo na wajasiriamali,

Kwasasa namiliki ekari 20 za ardhi huko kongowe kibaha mkoa wa Pwani, niko kwenye process za mwisho kupata hati miliki.suala lipo wizara ya ardhi kwasasa.

Shida kubwa nahitaji ushauri wa kibiashara na jinsi ya kupata capital ya hiyo biashara nitakayofanya kwenye ardhi hiyo.

Pia hata kama kuna mdau wowote anataka kuingia ubia basi namkaribisha.

natanguliza shukrani zangu za dhati.

you may contact me via the following mobile number,

+255 787 403865

+255 755 403865
 
Mkubwa hongera kwa utafuta ushauri wa kibiashara hapa JF maana ungeingia mtaani waungwana wangeweza kwambia viwanja maeneo hayo vinalipa uza. Kimsingi inatakiwa kutathmini eneo linafa kwa biashara gana hii itahusisha kufanya upembuzi yakinifu 'feasibility study' wa mradi ambao unafit eneo hilo. Nategemea kurudi Tanzania siku za usoni kama ntakikuta tutaona tufanye nini hata hivyo ntakupigia kwa numba zako hapo juu nikuuzie mawazo kidogo.
 
Ndugu yangu hapo juu nashukuru sana kwa mawazo yako, nategemea kupokea simu yako kwa mchango chanya wa mawazo.

kwa eneo lile la kibaha mwanzo niliomba hati ya shamba then nikaona niombe hati ya kiwanja baadala ya shamba lengo likiwa hapo baadaye nitakapopata capital nataka kuanzisha shule ya sekondari ya kulipia (private) kwani kwa mkoa wa pwani hitaji ili ni muhimu sana kwani sulaa la elimu kwa mkoa huo bado liko nyuma kutoka either na mila potofu zisizo faa au sababu zingine za kijamii.

wadau vipi kuhusu NSSF,PPF n taasisi zingine hawezi kuingia ubia hapo?

karibuni kwa mawazo
 
Swali langu je naulizia kama ni Limited company.

Inatakiwa kampuni iwe na watu wangapi, maana kampuni nyingi wanasema ladhima muwe zaidi ya watu 2 mpaka 50. Apo nisaidie kama nataka kampuni iwe yangu bila kushirikiana na watu
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom