Startimes yatoa ufafanuzi kuhusu kuonekana chaneli za nyumbani

Mkuu mimi binafsi baada ya copa america na nba season kuisha sijanunua kifurushi chochote na bado channels local zote nazipata. Si kweli kama watu wanavyosema kuwa kuona local tv lazima ulipie startimes.
Kwa wale wenye vingamuzi vya zamani unapata local channels hata kama hujalipia mwisho wa mwezi. Ila kwa ving'amuzi vipya vya antenna kila mwezi lazima ulipie. Bei nimenunua sh.40,000/= baada ya ofa kuisha channels zote zimekata na nikasema sinunui kifurushi cha mwezi hata siku moja kwa ajili ya local channels yaani hadi taarifa ya habari nilipie??.
 
Julai 14, 2016

UFAFANUZI KUHUSIANA NA HUDUMA ZA STARTIMES

Kampuni ya StarTimes Tanzania kupitia ving’amuzi vyake imejizatiti kuhakikisha watanzania wote wanafikiwa na huduma za matangazo ya dijitali kwa gharama nafuu ambayo kila mtu ataimudu.

StarTimes inajivunia kuwa kampuni iliyoleta mapinduzi ya matangazo ya dijitali nchini tangu kuzimwa kwa mitambo ya analogia kwa mara ya kwanza mwishoni mwa mwaka 2012 na kuifanya Tanzania kuwa mfano wa kuigwa Afrika ya Mashariki.

Hivi karibuni kumekuwa na taarifa zisizo na uhakika wala kufanyiwa utafiti wa kutosha zikisambazwa katika mitandao ya kijamii kwamba StarTimes inauza ving’amuzi na vifurushi vyake kwa gharama za juu ambazo mtanzania mwenye kipato cha chini hawezi kumudu pamoja na kuwatoza wateja wake kutazama chaneli za nyumbani.

StarTimes inapenda kutoa ufafanuzi kwamba si kweli inatoa huduma zake kwa bei ya juu kama taarifa hiyo iliyosambazwa inavyosema.

1. Kwanza kabisa, StarTimes ni kampuni pekee inayouza ving’amuzi vyake kwa gharama nafuu kabisa ambayo mtanzania yoyote anaweza kuimudu. Bei zetu zinaanzia shilingi 22,000/- kwa vile vya antenna na shilingi 86,000/- vya dishi, vyote vikiwa vimeunganishwa na ofa ya mwezi mmoja ya kifurushi cha bure kwa kila mojawapo.

2. Pili, kampuni ya StarTimes ina vifurushi vya gharama nafuu kwa malipo ya mwisho wa mwezi vikiwa na chaneli nyingi na za kuvutia za ndani na nje. Bei ya vifurushi kwa ving’amuzi vya antenna inaanzia shilingi 5000/- huku ving’amuzi vya dishi vikianzia shilingi 8000/- tu.

3. Na mwisho tungependa kutoa ufafanuzi juu ya suala la StarTimes kuwatoza watanzania ili kutazama chaneli za nyumbani. Si kweli kwamba kampuni yetu inawatoza watanzania ili kutazama chaneli za nyumbani bali huwa zinatokea hitilafu za kimtandao ambazo husababisha baadhi ya chaneli kutoonekana na kisha kushughulikiwa mara moja. Na hali hiyo huwa inajitokeza mara chache ambapo timu yetu makini ya mafundi huitaarifu uongozi ili kuweza kuwafahamisha wateja wetu wapendwa.

Mwisho, StarTimes inatoa wito kwa wateja wake na watanzania kwa ujumla kuwa makini na kuzipuuza taarifa za uzushi zisizokuwa na uhakika zinazosambazwa mitandaoni. Taarifa sahihi na za uhakika hutolewa na uongozi wa StarTimes pekee na si vinginevyo na siku zote kukiwa na habari yoyote haitosita kufanya hivyo.

Asanteni kwa kuendelea kutuunga mkono kwa kufurahia huduma na bidhaa zetu.

Lanfang Liao

Afisa Mtendaji Mkuu
Uwongo si kitu kizuri kwa kampuni Kama hii

1. Startimes siyo kampuni ya kwanza kuleta mfumo WA kidigitali Tz. Sisi nyumbani kwetu tumekuwa tukitumia digitali tokea mwaka 2000 Na tuliona channel zote za nyumbani, BBC, CNN, B4U, TVM Na nyingine Kama 70 bure kabisa tukitumia king'amuzi cha strong, naamini wengi wetu humu Ni mashahidi kwa kutumia ving'amuzi hivyo pamoja na mediacom.
Startimes Ni kampuni ya kibepari iliyoihadaa serikali kuzima mtambo wa analojia Ili waweze kufanya biashara, Na ninapenda kuwaambia waTz, kuwa bado wana uwezo wa kutumia ving'amuzi hivyo bure kabisa.

Pili, Mimi binafsi nilinunua king'amuzi cha startimes tokea nimenunua king'amuzi hichi sijawahi ona channel za nyumbani bure hata siku moja zaidi ya TBC 1, ambao ndo wakala Wao katika mpango wa kutuhadaa mpaka wakawapa eneo, sasa Ni mwaka mmoja umepita nalipia kila mwezi Na channel zao za hovyohovyo, nyingi zikiwa Ni za kichina.

Startimes wamenidhulumu kifurushi cha 5000 since march pamoja Na kukfuatilia kwa miezi 3, bila mafanikio mpaka ikafikia hatua ya dada mmoja ambaye Ni muhudumu wa startimes kuniambia eti mbona unafuatilia 5000 Tu kwa muda wote huo?, nilikasirika Sana.

Kiukweli hii kampuni Ni tatizo Na ninailaumu Sana serikali kupitia mamlaka yake ya TCRA.

Kwa sasa najipanga nitumir ving'amuzi vya strong bure kabisa Kama ilivyokuwa tunatumia nyumbani kwetu.

Nawashauri wengine waachane na mabepari hawa, nikifanikiwa kununua strong au ving'amuzi vingine nitawapa mrejesho.

Zaidi Ni kwamba channel za startimes tena zile muhimu zina stack Sana hasa maeneo ya pembezoni Kama kigamboni hata iweke antena ya nje huwezi ona channel zote kwa position moja, yaani ukielekezea sehemu Fulani Kuna baadhi ya channel zinapotea and vice versa.
 
Hawa wanafiki kabisa.

Siku hizi kifurushi kikiisha wanaondoa hadi local channel zote isipokuwa TBC 1 tu.

Hii ni kwa ving'amuzi vyote vipya na vya zamani.
 
Guys tusiwe wajinga Kama vile tumenatishwa kwa gundi kutumia ving'amuzi vyao vinavyostack.

Tununue King'amuzi cha strong yaani hakuna longolongo hata kidogo
 
Guys tusiwe wajinga Kama vile tumenatishwa kwa gundi kutumia ving'amuzi vyao vinavyostack.

Tununue King'amuzi cha strong yaani hakuna longolongo hata kidogo
Ndg yang, emb naomba ufafanuzi kidogo kuh:king'amuzi cha strong, kwamba ni cha dish ama namna gani na kinafanyaje kazi, ili nichukue uamzi madhubuti.
 
.
Ndg yang, emb naomba ufafanuzi kidogo kuh:king'amuzi cha strong, kwamba ni cha dish ama namna gani na kinafanyaje kazi, ili nichukue uamzi madhubuti.
..ni king'amuzi cha dish kinachotumia satellite, Ni suala la kukinunua Tu Na kujaza frequency then unaangalia channel ukiwa popote pale duniani
 
5000÷30=166.66 Kwa siku
Hahaaahaaaa tu assume wateja wote wa star times wanataka local channel free na hawanunui kifurushi chochote kwa mwezi. Turudi kwa kampuni ya star times walipe kodi kwa serikali, walipie masafa tcra, walipe mishaharaa wafanyakazi wao. Najaribu kufikiri tu. kiukweli 5000 ni hela nyingi kwa familia nyingi masikini lakini tukubali as long as tulikubali kuchange technology kutoka analog kwenda digital lazima kuna gharama zake simple tu unataka kitu bora kuna cost zake.
 
"Ndugu mteja,muda wa kufurahia channeli kwa bure umeisha,lipia 6000 utafurahia chaneli 20 na za ndani kwenye kifurushi cha Nyota,lipia 12000 utafurahia mechi za Real Madrid, Barcelona na mechi nyingine za ICC kwenye kifurushi cha Mambo, piga 0764700800."
 
Kwako wewe Lanfang Liao Afisa Mtendaji Mkuu

Wewe ni mchina Muongo kuliko wachina wote... na Taarifa uliyoitoa ni uongo mtupu.. Hata Kwangu Local Channel zote hazishiki zaidi ya TBC1 pekee... Mitambo yenu ni Digital so huna la kudanganya Watanzania labda kwenu huko uchinani kwanza ungekuwa ushanyongwa.... Natamani nikutukane ila Sheria zetu kali kwetu tu na sio kwenu wageni... Punguza uongo waache watu walalamike na hao watetezi wako unawalipa buku saba nini?
hahaaaa https://jamii.app/JFUserGuide this chinesse
 
3. Na mwisho tungependa kutoa ufafanuzi juu ya suala la StarTimes kuwatoza watanzania ili kutazama chaneli za nyumbani. Si kweli kwamba kampuni yetu inawatoza watanzania ili kutazama chaneli za nyumbani bali huwa zinatokea hitilafu za kimtandao ambazo husababisha baadhi ya chaneli kutoonekana na kisha kushughulikiwa mara moja. Na hali hiyo huwa inajitokeza mara chache ambapo timu yetu makini ya mafundi huitaarifu uongozi ili kuweza kuwafahamisha wateja wetu wapendwa.
 
3. Na mwisho tungependa kutoa ufafanuzi juu ya suala la StarTimes kuwatoza watanzania ili kutazama chaneli za nyumbani. Si kweli kwamba kampuni yetu inawatoza watanzania ili kutazama chaneli za nyumbani bali huwa zinatokea hitilafu za kimtandao ambazo husababisha baadhi ya chaneli kutoonekana na kisha kushughulikiwa mara moja. Na hali hiyo huwa inajitokeza mara chache ambapo timu yetu makini ya mafundi huitaarifu uongozi ili kuweza kuwafahamisha wateja wetu wapendwa.


HAPA WAMEMAANISHA NINI???(
 
Mimi ni mteja wa Startime tokea mwaka 2010 kabla ya kuzimwa analogi,lakini hivi ninavyozungumza wameniachia liTBC lao ambalo huwa silifagilii. Halafu watu wasiwatetee kwa kuwalinganisha na wengine hawa wameingia ubia na Serikali kupitia TBC,kwahiyo hata mitambo wanayotumia ni ya Serikali (tbc) ambayo ni ya wananchi na moja ya masharti yao ni kuacha Local chanels. Kwahiyo watu wasizilinganishe na ma DSTV,TING,GULF, wala na ving'amuzi ambavyo havina ubia na Serikali yetu,wanatumia mitambo yetu hawajasimika mitambo yao kwa maana nyingine tunaweza kusema wanajiendesha kwa kodi yetu. Tanzania - StarTimes
 
Mimi ni mteja wa Startime tokea mwaka 2010 kabla ya kuzimwa analogi,lakini hivi ninavyozungumza wameniachia liTBC lao ambalo huwa silifagilii. Halafu watu wasiwatetee kwa kuwalinganisha na wengine hawa wameingia ubia na Serikali kupitia TBC,kwahiyo hata mitambo wanayotumia ni ya Serikali (tbc) ambayo ni ya wananchi na moja ya masharti yao ni kuacha Local chanels. Kwahiyo watu wasizilinganishe na ma DSTV,TING,GULF, wala na ving'amuzi ambavyo havina ubia na Serikali yetu,wanatumia mitambo yetu hawajasimika mitambo yao kwa maana nyingine tunaweza kusema wanajiendesha kwa kodi yetu. http://en.startimes.com.cn/tanzania/487.htm
 
Mimi natumia dish ila niliambiwa kuwa ninata kiwa kulipia shs 57000 ili niweze kupata local chanel. Nili lipia hiyo hela ambayo ilikuwa ya mwezi mmoja shs 36000 na iliyobakia ni yakufunguliwa local chanel. Sasa wabishe hili niwape uthibitisho
 
ila jaman watatnzania tumezoea mteremko, kha!! kampuni gani ikupe king'amuzi bei rahisi hvyo? bado tena muone bure? m ndo mana nahisi wakatofautisha.kama unataka kuona channel bure, nunua kwa bei kubwa
we mama unaonekana unauhusiano na startime..
mimi nimilipia kifurushi cha uhuru dec 26 natakiwa mpaka muda huu niwe naona channel zote 70 na cha kushangaza leo nikisarch inasema "channel list is empty!" hii manayake nini?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom