Startimes yatoa ufafanuzi kuhusu kuonekana chaneli za nyumbani

belie

JF-Expert Member
Sep 19, 2014
387
260
Julai 14, 2016

UFAFANUZI KUHUSIANA NA HUDUMA ZA STARTIMES

Kampuni ya StarTimes Tanzania kupitia ving’amuzi vyake imejizatiti kuhakikisha watanzania wote wanafikiwa na huduma za matangazo ya dijitali kwa gharama nafuu ambayo kila mtu ataimudu.

StarTimes inajivunia kuwa kampuni iliyoleta mapinduzi ya matangazo ya dijitali nchini tangu kuzimwa kwa mitambo ya analogia kwa mara ya kwanza mwishoni mwa mwaka 2012 na kuifanya Tanzania kuwa mfano wa kuigwa Afrika ya Mashariki.

Hivi karibuni kumekuwa na taarifa zisizo na uhakika wala kufanyiwa utafiti wa kutosha zikisambazwa katika mitandao ya kijamii kwamba StarTimes inauza ving’amuzi na vifurushi vyake kwa gharama za juu ambazo mtanzania mwenye kipato cha chini hawezi kumudu pamoja na kuwatoza wateja wake kutazama chaneli za nyumbani.

StarTimes inapenda kutoa ufafanuzi kwamba si kweli inatoa huduma zake kwa bei ya juu kama taarifa hiyo iliyosambazwa inavyosema.

1. Kwanza kabisa, StarTimes ni kampuni pekee inayouza ving’amuzi vyake kwa gharama nafuu kabisa ambayo mtanzania yoyote anaweza kuimudu. Bei zetu zinaanzia shilingi 22,000/- kwa vile vya antenna na shilingi 86,000/- vya dishi, vyote vikiwa vimeunganishwa na ofa ya mwezi mmoja ya kifurushi cha bure kwa kila mojawapo.

2. Pili, kampuni ya StarTimes ina vifurushi vya gharama nafuu kwa malipo ya mwisho wa mwezi vikiwa na chaneli nyingi na za kuvutia za ndani na nje. Bei ya vifurushi kwa ving’amuzi vya antenna inaanzia shilingi 5000/- huku ving’amuzi vya dishi vikianzia shilingi 8000/- tu.

3. Na mwisho tungependa kutoa ufafanuzi juu ya suala la StarTimes kuwatoza watanzania ili kutazama chaneli za nyumbani. Si kweli kwamba kampuni yetu inawatoza watanzania ili kutazama chaneli za nyumbani bali huwa zinatokea hitilafu za kimtandao ambazo husababisha baadhi ya chaneli kutoonekana na kisha kushughulikiwa mara moja. Na hali hiyo huwa inajitokeza mara chache ambapo timu yetu makini ya mafundi huitaarifu uongozi ili kuweza kuwafahamisha wateja wetu wapendwa.

Mwisho, StarTimes inatoa wito kwa wateja wake na watanzania kwa ujumla kuwa makini na kuzipuuza taarifa za uzushi zisizokuwa na uhakika zinazosambazwa mitandaoni. Taarifa sahihi na za uhakika hutolewa na uongozi wa StarTimes pekee na si vinginevyo na siku zote kukiwa na habari yoyote haitosita kufanya hivyo.

Asanteni kwa kuendelea kutuunga mkono kwa kufurahia huduma na bidhaa zetu.

Lanfang Liao

Afisa Mtendaji Mkuu
 
Attachments

  • IMG-20160714-WA0001.jpg
    IMG-20160714-WA0001.jpg
    101.6 KB · Views: 568
Star Times hawaja wawazi.

Kuna ving'amuzi na dish wanavyo uza kwa promosheni ambavyo vina masharti yake. Mara ya mwisho kununua kutoka kwao walikuwa wanauza dish kwa bei mbili. Bei ya promosheni ni kwamba kama utakuwa hukulipia kwa mwezi husika basi itaonekana channel moja tu ya nyumbani. Ila ukinunua dish kwa bei ya kawaida hata kama hujalipia utaendelea kuona channel zote za nyumbani. Vile vile na ving'amuzi pia.

Haya maneno ni kama ya miezi mitatu iliyopita. Labda kama wamebadili.
 
ila jaman watatnzania tumezoea mteremko, kha!! kampuni gani ikupe king'amuzi bei rahisi hvyo? bado tena muone bure? m ndo mana nahisi wakatofautisha.kama unataka kuona channel bure, nunua kwa bei kubwa
 
JINA la Afisa mtendaji ni la China au! star time ni Nembo. Tunahitaji utafiti China kingamuzi ni dollar ngapi? hadi antenna ni original? hapo majibu
 
sasa we nawe hata aibu huoni, unanunua 22000 bado unasema uone channel bure, dstv au azam sijui unanunua laki na ushee, bado unalipia local channel, :cool:
Point hapa waseme ukweli sio porojo. Ninavyo ving'amuzi vyote DSTV,DIGTEK
na Start Times cha 22,000 na vile vya 50,000 kwenye vibiashara vyangu naujua ukweli
 
Star times ni vema wakawa wakweli,mimi niliwapigia kwa namba yao ya huduma kwa wateja kuwauliza ni kwanini wamenifungia kuona local channel na wamenibakizia TBC pekee,majibu walioyatoa ni kwamba wanafanya maboresho hivyo nikihitaji kuona chennel nyingine za ziada zaidi ya TBC nahitajika kununua kifurushi walau cha 5000.
Hiki wanachoeleza hapa ni mambo ya hovyo kwani sasa nina wiki tatu napata TBC pekee.Sasa haya nimaboresho gani yasioisha.
 
Jamani wamefungaaaaaa,wasikatae.Halafu ni bora wangesema kama wanafunga tujipange,yaan natamani nimzawadie MTU khaaaa.......
 
Mkuu mimi binafsi baada ya copa america na nba season kuisha sijanunua kifurushi chochote na bado channels local zote nazipata. Si kweli kama watu wanavyosema kuwa kuona local tv lazima ulipie startimes.
Usibishe wakati hukagui ving'amuzi kwenye majumba ya watu, mimi leo asubuhi nimeamka nawasha TV king,amuzi kinaniandikia local channel please recharge! nikachoka kabisa, nimezima na kuwasha zaidi ya mara tatu ujumbe ni huohuo, labda kama ni kweli kuna hitilafu waseme hivyo ila kubisha kila jambo si vizuri.
 
Star times ni vema wakawa wakweli,mimi niliwapigia kwa namba yao ya huduma kwa wateja kuwauliza ni kwanini wamenifungia kuona local channel na wamenibakizia TBC pekee,majibu walioyatoa ni kwamba wanafanya maboresho hivyo nikihitaji kuona chennel nyingine za ziada zaidi ya TBC nahitajika kununua kifurushi walau cha 5000.
Hiki wanachoeleza hapa ni mambo ya hovyo kwani sasa nina wiki tatu napata TBC pekee.Sasa haya nimaboresho gani yasioisha.
Halufu watu wanakuja hapa kuwatetea kama vile wanafanya ukaguzi wa ving'amuzi kwenye majumba ya watu, leo ndio balaa wengi wanalia wamefungiwa.
 
Usibishe wakati hukagui ving'amuzi kwenye majumba ya watu, mimi leo asubuhi nimeamka nawasha TV king,amuzi kinaniandikia local channel please recharge! nikachoka kabisa, nimezima na kuwasha zaidi ya mara tatu ujumbe ni huohuo, labda kama ni kweli kuna hitilafu waseme hivyo ila kubisha kila jambo si vizuri.
Kwangu zinaonekana bila kulipia, sasa niseme ni kweli hazionekani?
 
STARTIMES ni wajanja!. Walizuia local chanel kwa baadhi ya mikoa na kuwapigia simu wateja kuwa limetokea tatizo la kiufundi. Waliwataka wateja kulipia sh 5000 ili zirudi. Tatizo waliweke wao, mteja alipe. Kama si wizi, litafutwe neno sahihi la kuhalalisha kitendo hicho.
 
Back
Top Bottom