Startimes yaomba radhi wateja wake

Mmiskiry

Member
Mar 1, 2018
55
21
STARTIMES YAOMBA RADHI WATEJA WAKE.

Kampuni ya StarTimes Media (T) Ltd, imewaomba radhi wateja wake pendwa na umma kwa ujumla kwa kutopata chaneli za bure kwa muda sasa.
Taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi Mtendaji Star Media(T)Wang Xiaobo amesema leo kuwa hiyo imesababishwa na kukosekana kwa elimu na mawasiliano mazuri kuhusu aina ya tofauti za dikoda (ving’amuzi) tulizonazo, ambayo yamesababisha kwa wateja wao kuendelea kulipia chaneli za bure.

"Tunapenda kuwafahamisha wateja wetu kuwa ziko aina mbili za dikoda, ya kwanza ni ile ya Chaneli za bure (FTA) ambayo mteja halazimiki kila mwezi ili kutazama chaneli za bure.
"Na nyingine ni ya chaneli za kulipia, ambayo mteja atatakiwa kulipia kifurushi chake kila mwezi," amesema

Ameongeza kwa wateja wapya, dikoda (ving’amuzi) hizo zinapatikana kwenye maduka yao pamoja na mawakala wao, lakini kwa wateja ambao tayari wameshanunua dikoda (ving’amuzi) za kulipia wanaweza kubadilisha dikoda (ving’amuzi) zao kuwa FTA kwa kutembelea katika ofisi zetu na kupata utaratibu.

Amesisitiza Star Media (T) Ltd, itaendelea kuzingatia masharti yote ya leseni, pia inaufahamisha umma kwamba imekubali kufuata na kutekeleza maagizo ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ikiwamo kulipa faini ambayo tayari imeshaanza.

Pia wanawafahamisha umma wa watanzania kwamba sasa wanaweza kuendelea kufurahia chaneli za bure na huduma zao kwa ujumla.
 
Hapa ni wakae na TCRA wamalizane.. Maana Huwezi Kuniambia Mie nina Kampuni yangu Nikuuuzie Decoder nikupe channel bure.. halafu ninajua Watanzania asilimia 90 hawawezi kuangalia TV za Nje wataangalia Hizo hizo za Bure

Sasa si nitafunga Kampuni
 
Kuna matangazo deilee, kwani anayetumia antenna analipia antenna yake
 
Yaani anatuona hatufikirii kabisa!!! hizo za FTA walianza lili kuziuza, na zina tofauti gani na hizi za kawaida? kinachotakiwa ni channel ama decoder? mbona wana uwezo wa kuzifungia na kuziruhusu? waachie mzigo waache usanii, wa kutulipisha dekoda nyingine ama kujifanya zimeisha hazipo ama kuziuza gali (kama zipo) ili ukate tamaa waendelee kukuandikia ( this channel belongs to local please recharge)Sasa hivi hawana option maana wale aliokuwa anawalalamikia kuwa hawana kibali wameshafungiwa sasa hana pa kutokea, asitoe utetezi mwepesi kana kwamba hatujui masuala ya mawasil
 
Daaa, Nchi hii wananchi wanafanywa mpira wa danadana Sana. Startime wanaubia na serikali na ndipo TBC ilipowekeza, je, kuwekeza kwenye decoder toka mwanzo hili hawakulijua na serikali walio wabia pia hawakulijua na TCRA nao hawakufahamu?
Leo unasema tunadecoder mbili, moja y'all FTA na nyingine kulipia, hebu turudi mwanzo wa matangazo name uuzwaji wa vingamuzi vyao waliwahi kutoa ufafanuzi huu? Hebu ona tunavyojaziwa madecoder ndani ya kampuni moja, huu si ujuha? Aisee kweli mnyime Mtu ELIMU umgeuzegeuze utakavyo.
 
Mi nachangia tu, maana habari nazipata kwenye JF na mitandaoni niliposabuskraibu, na burudani zote nazipata online, so kwa kawaida decoder zinatakiwa zilipiwe na channel zenye malipo kuziona km zile za movies etc ila sio za umma, maana zile hazina kodi kubwa km zile za kuuzwa, sikiliza vizuri au fuatilia mifumo ya malipo ya foreign channel na local channel
 
Hapa ni wakae na TCRA wamalizane.. Maana Huwezi Kuniambia Mie nina Kampuni yangu Nikuuuzie Decoder nikupe channel bure.. halafu ninajua Watanzania asilimia 90 hawawezi kuangalia TV za Nje wataangalia Hizo hizo za Bure

Sasa si nitafunga Kampuni
True..sasa kama dstv,ukiacha za nyumbani zisilipiwe hapa wengi hawatalipia kingamuzi..labda wale wa mpira tu..the same same kwa azam..hizi kampuni zinaenda kufa
 
Kama watanzania wengi waliweza kulipia hizo fta kwenye azam na dstv na hatujawahi kusikia malalamiko yao shida iko wapi sasa??

Na kwa nini tcra na mamlaka husika nyingine zisikae chini ziangalie namna ya kubadilisha hizi sheria kwani azam na dstv wanawateja wengi sana tz na kuwazuia kuonyesha fta kutaziathiri kampuni hizo pamoja na kuleta kero kwa wananchi..
 
Tisiiaraei anazuga, kwa kifupi tu ni kwamba wametengenezewa soko la visembuzi
 
Hapa ni wakae na TCRA wamalizane.. Maana Huwezi Kuniambia Mie nina Kampuni yangu Nikuuuzie Decoder nikupe channel bure.. halafu ninajua Watanzania asilimia 90 hawawezi kuangalia TV za Nje wataangalia Hizo hizo za Bure

Sasa si nitafunga Kampuni
Ni kweli kama TCRA waliona ni vema kuhama kutoka analogue kuja digital ni lazima tulipie hizi kampuni ni uwekezaji wanahitaji kupata faida kama ilivyo kwenye kampuni za simu mbona huko hamtwambii tukipiga simu za ndani iwe bure?
 
Back
Top Bottom