Yericko Nyerere
JF-Expert Member
- Dec 22, 2010
- 16,987
- 20,271
Ni rahisi ngamia kupenya katika tundu la sindano kuliko Taifa Stars kuifunga Morocco.Mkuu, kazi ipo! Tusubiri miujiza labda.
Kama nigeria wametolewa na egypt nao nje pamoja utemi wao, lolote laweza kutokea. Vijana wanatakiwa waache uoga, uivivu wa dkk 90! wakomae mwanzo mwisho wataweza kuwabania mbona.
Hivi bado kuna mtanzania yeyote mwenye matumaini ya kufuzu kuingia kwenye final baada ya leo, ajitokeze sasa tumsikie.
Just imagine, tunatakiwa kushinda kwa zaidi ya goli 4 kwa bila. Na hii tutasonga mbele endapo tu Algeria wataifunga Central Africa leo. Tusisahau hapa nyumbani Morocco walituchapa goli moja. Tusisahau katika line up yetu ya leo,hakuna Nizar, Nsajigwa na Victor costa.
Mpaka hapo mimi sijaona tunatoka vipi hapo. Tusidanganyane wajameni.........
Nawatakia kila la kheri vijana wetu wanaotupeperushia bendera yetu huko. Nawaombea wawe mabalozi wema na warudi na ushindi.
kwa jinsi unavyowaabudu waarabu nilidhani ungeweka uzalendo pembeni na kutaka waarabu washinde! big up lady!
Mechi inaanza saa nne na nusu usiku kwa saa za Afrika mashariki (22hr30). Tujipe moyo tu na kuonyesha uzalendo lakini ukweli ni kwamba hatuendi popote tunakamilisha ratiba tu!
Mkuu nakusahuri ubadili/rekebisha kichwa cha habari hii...Hivi bado kuna mtanzania yeyote mwenye matumaini ya kufuzu kuingia kwenye final baada ya leo, ajitokeze sasa tumsikie.