Star TV warudia Miss TZ,wachakachua kuzomewa kwa JK

urasa

JF-Expert Member
Aug 12, 2010
434
2
usiku wa kuamkia leo tar 3 oct kituo cha star tv walikuwa wanafanya marudi ya shivdano la miss tz 2010,kile kipengele cha yule miss aliyezomewa tokana na kumfagilia jk wamekiondoa,hivi wanafanya hayo kwa maslahi ya nani haswa?wanatufanya sisi ni mandondocha?
 
Kazi kweli kweli hata mimi nilikuwa naangalia nikaishia kustaajabu!
 
Tutawafuatilia kila kitu wanachofanya iwe kwenye kampeni zao hata kwenye hizo media zao hadi waache ujinga wao
 
Hadi STAR TV nao wamenunuliwa??? Hee makubwa!! Wangetakiwa wasiedit kitu chochote pale.
 
usiku wa kuamkia leo tar 3 oct kituo cha star tv walikuwa wanafanya marudi ya shivdano la miss tz 2010,kile kipengele cha yule miss aliyezomewa tokana na kumfagilia jk wamekiondoa,hivi wanafanya hayo kwa maslahi ya nani haswa?wanatufanya sisi ni mandondocha?

Labda muda uliotengwa kutangaza hicho kipindi ni mfupi kuliko urefu wa tukio la mchakato wa Miss Tanzania, hivi wakaamua wapunguze urefu wa kipindi. Wakaanza kujadili sehemu gani tukate, kule mwanzo kwenye utambulisho, pale alipoteleza yule mlimbwende na kuanguka, pale yule miss aliyepozomewa, pale mshindi alipopatikana, pale gari ilipotolewa nk; na kuamua waondoe huyo aliyezomewa!!! Ni mawazo tu, ila Mkuu wa Star TV ana jibu la uhakika, nashauri wana JF walioko Mwanza wamfuatilie.
 
STAR TV inamilikiwa na kada wa CCM Anthony Diallo.

labda huyo mlimbwende asingezomewa hicho kipengele kingekuwa kinarudiwa kila siku.
 
Hata kama wamechakachua, lakini wamechelewa kwani kila mtu aliona live.......zaidi wanazidi kuweka kumbukumbu za watu vizuri kuhusiana na tukio lile.
 
Jamani kwani hamfahamu kuwa STAR TV na RADIO FREE AFRICA ni mali ya kada maarufu wa CCM Mzee DIALLO???. Hivyo si ajabu kutokea hayo yaliyotokea.
 
Hata mimi kabla ya kuona marudio yao sikuwahi kufikiri kwamba kuna-miss aliongea upuuzi kiasi kile..ila nikashangaa anachekacheka halafu wakamkata kumbe baadae alizomewa?
 
Labda muda uliotengwa kutangaza hicho kipindi ni mfupi kuliko urefu wa tukio la mchakato wa Miss Tanzania, hivi wakaamua wapunguze urefu wa kipindi. Wakaanza kujadili sehemu gani tukate, kule mwanzo kwenye utambulisho, pale alipoteleza yule mlimbwende na kuanguka, pale yule miss aliyepozomewa, pale mshindi alipopatikana, pale gari ilipotolewa nk; na kuamua waondoe huyo aliyezomewa!!! Ni mawazo tu, ila Mkuu wa Star TV ana jibu la uhakika, nashauri wana JF walioko Mwanza wamfuatilie.

Hicho kipengele hakikutakiwa kuchakachuliwa kilikuwa cha muhimu sana
 
Jamani kwani hamfahamu kuwa STAR TV na RADIO FREE AFRICA ni mali ya kada maarufu wa CCM Mzee DIALLO???. Hivyo si ajabu kutokea hayo yaliyotokea.

Hiki chama acheni kife kama watu feki kama Diallo ndio wanaitwa makada wa chama!!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom