Star Tv na Tuongee Magazeti

Retired

JF-Expert Member
Jul 22, 2016
43,394
81,235
Inasikitisha kuwa lile agizo la Mwakyembe kuwa visomwe vichwa tu vya habari katika magazeti linatekelezwa katika hali ya kusikitisha na woga. Ni afadhali muda huo mkautumia kwa kitu ambacho ni cha manufaa kuliko kusoma vichwa vya habari tu katika magazeti. Lengo la kupasha habari linakuwa halijatimia hivyo mnapoteza muda tu! Utumie kwa kitu kingine
 
lengo lao limetimia serikali ya nchi hii haitaki watu wake wapate habari kabisa, waliondoa huduma za chanel za bure wakijua wengi tutaumia, sasa wamekuja na zuio la magazeti kusomwa, ukisema hata vichwa vya habari visisomwe ndio itakuwa shangwe kabisa serikalini, nchi pekee ambayo habari ni anasa.
 
Sasa mbona kama ina back fire, maana hata vile vichwa vya habari vinavyomhusu mtukufu raisi navyo wanasoma namna hiyo?mfano ishu ya mchanga may be habari ingemsifia raisi lakini kwa maamuzi ya kusoma vichwa tu basi inaishia juu kwa juu. Soon tutasikia wakitengua hili jambo.
 
Back
Top Bottom