Star tv na mahojiano hovyo

Star tv na mahojiano hovyo

Nawashangaa sana kwa hicho mnachokiandika humu kumbuka mmilikiwa chombo hicho ni CCM(Dialo) na pia tukumbuke ni kituo hikihiki kilicho mtumia Mwigulu na Zitto kueneza Propaganda za ule mkanda feki wa Lwakatare na pia juzijuzi Mchange alitumia chombo hiki hiki kuleta porojo zake kuwa viongozi wa CDM ndio huwa wanapanga mauaji hapa nchini na hadi polisi kutamka kuwa watachukua hatua lakini wamefyata.
Hivi mnaweza kutuambia wakati chombo hiki kikieneza uzushi na uongo juu ya CHADEMA na viongozi wake mlitoa comment kulaani kwa kilichokuwa kikifanyika?

Tatizo hapa si kulaani.Mimi nilifuatilia sana mahaojiano yale ya Mchange na Mnyika Star Tv. Sioni kosa la Star Tv hapa. Kwani walichokifanya kilikuwa sawa tu ukizingatia pande zote mbili zilikuwepo. Kilichotakiwa pale ni kujibu hoja za Mchange. Lakini pia mimi binafsi sikupata kumwona Mchange zaidi ya kumsoma hapa JF kwa vile anatumia jina halisi. Ukipewa uwanja kama ule ni vizuri zaidi kuonyesha uwezo wako wa kufikiri na kuchanganua mambo.Nashukuru nilipata kumjua Mchange kwani alichokuwa anakifanya ni cha kitoto sana.Kama wakati yupo Chadema hakuweza kufichua maovu akasubiri atolewe ndipo aanike uovu.Hiki ni kitu ambacho hakikubaliki kwa watu wenye uelewa.Mimi leo hata kama nikathibitishiwa kuwa alichokisema Mchange ni sahihi bado nitapingana nae kwani haukuwa wakati wake tena.Angesema wakati huo ningemwona ni mwenye akili za juu sana.Binafsi nilimdharau zaidi na kuona kuwa Chadema walikuwa sahihi kuwatoa watu kama hawa. Hakuonewa hata kidogo.
 
Back
Top Bottom