Baraghash
JF-Expert Member
- Dec 18, 2012
- 2,713
- 1,790
Jana asubuhi kwenye StarTV katika kipindi cha Tuongee asubuhi, chenye mada " sakata la Sukari" upande wa Dsm, alialikwa Mchambuzi wa mambo ya uchumi na siasa , aliebatizwa jina na mwenyekiti mwenza, kuwa "mzee wa data" Renatus Mkinga.
Katika muendelezo wa majadiliano, mara kwa ghafla na jazba,akatoka kwenye mada, akaanza kuisakama Zanzibar, kwa ruhusa ya muongozaji, Nd.Yussuf, kwa lugha ya kifedhuli, kiburi na isio na staha kwa Rais mstaafu wa Zanzibar Dr. Salmini Amour na utwala wake uliodumu miaka 10
Mkinga huku akiongozwa na mtangazaji Yussuf Kamoto alisema " Zakaria alimtia mfukoni Rais wa Zanzibar Dr Salmin Amour na utawala wake na alikuwa halipi kodi .......Zanzibar kuna maghala mengi ( wakati huu) yanayoficha sukari ya nyumbani na viwandani , iliokwisha muda wa matumizi........wanaichanganya na halafu kuileta bara wakijua kuwa ni sumu kwa binadamu "
Ya Zakaria na mwachia mwenywe kama atamuomba Mkinga kuyathibitisha hayo alioyasema, au Serikali ya Zanzibar kutuhumiwa kuwa wanaratibu ufichaji wa sukari na uchakachuaji wake, lakini kinachouma na kukisemea ni kumdhalilisha Rais wetu, jasiri, Komandoo Dr Salmini Amour kusema alitiwa mfukoni.
Hili ni kosa kubwa kufanyiwa Kiongozi wa nchi, huku mtangazaji mdhamini akishabikia ( bila ya kumkemea)
Mtukanaji huyu anaeonekana yuko juu ya sheria na maadili na alishakataliwa na vituo kadhaa kwa tabia yake hiyo
Zanzibar inastahili kuombwa radhi, isipokuwa tu kama StarTV ina sera za kuwatusi viongozi wa Zanzibar na watu wake.
Nakumbuka Mwl. Nyerere alipotuhumiwa kutiwa mfukoni na mgiriki mmoja, sote tunakijua kilichotokea ikabidi hata Rais Makarios wa Cyprus aingilie kati!