Stand Utd ikishuka lawama kwa Nani?

Pukudu

JF-Expert Member
Jan 7, 2011
3,148
2,219
Timu ya Stand Utd ya mkoani Shinyanga iko katika hatari ya kushuka daraja ikiwa na point 28. Na hii ni baada ya kupoteza mechi zke Tatu za ugenini za hivi karibuni.

Stand Utd kama timu zingine zilizokuwa ligi kuu Zina changamoto nyingi kubwa ni kipato. Pamoja na udhamini wa BinSlum kupitia matairi ya Double Star, Exim Bank, Vodacom, Azam TV bado imekuwa na hali ngumu kifedha ambayo imechangia kufanya Vibaya.

Usiku wa leo nimekuwa na hali ya usononi na stress ambayo imenisukuma kuandika uzi huu, kwa upande wangu Stand Utd nilianza kuipenda tangia ikiwa ligi ya wilaya, nimehudhuria mechi na mazoezi kwenye viwanja vya Buluba, Shycom na Sabasaba. Kwa wakazi wa Shinyanga tunajua kashkash timu iliyopitia kuanzia ubingwa wa wilaya, mkoa, hadi kuwa mabingwa wa mikoa na kwenda ligi daraja la kwanza na kupanda Ligi Kuu. Kumbuka stand Utd kwenye ngazi zote ilifanikiwa kupanda Bila kusuasua. Kwa nini tulegee ligi kuu?

Kusuasua kwa timu yetu kunatokana na matatizo mengi je? Ni uongozi? Ukata? Ushirikina? Wachezaji? Siasa? SHIREFA na SHIDEFA au wapenzi na mashabiki?

Kwa upande wangu naona unafiq wetu wadau umechangia na hii ni kutokana na kulea uovu, kukaa kimya na kujipa moyo mambo yatakuwa poa?

NB. hata Stand ikishuka sitashabikia Mwadui F. C ntahamishia mapenzi yangu Boko Haram F. C

Sio kama natafuta mtu wa kumuangushia jumba bovu, Bali naona ni bora tufunguke tuseme ukweli. Nawasubiri wadau aka Wana! Wa Chama la Wana. Najua wake watakaonichukia kwa kusema ntakachosema na nnajua wengi mtanifahamu ila poa tu.
 
Hivi ku upload audio unafanyaje? Ili niweke wimbo wa Stand Utd Chama la Wana!
Nimeamua kujilipua
Ila mengine ntamezea ili kujenga umoja wa timu dhidi ya Ruvu Shooting
 
Lawama kwa wote waliofurahia kupanda daraja kimagumashi na kuwadhulumu Mwadui nafasi yake msimu jana.. Mshale unarudi unarudi porini!
 
Mphamvu tulipanda kwa juhudi zeta na point tulipata baada ya Kanembwe kuharibu mechi walk sio Mwadui
 
Last edited by a moderator:
Tunataka kujua na mechi ziluzouzwa hela iko wapi
 
Figisu zipi wakati shirefa walikuwa upande wa Mwadui na tukibaki ligi kuu haturudii makosa!

SHIREFA kitu gani mbele ya pesa... Uzuri unajua kilichotokea ila unajikaza kisabuni! Mchimba kisima kaingia mwenyewe... Wasalimieni FDL!
 
Tunataka kujua na mechi ziluzouzwa hela iko wapi

Timu gani ambazo pasi na shaka Stend, Ndanda, Polisli na Prison tatu kati hizo nne zitashuka daraja kwa hali ilivyo. Sasa sjui ni nani kati ya hao wanne ataponea tundu la sindano? Mimi sijui!
 
Timu gani ambazo pasi na shaka Stend, Ndanda, Polisli na Prison tatu kati hizo nne zitashuka daraja kwa hali ilivyo. Sasa sjui ni nani kati ya hao wanne ataponea tundu la sindano? Mimi sijui!

Zinashuka timu 2 na kupanda timu nne ambazo ni Toto, Mwadui, African Sports na Maji maji
 
Kama Toto African na Mgambo Shooting tu, hayo ndiyo malipo ya kukamia mechi moja tu nyingine zoote wanaachia. Acha washuke ili wajue ligi haina timu ya Simba pekee.
 
Back
Top Bottom