Stand up comedy: Kenya kuna Eric Omondi, Uganda kuna Kansiime na Bongo kuna nani?

brave one

JF-Expert Member
Feb 5, 2013
4,876
7,366
Stand up comedy Bongo imeanza kupata nafasi kwa kasi lakini kuna changamoto kubwa hasa ya kuwa na wachekeshaji mahiri watu kama.

Mc pili pili yeye anajitaidi lakini anarudia rudia sana aina ya vichekesho vyake kwenye events tofauti.

Idris Sultan huyu jamaa sidhani kama ana talent ya kuchekesha japo kwenye social media anawafuasi wengi, nimeona baadhi ya show zake bado sijaona kiwango.

Stave Nyerere huyu jamaa nae si haba japo anachekesha kwa kuponda watu(anawachamba kama wadada wanavyoita).

Je, mbongo tunaweza kuwa na comedian wazuri waliofikia level za Eric Omondi wa Kenya au Anne Kansiime wa Uganda?

Kati ya hawa yupi anaweza fika huko
- Mpoki
- Idris Sultan
- Stive Nyerere
- Mc Pilipili
- Katarina wa Karatu
- Dogo pepe
- Joti
- Masanja Mkandamizaji
- Bambo
 
Hakuna wa kuwafikia

Hata Evans nani sijui alijaribu akapwaya, na Idrissi akaishia kwenye mahaba ya kutafuta kiki kuliko kutumia kipaji chake kujiendeleza na alifahamika nchi nyingi Africa.

Tabu hawatuli kujiendelezakuna ujuzi wanakosa, watanzania wengi na ni wavivu kutaka kujifunza.
 
Bongo kuna wachumia tumbo tu. Kama vile kila mtu anaweza kujifanya mtangazaji au mwanamuziki hali kadhalika na huo uchekeshaji kila mtu alie na kiumaarufu kidogo mfano wa Idris Sultan nae anajiita comedian kwa vile akiongea pumba mbele ya vitoto vya chuo vinacheka kinafiki kumbe vyenyewe vinazengea hela za chips tu. Msishangae kesho Le Mutuz nae akasema ni comedian.
 
Bongo kuna wachumia tumbo tu. Kama vile kila mtu anaweza kujifanya muigazaji au mwanamuziki hali kadhalika na huo uchekeshaji kila mtu alie na kiumaarufu kidogo mfano wa Idris Sultan nae anajiita comedian kwa vile akiongea pumba mbele ya vitoto vya chuo vinacheka kinafiki kumbe vyenyewe vinazengea hela za chips tu. Msishangae kesho Le Mutuz nae akasema ni comedian.
Le mutuz
 
Hakuna wa kuwafikia

Hata Evans nani sijui alijaribu akapwaya, na Idrissi akaishia kwenye mahaba ya kutafuta kiki kuliko kutumia kipaji chake kujiendeleza na alifahamika nchi nyingi Africa.

Tabu hawatuli kujiendelezakuna ujuzi wanakosa, watanzania wengi na ni wavivu kutaka kujifunza.
kwenye ubunifu wa Tz zero kabisa, wanasahau kuwa dunia ya leo ya teknolojia huwezi kumuiga Kevin Hart kila kitu halafu utegemee kuvutia maana hakuna atakaeona kipya ambacho hawajakiona tayari kwenye Youtube. Kuna video ya waarabu ili trend hivi karibuni ya mchunga mbuzi kuita majina mbuzi wako zizini, hata wiki haikupita Joti nae kasambaza ya kwake ambayo amecopy A to Z and that's as far as being creative goes for us.
 
Tusiwalaumu sana Kuna wengine wazuri kama joti, mpoki ila tatizo lugha ya kingereza na Kuna wengine wanajua lugha ila hawajui kuchekesha kama mc pilipili, evance na idris nikiwatizamaga hata sioni wanachochekesha.
 
kwenye ubunifu wa Tz zero kabisa, wanasahau kuwa dunia ya leo ya teknolojia huwezi kumuiga Kevin Hart kila kitu halafu utegemee kuvutia maana hakuna atakaeona kipya ambacho hawajakiona tayari kwenye Youtube. Kuna video ya waarabu ili trend hivi karibuni ya mchunga mbuzi kuita majina mbuzi wako zizini, hata wiki haikupita Joti nae kasambaza ya kwake ambayo amecopy A to Z and that's as far as being creative goes for us.
Hata mc pili pili ni mtu wa kucopy na kupeste sana ukimsikiliza ni kama anakusimulia kitu unachokijua
 
Hata mc pili pili ni mtu wa kucopy na kupeste sana ukimsikiliza ni kama anakusimulia kitu unachokijua
na hao ndio macomedian wetu. Comedy ni kipaji cha mtu na inapaswa awe na uwezo wa kuchekesha bila kutumia nguvu. Sasa hawa wa kwetu ni kama vile wanajitekenya wenyewe halafu wanacheka.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom