"Stakabadhi ghalani zaiua CCM Kilwa' | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

"Stakabadhi ghalani zaiua CCM Kilwa'

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by mzee wa mawe, Aug 6, 2011.

 1. m

  mzee wa mawe Senior Member

  #1
  Aug 6, 2011
  Joined: Aug 2, 2011
  Messages: 151
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  WANACHAMA 395 wa chama cha mapinduzi (ccm) wilayani Kilwa, mkoani Lindi wamejiunga na CUF baada ya kuchukizwa na mfumo wa stakabadhi ghalani katika ununuzi wa zao la ufuta. Akizungumza jana jijini Dar es salaam, Naibu mkurugenzi wa mipango, uchaguzi na Bunge wa CUF, Shaweji mketo, alisema zoezi hilo lilifanyika wakati wa ziara yake wilayani humo kuanzia julai 23 hadi 29, mwaka huu.

  Mketo alisema jumla ya waliojiunga na chama hicho ni 1,108, huku 395 wakitokea CCM na ambao amewakabidhi za chama hicho. Alisema wanachama 675 hawakuwa na chama na 38 kutoka CHADEMA.

  Mketo alisema wanachama wengi waliojiunga na chama hicho walisema kuwa walikasirishwa na mfumo wa stakabadhi ghalani ambao umekuwa ukiwanyonya wakulima. Alisema kuwa kilio cha wakulima hao ni kutaka uhuru wa kuuza ufuta kwa wafanyabiashara ambao hununua kwa sh 1,700 kwa kilo badala ya vyama vya ushirika vinavyonunua kwa sh 1,000 kama vilivyo agizwa na serikali.
   
 2. m

  mzee wa njaa JF-Expert Member

  #2
  Aug 6, 2011
  Joined: Jun 16, 2011
  Messages: 1,368
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Stakabadhi Ghalani ni uwizi mtupu.................................Nenda Tandahimba ujue.
   
 3. w

  woyowoyo Senior Member

  #3
  Aug 6, 2011
  Joined: Jul 24, 2011
  Messages: 173
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kusini mbona CCM kushiney!
   
 4. n

  ngwendu JF-Expert Member

  #4
  Aug 6, 2011
  Joined: Jun 7, 2010
  Messages: 1,967
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Asante kwa taarifa mkuu ila usitarajie kupata michango humu na hata kama utapata itakuwa ni negative contributions. Subiri mazezeta ya chadema yaione hii chokochoko niliyoianzisha.
  R.I.P CCM very soon
   
 5. m

  mkigoma JF-Expert Member

  #5
  Aug 6, 2011
  Joined: Jul 26, 2011
  Messages: 1,182
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  kule Lindi CUF siwana mbunge suleman bungara
   
Loading...