"Kitendo cha kutuachisha kazi bila kutulipa stahili zetu ni cha uonevu mkubwa, haiwezekani tusaini mkataba mpya kabla ya kulipwa haki zetu za mkataba wa zamani. Hilo tumelikataa ndio maana wameamua kutuachisha kazi na kutakiwa kukabidhi vifaa na nyumba zao ifikapo saa sita Januari 7 na sisi wa mkataba wa kudumu tuwe tumekabidhi nyumba saa sita kamili Januari 28," alisema mmoja wa walimu hao waanzilishi.
Huku wakionyesha kusikitishwa na uamuzi wa uongozi wa shule hiyo na kulalamikia ukiukwaji mkubwa wa haki zao na vitisho, walidai kuwa ndio walioweza kuifikisha shule hiyo hapo ilipo na kuiwezesha kuwa shule bora nchini, lakini wanashangazwa na kitendo cha kutimuliwa bila kujali juhudi zao.