THE BIG SHOW
JF-Expert Member
- Feb 28, 2012
- 16,922
- 13,494
With Reference to the below attachment Mods nitaomba muiweke sawa hebu tuzid kulitizima hili suala la NSSF na wabaya wa Dr Dau kwa muktadha mwingine leo hii...
Maana almost mwez sasa NSSF na Dr Dau kwenye magazeti na hata hapa JF wamekuwa kama Macelebrity wa aina ya pekee kwa kutupiwa kila aina ya uozo,shutuma na kashfa tena zisizo na hata chembe ya ushahid kisha na wao wachafuliwaji wakiwa wameendelea kukaa zao kimyaa badala yake tunaona vyombo vingine vyenye hadhi kujitokeza na kuweka mambo sawa na kuondoa taharuki hiyo kwa jamii...
Tuliona hapo awali CAG akikanusha zile zilizosemwa kuwa ni Reports zake ambazo wazandiki walizisimamia kama ni hoja yao na kuivumisha magazateni na mitandaon kuwa NSSF tena chini ya Dr Dau limekua ni shirika ambalo limehusika katika usimamiz wa hovyo wa miradi na kuhusika katika harufu za ufisadi na ubadhirifu...
CAG Ofc ilitokezea kwa umma na kukanusha habari hizo na kusema kwamba hao ni watu tuh na motives zao...na kwamba wasubiri Genuine CAG Reports zitapelekwa bungeni tena kwa bunge linaloanza leo hii tar 19.04.2016 na kwamba wananchi wawe na subira kwan ukweli utawekwa wazi na vyombo vinavyohusika...
Kama hiyo haitoshi...jana SSRA kama Regulatory Authority wa hiz pension funds imetokezea na kusimama na kuwaeleza watanzania na wanachama wa NSSF ya kwamba wapuuze maneno ya magazetin na mitandaon ambayo kwa kias kikubwa yamejaa hilaa..unafiki...chuki na upotoshaji eti ya kwamba NSSF imechoka na inasuasua katika kulipa mafao ya wanachama wake na hiyo ni kutokana na kufail katika aina za uwekezaji ambao umekuwa unafanya..SSRA inaendelea kusema kwamba NSSF iko imara na hakuna uwekezaji holela katika miradi yake inayoifanya wala ufisadii..
Ifahamike kuwa SSRA kama Regulatory Authority kwa mifuko hiyo ndiyo chombo pekee kinachotoa miongozo ya wapi mifuko hiyo iwekeze na wapi isiwekeze...mifuko hiyo haiwekez kiholela au kwa matakwa yao binafsi...
Either maamuz katika kila kinachofanywa na NSSF kama shirika lazima yapitie kwa board of Directors kabla hayajashuka chini kwa utekelezaji...
NSSFsiyo Dau..Dau was only DG na katibu kwa hiyo Board Of Trustees..lakin inashangaza kwa hawa wachafuz na wazandiki kila wakiigusa NSSF lazima wamguse Dr Dau kana kwamba Dau aliiweka hiyo Nssf chumbani kwake kwa kila nyanja ya maamuz...
Kukosekana kwa ushahid wa tuhuma na character assassination kwa Dr Dau ndiko kunakotufanya wengine tuconclude kuwa Dr Dau anasakamwa na hapendwi na hao wabaya wake kwa sababu tuh ya Islamophobia na chuki za kidini..
Yes.shida kwa Dr Dau ni uislam wake..kwa sababu utakuja kuona kwamba Dr Dau kaanza kusakamwa longtime agoo kabla ya hiz propaganda zake ya kwamba mara ooh kageuza NSSF msikiti...mara Ooh NSSF kuna udini..na mambo kibaoo...
Huu upepo tunaouona kwa sasa utakuja kuona umeanza kuvuma mara tuh baada ya Dau kuondoka hapo NSSFna sasa wabaya wake wakihaha kuhakikisha image yake inachafuka na mambo mengine yoote mazuri ambayo ameyafanya NSSF yanasahaulikaaa...
Tunawaambia kwamba ni rahis sana kusema uongo na unafiki lakin ni vigumu sana kuutetea uongo huoo..
Story hii ya NSSF naa Dr Dau mimi naifananisha kama safina ya Nabii Nuhu...bimaana ya kwamba wale wale waliokadiriki kunyea mavi safina hiyo ndiyo hao hao wanaoshiriki kuisafisha..
Ndug zangu uongo na unafiki haufai..na mbaya zaid wapo watu wanamtukana Dr Dau huku wakitutukana na sisi waislam eti ya kwamba haya sasa Dr Dau kaondoka tuone sasa nyiny kina bwashee mtapata wapi hela ya futari..hayo ni maneno rahis kuyaongea lakin ni maneno yanayojenga chuki na uhasama na kutuaminisha sisi kuwa kumbe tatizo ni udini...
Tunamtahadharisha Dr Magufuli kuwa nchi hii ni yetu sote..na yeye asiingizwe kwenye Trap hii ya udini..sisi tumempigia kura yeye si kwa sababu ya ukatoliki wake..la hasha..tumemchagua kwa kujua kuwa anafaa kuongoza nchi hii kwa haki na usawa..anapofanya maamuz yake aangalie kwenye ukweli na uhalisia..na siyo maneno ya chuki na propaganda...infact wapo watu ambao wao chuki zao za udini zipo waz waz na hawapendi kabisa kuona jamii moja inapata nafas katika ngaz yeyote yenye tija serikalin..
Sisi kama waislam ambao tumemchagua tupo macho kuangalia utendaji wake...asiwe na upendeleo kwa pande yeyote na sisi tutamuunga mkono...
Bado tutazid kuendelea kumpongeza Dr Dau kwa utumishi wake uliotukuka na as a muslim you have made us so much proud kuwa mchango wetu katika jamii hii ni mkubwa na bado tuna heshima kubwa kama vile ilivyo kwa watu wengine...