SSRA, PPF, NSSF hawasomeki

SSRA, PPF, NSSF hawasomeki

Serikali ilipaswa kurizika na kodi wanayopata kwa mwezi tena kodi yenyewe anayokatwa mfanyakazi ni kubwa mno,wakaona haitoshi wakaamua kuchukua tena na hiyo michango ya mlala hoi.
Halafu pesa za kununua wapinzani kwa pesa ipi
 
Dawa ya Sheria kama hizo ni Mahakama. Tujifunze kufungua kesi mahakamani kwa ajili ya kupinga sheria kama hizo, kuaamikia humu mitandaoni aafu mnachagua wabunge wa ccm wengi hakuta saidia[/QUOT sure thing
 
Wazee wetu walipopigania uhuru pamoja na mambo mwingine walidhamilia kuufuta unyonyaji jambo ambalo sidhani Kama kunadalili njema ya kuufuta Labda ni kutokana na kuuenzi Ubepari.Tabaka la wafanyakazi sasa linaingia kwenye ukoloni mamboleo!!
Je,nikweli kunadhamira ya kweli ya kututoa sehemu moja na kutupeleka mbele? Naanza kushuhudia yale matumaini na ndoto zangu kufifia kwasababu tunapoambiwa tunataka kwenda ng'ambo lakini unavunja daraja la kuvukia unatuacha na maswali mengi Sana. Kiukweli namimi nimeanza kupata Shaka na matumaini yangu yanazidi kufifia.
 
Nchi yawiziiikwann wanachukua pesa zetu hakuna sheria ya kukataa kuwekewa pesa si bora uweke kwenye kibubu naapa ukifa watoto wako hawapsti HII pesa serikali ya Tanzania ni wezi
Kuna tatizo mahala,nashangaa hata viongozi wa vyama vya wafanyakazi wapo kimya tu.Fedha zetu zimekua za kufanyia chaguzi zisizo na kikomo na kuna mtu mmoja amekua akitembea na maburunguti ya fedha huku akigawa barabarani apendavyo hizo ni fedha zetu tulizopaswa kulipwa.
 
Kuna tatizo mahala,nashangaa hata viongozi wa vyama vya wafanyakazi wapo kimya tu.Fedha zetu zimekua za kufanyia chaguzi zisizo na kikomo na kuna mtu mmoja amekua akitembea na maburunguti ya fedha huku akigawa barabarani apendavyo hizo ni fedha zetu tulizopaswa kulipwa.

Mkuu hao TUCTA ndo Jipu kabisa,yaani wao na serikali ya wanyonge ni kitu kimoja wanashindwa hata kutetea maslai ya wafanyakazi isitoshe wanakata tu 2%,pesa ya wafanyakazi kukata ruksa lakini kwenye kusimamia maslai ya wafanyakazi hujitenga kabisa, Viongozi katka hii inchi ni wabinafsi sana.
 
Mabadiliko PPF na NSSF imekuwa mwiba mchungu na wenye sumu kali kwa wafanyazi wanyonge yaani ma
Blabla zinazoendelea sasa kuhusu fao la kukosa ajira kama mbadala wa withdrawal, ni geresha tu. Ukweli ni kwamba mifuko ya hifadhi ya jamii ni source nzuri sana ya mapato kwa Serikali.

Ukweli ni kwamba Gvt imeamua makusudi kuwaibia wanachama wa mifuko hii na umma unapumbazwa kupitia vibaraka kama SSRA na baadhi ya wahariri wa media.
Si kweli kwamba Serikali inajali welfare ya mtanzania atakapokuwa mzee wa miaka 60. Ni unafiki mtupu. Wanajua wakikunyima pesa yako sasa utakufa anyway na hivyo kutodai mafao yako. Hivyo PSSSF na NSSF kupendelea kuneemeka kwa pesa za wafu. Cursed SSRA. Why nilazimishwe kusubiri miaka 55 kuchukua pesa yangu ya mafao baada ya kuachishwa kazi? Kwa nini nilazimishwe kuchukua roborobo kupitia ujinga unaoitwa unemployment benefit!!?

Wanasema unapoacha kazi sehemu A uombe kazi sehemu C! Hivi akina Mhagama wanajifanya hawajui ugumu wa kupata ajira Bongo? Kwa uchumi gani? Wanapata wapi courage ya kumwambia mtu aliyeanza kazi akiwa na miaka 49 asubiri hadi miaka 60 ndio achukue pesa zake ambazo kiukweli ni ndogo masikini. Nani atamwajiri mtu mwenye miaka 50?

Nasikia hawajazingatia hata mfumuko wa bei. Ukiwa na laki moja baada ya miaka 10 utakuja kulipwa kiasi hicho hicho. No interest. No nothing. Huu ni mpango wa ovyo kabisa na ni kaburi kwa wanachama wenye mishahara midogo. Mtu ana milioni 2 mnataka kumpa kidogo kidogo eti kusubiri apate ajira nyingine. Si mumpe hela yake akajiajiri?

This is a great injustice and the whole law is bad very bad to low income earners.

Ajira hakuna waacheni wanachama watafute plan B. Kwani lazima kuajiriwa? Watu wapewe pesa zao bwana pindi tu wanapoacha kazi. Mtajitakia laana za bureee wanachama wakifa kabla ya kulipwa fedha zao.
Kwa nini LAPF hujawaweka ktk list yako?
Serikali ya MAGU inatumia hela zetu na kutuangamiza. Serikali ndio imeweka pini.
 
Kila siku sirikali sikivu inasema Mapato yameongezeka kwa sasa wanapata kwa mwezi zaidi ya 1.3T,sasa mbona still mnawaibia walalahoi fao lao la kujitoa? mtu amejidunduliza anajua kamkataba kake kwa muhindi kakiisha anachukua milioni yake mbili anafungua biashara yake kisha Wanasiasa walafi wanazuia asichukue,hiyo ni laana.

Wabunge wanaopitisha sheria kandamizi wao wenyewe wakimaliza miaka mi5 wanachukua mafao yao kwanini wafanyakazi wasichukue? Kama wanawaonea huruma wakiwa wazee,mbona wazee waliopo mitaani hakuna chochote serikali inawasaidia? Mnatumia fedha za walalahoi kununua midrimlaina na kujenga esijiara na standadigeji upuuzi mtupu.

Walipeni mafao yao watu waliochishwa kazi,unemployement benefit ya miezi 6 yanini? Mmewakata 30% ya kodi miaka yote bado tu hamdaridhika? Poleni sana mnaodai mafao, Zitto alipigania sana Bungeni huu upuuzi usipitishwe kwakuwa MABASHITE ya SISIEMU ni Mengi Bungeni yakapitisha UTUMBO.

Nawashauri Mtafuteni Jebra Kambole akawafungulie kesi Mahakamani ya Kupinga huu UPUUZI mchangineni pesa afungue kesi,tafuteni wanasheria wengi mkapinge mahakamani UPUUZI wa WAKOLOMIJE,Kitendo cha kufungua kesi tu ni Ushindi kwenu maana itaonyesha kwamba hamkubaliani na serikali kwa Upuuzi waliofanya na kama inavyojinasibu ni serikali sikivu wanaweza wakawasikiliza lakini mkitulia kimya na kupiga makelele JF nao wanawachukulia simple hivyo hivyo.
 
Binadamu tuko wasahahulifu sana na wabinafsi sana....
Hizo sheria bila shaka zinatungwa na watu ambap marupurupu tu anaweka msingi, bado vijisafari etc....hawezi kumwaza mtu wa chini....
Rais wa wanyonge nae alikubaliana na hili kweli..dah???
 
Kumwambia mtu ati asubiri hadi miaka 55 ndipo alipwe pesa zake mwenyewe mimi sielewi maana yake nini.
Eti zitamsaidia akizeeka!! Toka lini Serikali imeanza kujali wazee wanyonge? Ni ujinga. Ni unafiki. Ni ulaghai.
Hivi Irene kwa nini unipangie when kutumia hela yangu lakini? Mtu asubiri miaka 60 kulipwa laki moja? Kweli? Mna 'raana' nyie. What a lousy, hopeless Gvt......... gang of robbers.
 
Wabunge wa CCM bwana wanapitisha mambo ya kipumbavu. Sheria zingine sio applicable kwa mazingira ya Tz. Yenyewe yanapiga tu makofi. Kama clowns.
Despicable lawmakers
 
Dawa ya Sheria kama hizo ni Mahakama. Tujifunze kufungua kesi mahakamani kwa ajili ya kupinga sheria kama hizo, kuaamikia humu mitandaoni aafu mnachagua wabunge wa ccm wengi hakuta saidia
Huyo judge huko kateuliwa na jiwe, ataambiwa ole wako.....
 
Najua wafanyazi wana hasira sana na hiyo mishirika ya hifadhi ya jamii. Alaaniwe SSRA anayejaribu kula na kuvimbiwa hela ya wafanyazi wanyoooonge. Irene umeishauri vibaya gvt lisheria hilo halina mashiko wala makalio.
 
Hawa wahudumu..... kwanza kama pale millenium tower majibu kama mashetani, halafu Jana nimewasikia walisema wazi kuwa walioachishwa kazikuanzi tarehe 1.8.2018 hawatapewa mafao badala yake watafute kazi mpaka wapate waendele kuchangia
Eneo hili lina huduma mbaya sana unaenda unaambiwa maneno ya kipuuzi wakati ni pesa zako kwanini wanatulazimisha tuweke.pesa zetu kwenye mamifuko yao huu ni wizi wa hali ya juu nchi HII nachelea kusema.inalaana

Lipa kodi kwa maendeleo ya nchi yako.

Weka akiba kwa ajili ya uzee wako.
 
Huo utaratibu wa kusubiri sijui miaka 80 wafanye kwa wenye mamilioni 100 huko. Watu wa hela za mboga kama mil. 50, 20, mil moja hadi laki walipwe haraka. Kadri inavyozidi kuchelewa ndivyo inavyoshuka thamani.
Alas!! SSRA chini ya Irene, PPF chini ya Eliud na NSSF chini ya Erio wanatengeneza 'mv Nyerere ya kimyakimya' !!! If you know what I mean.....

Hakuna kitu PPF ndg uko nje ya wakati.
 
Najua wafanyazi wana hasira sana na hiyo mishirika ya hifadhi ya jamii. Alaaniwe SSRA anayejaribu kula na kuvimbiwa hela ya wafanyazi wanyoooonge. Irene umeishauri vibaya gvt lisheria hilo halina mashiko wala makalio.
Irene Isaka akatafute kazi nyingine kabisa,Upuuzi aliofanya utakuja kumrudia yeye na familia yake,anafurahia Mshahara mnono wa mil 15 kwa mwezi kwa kuumiza walala hoi wanaovuja jasho masaa 12 kwa siku kwa mshahara wa laki na nusu kwa mwezi? Walala hoi wanaokoga vumbi la cement viwandani,walala hoi wanaoiva kwa joto la nondo kiwandani,walala hoi wanavuta hewa ya sumu chini ya ardhi migodini,walala hoi wanaipigwa na jua masaa 12 wakitengeneza miundombinu,hao walala hoi wenye mikataba ya muda mfup wanategemea vimilioni vyao viwili walivyouksanya viwasaidie kanzisha hata biashara ndogo ndogo endapo mkataba ukiisha eti Irene Isaka na Genge lake la WAVIMBA MATUMBO kwa Mishahara ya zaidi ya milioni 10 kwa mwezi wanazuia eti wasipate mpaka watimize miaka 55.

Hivi mtu mlalahoi aliyefanya kazi kwenye mazingira hatarishi,aliyedhuru afya yake kipindi anafanya kazi,unategemea atafikisha miaka 55 wakati anaishi akiwa na stress kwa kumzuia fao lake? Irene kisaka unapata 15m kwa mwezi wewe una uhakika wa kusave zaidi ya milioni 12 kwa mwezi,Tangu uanze kazi SSRA una saving kubwa sana zaidi ya 600m,kwa mlalahoi anayelipwa laki na nusu kwa mwezi ambaye anaishi kwa kukopa kopa mshara akipata analipa madeni tu kisha anakoa tena huyu hata akifanya kazi miaka 10 hana saving hata 100,tegemeo lake ni fao la kujitoa tu ambalo wakati anajiunga na hiyo mifuko aliambiwa atapewa fedha zake akiacha kazi.

Ebu toeni sheria za kikoloni,huko mliko copy na ku_paste hizo sheria wasio na kazi wanalipwa Socila security kila mwezi na sio miezi 6 yenu hewa.
 
Kumwambia mtu ati asubiri hadi miaka 55 ndipo alipwe pesa zake mwenyewe mimi sielewi maana yake nini.
Eti zitamsaidia akizeeka!! Toka lini Serikali imeanza kujali wazee wanyonge? Ni ujinga. Ni unafiki. Ni ulaghai.
Hivi Irene kwa nini unipangie when kutumia hela yangu lakini? Mtu asubiri miaka 60 kulipwa laki moja? Kweli? Mna 'raana' nyie. What a lousy, hopeless Gvt......... gang of robbers.
Ale wa east Africa mpaka wamekufa hawajaona ndururu
 
Back
Top Bottom