SPYWARE NI NINI ?
Computer yako ina pop up blockers , ina pop up killers na kadhalika lakini
unaona popup nyingi sana zinakuja , saa nyingine computer yako haina hata pop up
blockers lakini popup windows zinakuja tu bila kuitwa , zinakutelea website
mbali mbali ambazo wewe hukuchagua zifunguke , lakini zinafunguka kwa lazima au
kilazima .
Kwanza nitaeleza popup window ni nini ( pop up window ni kurasa za tovuti (
webpages ) ambazo hufunguka juu ya page Fulani , kwa kufunguliwa au bila
kufunguliwa , mfano tembelea site hii
www.darmoto.8m.net hapa kuna page ingine
itakuja hiyo ndio popup window .
Kwanini watu wanatengeneza popups ? ni kwa sababu katika kurasa nyingine kuna
nafasi kidogo ya matangazo so wanatumia popups kutangaza bidhaa fulani au
huduma Fulani .
Kwasiku hizi sio popup zote ni nzuri , ukiona website inafungua popup zaidi ya 3
kwa mpigo ujue hiyo sio pop ya kawaida , hiyo ni spyware .
Je spyware ni nini ?
Spyware ni programme ndogo ndogo zinatengenezwa kwa ajili ya kutangaza huduma za
website Fulani au compuni Fulani , hasa za ngono au casino , na wakati mwingine
kupepeleza computer za watu Fulani au shirika Fulani , spyware nyingi
zinapatikana katika chatrooms hasa za IRC au msn na Yahoo chatrooms ndio
zinaingia kwa hapo .
Lakini sana zinatumika katika uchunguzi na upepelezi kutumia spyware mtu wa
marekani anaweza kuamuru computer yako hapa tz ifanye anachotaka yeye .
Spyware haionekani wakati inapoingia sawa na virus , vile vile spyware haiwi
detected na antivirus lazima uwe na spyware remover ndio utowe spyware sio
antivirus.
Utajuje kama kuna spyware katika computer yako ?
1- inafungua popup windows zaidi ya 3 mara kwa mara , hata kama hujafungua
site Fulani yenyewe itafungua tu
2- computer yako inakuwa slow kupita kiasi , hasa katika kufungua site
Fulani kama yahoo.com na hotmail , jua kwamba yahoo ndio site inayofunguka kwa
haraka kuliko site yoyote duniani , mara nyingi teste kwa kutumia yahoo spead ya
internet .
3- utaona computer ina freeze ukifungua baadhi ya page , hii ni kwa sababu
spyware huwa ina dial kama simu , kwahiyo ukifungua site Fulani mfano yahoo ,
spyware itataka kudial wakati wewe unatumia broadbad au dsl na sio dial ,
mchanganyiko hutokea .
4- ukifungua page kama yahoo , ina kuredirect na kukupeleka mfano seach.com
na nyingine ambazo wewe hutaki .
5- ukifungua page mfano google ukiseach kitu Fulani , utaona majibu yanakuja
lakini katika seach engine nyingine na sio google .
Nitatowaje Spyware ?
Kuna programme nyingi watu wanatengeneza na ambazo ni nzuri lakini nyingi
haziendani na matakwa ya watu wengi , nyingi haziko tested na nyingi sio rahisi
kutumia hazieleweki , ila chukuwa zote , kwa sasa hivi adware na windows care ndio programme
nzuri zaidi kwa ajili ya kutowa spyware katika computer yako , unaweza kupata
adaware kupitia hapa
Tucows Download kuna aina nyingi zaidi ila mpaka ujaribu na uone zinazofanya kazi kwamimi nimetumua hizo
Kwa mtumiaji wa kawaida tu , unaweza kuchukuwa adaware 2008 Profesinal , Windows care kuanzia ver 2 au professional na kuna spywareboot ingawa kuna aina mbali mbali za programu za kuondolea spyware hata antivirus ambazo ni all in one nazo zina uwezo wa kukuondolea spyware katika computer uki download programu hizo utakuta maelezo yake jinsi
ya kutumia na kutowa spyware katika computer yako au ukishanstall angalia katika help au unaweza kusearch katika google utapata maelezo zaidi
Nifanye nini nisipate spyware na virus ?
1 Siku zote katika utumiaji wa computer yako hakikisha una firewall , kwa
ajili ya kuzuia intruders wasiweze kupata upenyo katika computer yako au website
yako na kadhalika , kuna firewall za aina nyingi kama mcafee firewall hata
Norton , panda na kadhalika , lakini nzuri na rahisi kuliko zote ni zonealarm
version 4 na kuendelea , kwa kutumia zone alam unaweza kuchakuwa programme ipi
unapenda kutumia na ipi hutumii lakini hizo nyingine hazina function hizo
2 Kama unatumia antivirus hakikisha unafanya update kila baada ya siku 3
au 4 , ili kuweka tools na definition za kisasa zaidi , hizi updates unaweza
kuzidownload na hata kuweka kwa floppy kwa watumiaji wa nyumbani mfano Norton
nenda
Symantec This Page Has Moved hapa utapata definition za kisasa , kwa mcafee
tembelea site yao pia ila nying rahisi ni kudownload scanner moja inaitwa
stinger kutoka mcafee
3 Usitumie programme yoyote ambayo huijui au ambayo hujawahi kusikia
sehemu yoyote , tafadhali uliza watu wa technical support wataweza kukushauri
zaidi kuhusu matumizi ya program mbali mbali kutokana na kazi yako au taaluma
yako
4 Usitembelee site za kuhusu ngono au za bingo na casino ( camari )
spyware nyingi hata virus wengi wanatokana na site hizi , ingawa kuna tovuti za kamari ambazo ni salama au za bahati nasibu
5 Usipende kutumia floppy , cd ,au flash kwa computer zaidi ya 4 ( kama huja scan na kama huamini computer hizo haswa kama imetoka nje ya officer ) , kama
ni kazini na nyumbani ni hivyo tu usiitumie na internet café pia , kati ya
computer 4 utakazotumia 2 zitakuwa na virus au spyware , hiyo ni lazima kama
huna updates za kisasa huwezi kujua kama virus iko mpaka ianze kufanya maajabu .
6 Pia kusoma makala na issue mbali mbali kuhusu utumiaji wa computer na
program mbali mbali kufanya hivi utajua jinsi ya kutatua matatizo mengi
,computer za siku hizi sio lazima kuita fundi wa computer ni wewe mwenyewe tu na
roho yako haina maajabu yoyote ya kukufanya utishike .
7 Cha mwisho jiunge na club mbali mbali wa vijana wa computer kama
techtz : Tanzania Technical Support Forum
Katika group hizo kuna watu wengi wanaweza kukusaidia kwa kujibu maswali yako na
kero zako kuhusu computer , maisha , na mambo mbali mbali tena kwa lugha ya
kiswahili .
Mwisho kabisa ukiona kitu chochote usichoelewa katika computer yako uliza usichoke kuuliza utaeleweshwa na kusaidiwa kwa ukaribu zaidi
Kwa msaada zaidi unaweza kuniandikia