Spika wa bunge awa kituko,sasa aitwa mama posho | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Spika wa bunge awa kituko,sasa aitwa mama posho

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by sulphadoxine, Dec 16, 2011.

 1. sulphadoxine

  sulphadoxine JF-Expert Member

  #1
  Dec 16, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 2,264
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  SAKATA la posho limemtia doa kubwa Spika wa Bunge, Anne Makinda, ambaye alipewa nishani na Ikulu kwenye mazingira ya kutatanisha wakati wa sherehe za miaka 50 ya uhuru, huku wabunge wengi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wakisema tamko la chama chao limewaokoa dhidi ya hasira ya wananchi, ambao kwa maelezo yao "wangeweza kuwapiga mawe mtaani,"l


  Wanaharakati wanaopinga hatua hiyo ya Spika ya kuvunja katiba na kuamua kuongeza malipo ya posho ya kila siku (sitting allowance) ya wabunge kutoka shilingi 70,000 hadi 200,000 bila kupata kibali cha Ikulu, sasa wamempachika Spika huyo jina la "Mama posho."

  Kwa mujibu wa maelezo ya wabunge wengi wa CCM ambao baadhi wametuma salamu za pongezi kwa viongozi wa chama chao, kauli ya Spika Makinda kwamba posho hizo zinaongezwa kwa sababu ya ugumu wa maisha mjini Dodoma ambako Bunge hufanya mikutano yake, kwa kiasi kikubwa imelitenga Bunge na wapiga kura.

  Hii imefuatia tafrani kubwa iliyotokea kwenye sakata hilo, huku wanaopinga suala hilo kuonesha kushtushwa na jambo hili.

  Tayari baadhi ya watu wamekokotoa malipo ya jumla ya waheshimiwa hao baada ya nyongeza hiyo ya kinyemela ya Spika na kusema kuwa malipo ya mwezi mmoja tu ya mbunge ni sawa na mshahara wa mwalimu wa miaka mitatu.

  "Sababu zilizotolewa na Madame Speaker hazijajitosheleza na badala yake zimepandikiza chuki kati yetu, taasisi nzima ya Bunge kwa wananchi. Tusingeweza kueleweka, mtaani walianza kutuona kama wasaliti kwa kweli tulinasa hatukuwa na pa kutokea lakini tunamshukuru Katibu wa Itikadi na Uenezi Nape na chama kwa ujumla kutoa tamko.

  "Tamko lake angalau limeshusha hasira ya wananchi wengi na hata uamuzi wa Rais kutosaini waraka wa ongezeko la posho," alisema mmoja wa wabunge wa CCM kutoka mkoani Ruvuma.

  Mbunge mwingine ambaye ni Waziri amelieleza gazeti hili kwamba haikuwa wakati mwafaka kwa Spika Makinda kushinikiza posho mpya kwa wakati huu hata kama kuna wabunge walitaka afanye hivyo.

  "Uamuzi au ushauri wa chama kwamba si wakati mwafaka wa kuongeza posho kwa wabunge ni wa busara kabisa. Hakuna kilichokosewa na kwa kweli chama kimeonesha ujasiri wa kiuongozi.

  "Chama siku zote kipo juu ya wabunge waliochaguliwa kupitia tiketi yake na hata watendaji wa Serikali kwa hiyo, chama kinao wajibu wa kukosoa kundi lolote la viongozi wanaotoka ndani ya chama. Hapa wamekuwa sahihi, wabunge na Bunge kama taasisi walitaka kujiongezea posho lakini chama kimetoa ushauri kwa kusema hapana. Ni mwelekeo mzuri sana kwa chama," anasema mbunge mwingine.

  Lakini wakati wabunge hao na wenzao wakifurahia CCM kuwaokoa dhidi ya hasira za wananchi, mbunge mwingine amelieleza gazeti hili: "Nakwambia huko mitaani tungepigwa mawe hata kama ni kweli maisha magumu."

  Uamuzi wa CCM kupitia kwa Katibu wake wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, ulieleza kuwa kupandishwa kwa posho za wabunge kwa kisingizio cha ugumu wa maisha si cha msingi kwa sababu ugumu huo haupo kwa wabunge pekee bali hata wananchi wa kawaida, yakiwamo makundi ya wanataaluma kama madaktari, walimu na askari.

  Habari zaidi zinaeleza kuwa, wakati wabunge hao wakiunga mkono uamuzi wa chama chao, Spika Makinda anatajwa kutofurahia tamko la chama chake akiamini limeweka nyufa kati ya chama hicho na wabunge hasa wa CCM.

  Hata hivyo, baadhi ya wabunge wamemlaumu Spika wakisema alizungumzia suala hilo kabla mchakato wake haujafikia mwisho.

  Wabunge wengi wamemshutumu Makinda kwa kushindwa kumudu kiti hicho na kusema kuwa kashfa hii kamwe isingeweza kutokea chini ya uongozi wa Spika wa zamani wa Bunge, Samwel Sitta, ambaye alienguliwa kimizengwe kwenye nafasi hiyo na kupewa cheo cha Waziri wa Afrika Mashariki.

  Katika hali ambayo haijawahi kutokea, CCM imemkemea Makinda kwa kuongeza posho kinyume cha sheria, ikiwa ni mara ya kwanza kwa chama tawala kumpinga hadharani kiongozi wa nafasi ya juu kama Spika ambaye pia ni mjumbe wa Kamati Kuu ya chama hicho.

  “Tunaamini busara itatumika kuachana na jambo hili, kwani kuendelea nalo kunaweza kutafsiriwa ni kuwasaliti watendaji katika sekta nyingine wakiwemo walimu, askari, madaktari na wengineo,” alisema Nape mapema wiki hii.


  “Kwa kuongeza kiwango hicho cha posho kwa wabunge ni kuongeza pengo tofauti ya mapato kati ya wenye nacho na wasionacho katika jamii yetu hasa kwa kuegemea baadhi ya makundi.”

  Nape alieleza kuwa madai ya Spika Makinda kuwa sababu za kuongezeka kwa posho hizo kunatokana na kupanda kwa gharama za maisha mjini Dodoma, hayana msingi na yamesababisha hofu na shaka miongoni mwa Watanzania.

  “Na kwa kweli swali kubwa hapa linakuwa je, maisha yanapanda Dodoma peke yake na kwa wabunge tu?” Nape alihoji.
   
 2. Inkoskaz

  Inkoskaz JF-Expert Member

  #2
  Dec 16, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 6,317
  Likes Received: 437
  Trophy Points: 180
  haki yake!
   
 3. Ndachuwa

  Ndachuwa JF-Expert Member

  #3
  Dec 16, 2011
  Joined: Mar 8, 2006
  Messages: 4,529
  Likes Received: 725
  Trophy Points: 280
  Mwandishi wa bandiko hili atakuwa mfuasi wa NAPE
   
 4. mikatabafeki

  mikatabafeki JF-Expert Member

  #4
  Dec 16, 2011
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 12,837
  Likes Received: 2,101
  Trophy Points: 280
  katumwa na nani kuongeza hizo posho???????????tujiulize hapa.
   
 5. Donnie Charlie

  Donnie Charlie JF-Expert Member

  #5
  Dec 16, 2011
  Joined: Sep 16, 2009
  Messages: 6,575
  Likes Received: 841
  Trophy Points: 280
  unaweza kuta ametumwa na atangaze hivyo alafu m.kwere agome ili kujiongezea maksi kwa watz na Chama Cha Magamba
   
 6. kichomi

  kichomi JF-Expert Member

  #6
  Dec 16, 2011
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 511
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Haswaaa kusudio lao ndio hilo.
   
 7. blea

  blea JF-Expert Member

  #7
  Dec 16, 2011
  Joined: Nov 14, 2011
  Messages: 377
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 45
  njaa na shibe vitu viwili tofauti. hivyo basi hawezi kuwa salama mbele ya wenye njaa kwani ameruhusu wenye sibe waongeze bakuli zao ziwe kubwa zaidi huku wenye njaa wakibakia na vijiko tu tena vile vidogo vya chai
   
 8. MachoMakavu

  MachoMakavu JF-Expert Member

  #8
  Dec 16, 2011
  Joined: Feb 6, 2008
  Messages: 370
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  hizi move ya kupandisha posho alikua peke yake au katolewa kafara?
   
 9. C

  CHIPANJE JF-Expert Member

  #9
  Dec 16, 2011
  Joined: May 1, 2011
  Messages: 313
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Labda kwajili ya starehe zake,mbona wanafunzi wa vyuo vikuu wapo weng sana Dodoma na hajasema waongezewe fedha.Ulafi tu.
   
 10. nyabhingi

  nyabhingi JF-Expert Member

  #10
  Dec 16, 2011
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 10,896
  Likes Received: 5,357
  Trophy Points: 280
  i have two words for money hungry mps:f**k y'all
   
Loading...