Nenda kapike huelewi chochoteNyie mlitaka aombe ushaur kwa mwenyekiti wenu
Utakuwa mlamba miguu ya bashite weweNyie mlitaka aombe ushaur kwa mwenyekiti wenu
😛Spika ya kichina.
Waulize watu wa Kiteto kuhusu SolonAliezoea kula nyama za watu, kamwe hawezi kuacha hata iweje...![]()
![]()
...na aliezoea vya kunyonga, vya kuchinja hawezi...
![]()
![]()
![]()
![]()
![]()
Septemba 7, mwaka huu, Rais John Magufuli alipopokea ripoti mbili za kamati teule za Bunge, zilizochunguza shughuli za uchimbaji na biashara ya Tanzanite na almasi, alisema kuwa Ndugai alimpigia simu alipotaka kuteua wajumbe wa kamati.
Rais Magufuli alisema kuwa Ndugai alimpigia simu kumweleza jinsi alivyo na wakati mgumu kuteua wajumbe wa kamati hizo na kumuuliza ni wajumbe gani awateue.
Sina sababu ya kutilia shaka maneno ya Rais. Hivyo hili ni eneo ambalo Ndugai alijikwaa. Na kujikwaa huko kunalifanya Bunge lionekane halijitegemei wala kujiongoza lenyewe.
Kwanza lazima Ndugai akiri alijikwaa, kwa maana kiongozi wa Bunge hawezi kujadili na Rais kuhusu wajumbe wa kamati za kwenda kuikagua Serikali. Uzuri zaidi ni kwamba Ndugai anajua ni kosa.
Hata Rais Magufuli anafahamu kuwa taasisi za Serikali na Bunge hazipaswi kutengeneza timu ya pamoja.
Bunge na Serikali kuwa timu moja ni usaliti wa desturi za mifumo ya mihimili ya dola, dhambi kubwa iliyopo hapo ni kuisaliti Katiba. Ukishaisaliti Katiba maana yake umewasaliti wananchi.
Hata kama Ndugai alikuwa na nia njema kiasi gani, kitendo tu cha kubainika kuwa alimpigia simu Rais Magufuli ili kupata mawazo yake juu ya muundo wa kamati ni kushusha heshima na hadhi ya Bunge.
Ni vigumu kwa wananchi kuamini kama Bunge linatimiza wajibu wake sawasawa dhidi ya Serikali.
Ni kweli Rais anatamkwa kuwa sehemu ya Bunge, lakini Katiba imemtenganisha kabisa na shughuli za kila siku za Bunge. Rais ni sehemu ya Bunge kwa sababu kutokana na mamlaka yake ya ukuu wa nchi ndiye mwenye kuliitisha, kulizindua, kilihutubia wakati wowote akitaka, na kulivunja baada ya umri wake kutimia au dharura yoyote inapojitokeza.
Hapa pia ifahamike kuwa Rais nafasi yake ya kuliitisha, kulizindua, kulihutubia na hata kulivunja Bunge, inatokana na kofia yake ya ukuu wa nchi na si ukuu wa Serikali. Na kwa vile ni vigumu kutenganisha masilahi ya Rais ndani ya Serikali, ndiyo maana Katiba imemweka mbali na shughuli za kila siku bungeni.
Katika nchi ambazo zimeshika muundo wa Serikali ya Kibunge (Parliamentary Democracy), ambao umetenganisha mamlaka ya ukuu wa nchi na ukuu wa Serikali. Mkuu wa nchi ndiye mwenye mamlaka hayo ya kuitisha, kuzindua na kulivunja Bunge.
Tanzania ambayo mfumo wake ni nusu urais (Semi Presidential), kofia ya mkuu wa nchi na mkuu wa Serikali inavaliwa na mtu mmoja.
Waziri mkuu anakuwa mtendaji mkuu wa Serikali, akifanya kazi chini ya Rais. Hivyo, ni mwiko kwa Bunge kufanya mashauriano na Rais kuhusu utendaji wa kibunge.
Ndugai hajaanguka
Ni mapema kusema Ndugai ameanguka, ila kwa hakika amejikwaa, hivyo hadhi ya Bunge imeingia majaribuni. Hata siku moja Bunge halitakiwi kufanya kazi kwa maagizo au baraka za Serikali. Badala yake Serikali inatakiwa iwe macho kwa kuhofia uwepo wa Bunge.
Mtindo mpya wa Ndugai kushauriana na Rais Magufuli kama utaendelezwa, maana yake Serikali itakosa hofu dhidi ya Bunge na inapokuwa haina hofu na Bunge, tafsiri yake ni kwamba Bunge ni kibogoyo. Ndugai anatakiwa kuhakikisha nchi haifiki huko.
Ndugai anafahamu kuwa Bunge ni la uga mmoja tu wa mijadala, hivyo hoja na ripoti zote za kibunge, husomwa na kuwasilishwa kwa wabunge wote, kisha wabunge kujadili na kuweka maazimio inapobidi.
Lawama za sasa ni kuwa ripoti za kamati teule za Bunge zilizochunguza alamsi na Tanzanite hazikusomwa bungeni, hivyo wabunge wote hawakupata fursa ya kuzijadili, badala yake zikapelekwa kukabidhiwa kwa Rais Magufuli juu kwa juu.
Ripoti za Bunge ambazo zimesababisha Rais awaondoe kazini waziri na naibu waziri hazijajadiliwa na wabunge wenyewe. Hapa bila kupepesa maneno ni kwamba Spika amejikwaa. Yeye akiwa kiongozi wa Bunge amethubutu kuuondolea meno mhimili anaouongoza.
Februari mwaka huu, niliandika makala iliyoongozwa na swali: “Ndugai ni Solon wa Bunge la Tanzania?” Sababu ni namna alivyoliunganisha Bunge katika Mkutano wa Nne na Tano, baada ya Mkutano wa Tatu kuwa na mgawanyiko mkubwa kutokana na kususiwa na wapinzani.
Solon ni mtawala wa Ugiriki ya kale ambaye ndiye mwasisi wa mfumo wa utawala kuendeshwa kwa mawazo ya wananchi walio weng,i alipoanzisha Bunge la Waathens.
Mfumo ambao ndiyo umeleta Bunge, kwamba wawakilishi wa wananchi wanakuwa wasimamizi wa Serikali.
Baada ya Ndugai kutamba anaweza kumzuia Mbunge wa Kigoma Mjini (ACT-Wazalendo), Zitto Kabwe, asichangie chochote bungeni kwa miaka yote ya ubunge wake, kwa kosa la kulalamikia ripoti za kamati kutojadiliwa bungeni, najikosoa kumlinganisha spika huyo na Solon.
Chambuzi safiiSeptemba 7, mwaka huu, Rais John Magufuli alipopokea ripoti mbili za kamati teule za Bunge, zilizochunguza shughuli za uchimbaji na biashara ya Tanzanite na almasi, alisema kuwa Ndugai alimpigia simu alipotaka kuteua wajumbe wa kamati.