Mag3
Platinum Member
- May 31, 2008
- 13,065
- 22,758
Tarehe 12/6/2009, mbunge wa Micheweni (CUF), Shoka Khamisi Juma alitoa tuhuma bungeni kuwa CCM ina tabia ya kuiba shahada za wapiga kura pale inapoona haiungwi mkono. Naibu Spika, Anne Makinda alimtaka kutoa ushahidi kama anao na kumpa muda wa siku saba kuuwasilisha.
Hata hivyo tarehe 17/6/2009, Mh. Shoka Khamisi Juma aliweza kuwasilisha ushahidi wake kwa Spika, Mh. Samwel Sitta. Cha kushangaza, "Ni kweli ushahidi wake nimeupata lakini nimemkabidhi katibu wa bunge apitie kwa makini na kunishauri cha kufanya. Uchambuzi ukimalizika nitatolea mwongozo humu humu ukumbini pengine juma lijalo (juma hili)," alisema Sitta.
Nina kumbukumbu za Spika Sitta kukabidhi ripoti kwa polisi kwa uchunguzi zaidi lakini hatua yake hii imenistua kidogo, kulikoni ?