Spika Sitta..huku wataka na kule wataka - utafunika kombe? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Spika Sitta..huku wataka na kule wataka - utafunika kombe?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mag3, Jul 14, 2009.

 1. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #1
  Jul 14, 2009
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 9,094
  Likes Received: 6,188
  Trophy Points: 280
  Tarehe 12/6/2009, mbunge wa Micheweni (CUF), Shoka Khamisi Juma alitoa tuhuma bungeni kuwa CCM ina tabia ya kuiba shahada za wapiga kura pale inapoona haiungwi mkono. Naibu Spika, Anne Makinda alimtaka kutoa ushahidi kama anao na kumpa muda wa siku saba kuuwasilisha.

  Hata hivyo tarehe 17/6/2009, Mh. Shoka Khamisi Juma aliweza kuwasilisha ushahidi wake kwa Spika, Mh. Samwel Sitta. Cha kushangaza, "Ni kweli ushahidi wake nimeupata lakini nimemkabidhi katibu wa bunge apitie kwa makini na kunishauri cha kufanya. Uchambuzi ukimalizika nitatolea mwongozo humu humu ukumbini pengine juma lijalo (juma hili)," alisema Sitta.

  Nina kumbukumbu za Spika Sitta kukabidhi ripoti kwa polisi kwa uchunguzi zaidi lakini hatua yake hii imenistua kidogo, kulikoni ?
   
 2. Malafyale

  Malafyale JF-Expert Member

  #2
  Jul 15, 2009
  Joined: Aug 11, 2008
  Messages: 11,214
  Likes Received: 3,626
  Trophy Points: 280
  Kwa mujibu wa sheria za nchi hii,kuhujumu uchaguzi ni kosa la jinai na mtu ambaye ushahidi upo akituhumiwa kufanya hivyo inabidi apelekwe polisi na baadae kufikishwa kwenye mahakama za kisheria kujibu shitaka linalomkabili!

  Inanishangaza sana kwa Spika kupokea ushahidi,then kumpa mtu asiye na mamlaka ya uchunguzi eti ndiye achunguze,alitakiwa kupeleka ushahidi huo wa mbunge Shoka polisi ambao ndiyo hasa wenye kazi ya kuchunguza!

  Anyways,Spika Sitta nae ndiyo"walewale",hiyo tuhesabu kama imeisha!
   
 3. Ngisibara

  Ngisibara JF-Expert Member

  #3
  Jul 15, 2009
  Joined: Jan 2, 2009
  Messages: 2,083
  Likes Received: 431
  Trophy Points: 180
  Kule mkoa wa Pwani Kuna bwana mmoja aliwaeleza vijana fulani kuwa ameona kadi za kupigia kura nyingi tu katika ofisi ya serikali (nyingi kanda ya ziwa). akapewa dau ili awahakikishie. basi jamaa akaenda ofisini akazichomoa kiasi na akawapelekea kuwaonyesha jamaa zake, wale baada ya kuhakikisha kuwa ni kweli wakaona ohhhoooo hii ni sooo , Basi wakasubiri giza usiku wakaenda kutupa karibu na ofisi za wenyewe.......CCM. kama mtakumbuka hii iliwahi tangazwa hata redioni kuwa rundo la kadi zimeokotwa karibu na ofisi ya CCM
   
 4. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #4
  Jul 15, 2009
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  uchaguzi wao ...bunge lao
  kwani aliposema uletwe ushahidi alikusudia kuwa atafanya nini? au ndio alitegemea ushahidi haupo?
   
 5. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #5
  Jul 15, 2009
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 9,094
  Likes Received: 6,188
  Trophy Points: 280
  Mpaka dakika hii najiuliza maswali kadhaa:-
  1. Kama Mh. Shoka Khamisi Juma, mbunge wa Micheweni (CUF), angeshindwa kuwasilisha ushahidi, bungeni pangetosha?
  2. Kwa kuwa imeonekana dhahiri kuwa sheria ya uchaguzi kama ilivyopitishwa na bunge imekiukwa, je kuna mtu atawajibishwa ?
  3. Kwa kuwa Tume ya Uchaguzi chini ya Jaji Lewis Makame imeshindwa kusimamia sheria na kufumbia macho uhalifu huu, tutegemee nini 2010 ?
  4. Pamoja na vitendo hivi kufanyika hakuna vurugu zilizotokea, kwa nini serikali inatahayari na kujihami dhidi vurugu kwenye uchaguzi ujao ?
  5. Je baada ya Spika Sitta kukabidhiwa ushahidi wa wazi wa CCM kutokuheshimu sheria ataamua kufunika kombe mwanaharamu apite ?
  6. Je wabunge wa CCM wanaponyamazia vitendo hivi vya uhalifu sasa wanapata jeuri wapi ya kudai wanachukia ukifisadi ?
  7. Tumeshuhudia ya Mugabe Zimbabwe, tumeshuhudia ya Ahmadinejab Iran, tulishuhudia ya Kibaki Kenya - je CCM itatupeleka huko huko ?
  8. Je Jaji Lewis Makame wa Tanzania atafuata nyayo za Samwel Kivuitu wa Kenya au atazinduka na kusimamia uchaguzi wa huru na haki ?
   
Loading...