Spika Ndugai: Ni marufuku Wabunge kushiriki michezo ya kubashiri(betting)

BEHOLD

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2013
Posts
5,057
Reaction score
10,731
Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai amesema kuwa Mbunge yeyote atakayebainika kucheza michezo ya bahati nasibu(Kamari) atapelekwa kwenye Kamati ya maadili ya Bunge

Spika aliyasema hayo wakati Mbunge wa Ulanga, Goodluck Mlinga akichangia na kuongea kuhusu kamari kwa kusema wimbi kubwa la watanzania sasa hivi wanawaza kucheza kamari

Aidha, Mbunge Mlinga ameishauri Bodi ya Kamari nchini(Gaming Board) kutafuta namna nyingine ya kuratibu suala la kamari maana madhara yake ni makubwa kuliko viroba au bangi

MY TAKE:
Sina hakika kama kuna kuna kifungu hicho kwenye kanuni na miongozo ya bunge, Ila bila shaka Spika anatukumbusha kuwa kwa Mujibu wa Biblia na Quraani kubeti kama zilivyo kamari nyingine mfano BIKO na TATU MZUKA ni dhambi.

Lakini pia nimkumbushe Spika kuwa sehemu ya mapato ya kubeti na kamari nyinginezo hulipa kodi serikalini na pesa hiyohiyo ndio huwalipa posho, marupurupu na matibabu India.
 
Na kama kweli ametoa kauli hii, mara moja naomba aiamuru serikali itoe tamko katazo au mwongozo kuwa kubeti ni uhuni ni kitu cha hovyo kisichokuwa na heshima kinacho idhalilisha status ya mtu mchezo usio sahihi mchezo wa kitapeli na ivyo iwaombe na kuwa amuru wananchi wake kuacha mara moja kushiriki michezo hii ya kubet na kwa kuanzia ianze kuwanyanganya leseni ya kuendesha michezo hii haya makampuni ya kubetisha
 
Maisha ya bongo yenyewe ni ku-bet.
Awamu hii watu hata kula mio mitatu ni ku-bet, maana mtu anaamka asubuhi hajui kama siku itapita au lah.
 
Na kama kweli ametoa kauli hii, mara moja naomba aiamuru serikali itoe tamko katazo au mwongozo kuwa kubeti ni uhuni ni kitu cha hovyo kisichokuwa na heshima kinacho idhalilisha status ya mtu mchezo usio sahihi mchezo wa kitapeli na ivyo iwaombe na kuwa amuru wananchi wake kuacha mara moja kushiriki michezo hii ya kubet na kwa kuanzia ianze kuwanyanganya leseni ya kuendesha michezo hii haya makampuni ya kubetisha
mistari tembo, ujumbe sisimizi
 
Kwa sababu haiwezekani mtske kuwaokoa wabunge alafu sisi wananchi tuliowatuma wabunge mjengoni mtuache tukiangamia tukitafunwa na ili zimwi likujualo serikali itoe tangazo na katazo mara moja
 
Hata wabunge walivyomchagua kuwa speaker walibet maana hakukuwa na uhakika kuwa atakuwa speaker mzuri au mbaya maana ukitaka kujua tabia ya mtu mpe cheo..
 
Na kama kweli ametoa kauli hii, mara moja naomba aiamuru serikali itoe tamko katazo au mwongozo kuwa kubeti ni uhuni ni kitu cha hovyo kisichokuwa na heshima kinacho idhalilisha status ya mtu mchezo usio sahihi mchezo wa kitapeli na ivyo iwaombe na kuwa amuru wananchi wake kuacha mara moja kushiriki michezo hii ya kubet na kwa kuanzia ianze kuwanyanganya leseni ya kuendesha michezo hii haya makampuni ya kubetisha
Umeongea vyema mno, big up!
 
Back
Top Bottom