Spika Ndugai: Wabunge mnaotumia bodaboda kuweni makini maana mnapatikana kwa gharama kubwa sana

Linaongea ukweli kwamba hawakufika bungeni kwa haki bali walipitia mlango wa nyuma kwa kutumia pesa za walipa kodi
 
Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai, amewataka Wabunge wanaofanya safari za kuja na kuondoka Bungeni kwa kutumia Bodaboda kuwa makini zaidi na usafiri huo pamoja na Madereva wanaowabeba

Ndugai amesema "Sina shida na usafir huu lakini nawaomba umakini na kuwa na uhakika na huyo Dereva wa Bodaboda kwasababu kupatikana kwenu ni kwa gharama kubwa"

Pia, amesema ni vizuri Mbunge kutafakari Wananchi wake wakimuona kwenye Bodaboda watafikiria vipi.
Ndungai mwenyewe alipatikana kwa shs ngapi kule Kongwa?
 
Sina imani kwamba huyu jamaa yuko sawa kwa head
Shida ilianzia hapa
download.jpeg
 
Tatizo watanzania hawapendi kuelezwa ukweli
Sasa Mbunge utapandaje toyo kama wewe sio mpumbavu.
Lazima ujue toyo ina watu wake
Sasa msipende niingie ndani sana
Wewe elewa Mbunge hapaswi kupanda toyo.
In short lile la Ndugai ni Katazo kama una akili. Akipata tatizo tutamtibu na kodi za wananchi
Wakati Tundu lissu tulikataa kumtibu na kodi hizo hizo na hakupata ajali ya toyo
Kwa maelezo yako mtu wa hadhi unayofikiria,ili asipate matatizo unayoyajua,inabidi apande v8 au magari mengine ya hadhi?
Nadhani ungekua na uwezo kama wa Mungu,hata kifo ungehalalisha kwa baadhi ya watu,wengine ungeamua wasipatwe na mauti.
 
Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai, amewataka Wabunge wanaofanya safari za kuja na kuondoka Bungeni kwa kutumia Bodaboda kuwa makini zaidi na usafiri huo pamoja na Madereva wanaowabeba

Ndugai amesema "Sina shida na usafir huu lakini nawaomba umakini na kuwa na uhakika na huyo Dereva wa Bodaboda kwasababu kupatikana kwenu ni kwa gharama kubwa"

Pia, amesema ni vizuri Mbunge kutafakari Wananchi wake wakimuona kwenye Bodaboda watafikiria vipi.
Uzuri wabunge wapanda bodaboda ni wa ccm. Kina Mdee hawana jimbo wanapatikana kwa misheni town tu
 
Ndugai atupe mchanganuo

Mbunge wa CCM anapatikana kwa shilingi ____

Mbunge wa CDM anapatikana kwa shilingi ____

Mbunge wa ACT anapatikana kwa shilingi _____
 
Kupita bila kupingwa ndio gharama kubwa au wizi wa kura, simuelewi kabisa huyu maiti inayotembea..
 
Spika ana shida.It seems yeye mawazo yake ni kwamba wapo watu wa hadhi fulani nchini ambao hawapaswi kutumia Boda Boda.Huu ni mtimazo segregative ambao hauna budi kukewa kwa nguvu zote.Spika anataka kutuambia wanaotumia Boda Boda wakiwemo wananchi wengi wa kuwaida wao sio watu?Kusema kwamba wanannchi watamuonaje Mbunge anayepanda Boda Boda ni kujaribu tu kuhalalisha statement yake,lakini haifai.

Spika anapaswa kuwaomba wananchi radhi.
Hujamuelewa Spika! Spika anasisitiza umakini zaidi, maana hao madereva wengi wa bodaboda hawajasomea au kupata mafunzo kabla ya kuaanza kuendesha bodaboda,wanafundishana kiyenyeji tu alafu hao wanaingia barabarani kubeba abiria,na ndiyo maana unaona madereva wengi wa bodaboda hawana habari kabisa na Sheria za barabarani wanaona wao haziwahusu kabisa, ndiyo maana hata akikutaa taa nyekundu yeye ata force kupita tu! Na hii ndiyo inasababisha ajali za bodaboda kua nyingi kuliko ajali zingine!! Japokua madereva wazuri wapo pia lakini ni kwa uchache sana!!
 
Kwani kupanda bodaboda ni dhambi jaman..au ni low class citizen transport...? iseeee
Ndugai hataki wabunge wachangie uchumi wa wanyonge wakati ndio huwa wanawpa kura naona anapandisha mabega kwa sababu yeye kapata

Eti wapiga kura wao watawaonaje? watawaona poa tu na kuwashukuru kwa kuwachangia pato lao.Ndugai vipi?
 
Hujamuelewa Spika! Spika anasisitiza umakini zaidi, maana hao madereva wengi wa bodaboda hawajasomea au kupata mafunzo kabla ya kuaanza kuendesha bodaboda,wanafundishana kiyenyeji tu alafu hao wanaingia barabarani kubeba abiria
Yeye Traffic? mtu huwa hapewi leseni bila kupitia Traffic kuidhinishwa
 
Hujamuelewa Spika! Spika anasisitiza umakini zaidi, maana hao madereva wengi wa bodaboda hawajasomea au kupata mafunzo kabla ya kuaanza kuendesha bodaboda,wanafundishana kiyenyeji tu alafu hao wanaingia barabarani kubeba abiria,na ndiyo maana unaona madereva wengi wa bodaboda hawana habari kabisa na Sheria za barabarani wanaona wao haziwahusu kabisa, ndiyo maana hata akikutaa taa nyekundu yeye ata force kupita tu! Na hii ndiyo inasababisha ajali za bodaboda kua nyingi kuliko ajali zingine!! Japokua madereva wazuri wapo pia lakini ni kwa uchache sana!!
Hapana mkuu,statement ya Ndugai kwamba wananchi wa jimbo la Mbunge anayepanda Boda Boda watamuonaje,ni contravesial na sio sahihi.Infact I can also add,ni dharau kwa mwananchi yeyote anayepanda Boda Boda.Huko ni kupandisha mabega.Mkuu Ndugai tunamjua,ni mpandisha mabega,usimtetee.
 
Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai, amewataka Wabunge wanaofanya safari za kuja na kuondoka Bungeni kwa kutumia Bodaboda kuwa makini zaidi na usafiri huo pamoja na Madereva wanaowabeba

Ndugai amesema "Sina shida na usafir huu lakini nawaomba umakini na kuwa na uhakika na huyo Dereva wa Bodaboda kwasababu kupatikana kwenu ni kwa gharama kubwa"

Pia, amesema ni vizuri Mbunge kutafakari Wananchi wake wakimuona kwenye Bodaboda watafikiria vipi.
Mbunge ester bulaya ana bodaboda wake.
 
Spika Ndugai Yuko sahihi kuwapa tahadhari kwani yeye ndiye anajua gharama zinazotumika punde Mbunge anapopata ajali... lakini pia spika yeye ndiye anasaini allowances za usafiri na magari Kwa wabunge wote..na sidhani angependa wabunge wapate matatizo wakati wakiwa Bungeni Kwa uzembe au ubahiri wao...Hii ni Sawa na mzazi kukupatia pesa ya usafiri kwenda shule but mtoto anatumia nauli kununua fegi na kuhonga wenzake na kuamua kudandia malori ya mizigo na mafuta yaendayo taratibu hivyo kuwa rahisi kudandia na kushuka Kwa kuruka.
 
Back
Top Bottom